Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Utaambulia nini kwenye Wazo la Leo?

Utaambulia nini kwenye Wazo la Leo?
Jifunze kutambua vitu muhimu kwenye maisha yako kwanza. Vingine ni vya ziada. Hiyo yaweza kuwa siri ya maisha bora hapa Duniani.
Kupokea na Kutoa ni kama watoto mapacha. Siku zote wanaongozana pamoja haswa wanapokuwa wadogo.
Leo hii tunaishi kwenye Dunia yenye fursa mbalimbali. Fursa hizo zinatubariki na pia tunazitumia kubadili wengine. Ni sawa na kusema tunapokea na pia kutoa.
Haijalishi ni fursa gani iko mbele yako, kama ni kusoma, kazi, kupata mwenza au hata kitu chochote ukipendacho kinachokupatia maarifa kama vile Karakana ya Ubongo, hizo zote ni fursa.
Madhalani tunapenda kuishi. Tufikirie pamoja maswali ya kujiuliza ili tufanye majaribio (Experiments). Tusipende sana kukimbilia majibu maana ni njia rahisi zaidi ya kujiua. Haswa jibu linapokuwa siyo lenyewe
.
Ni vizuri kutambua ya kuwa, hata unapokuwa umeshapata jibu la kwanza, endelea kufikiri ili upate jibu la pili, tatu, nne na kuendelea ili usiwe Mfu. Ipe akili isiyoonekana kazi ya kufanya. Maisha yako unaona jinsi yanavyoboreka.
Je, pamoja na fursa kibao zilizopo ni kwa nini maisha ni magumu?
Kwa nini hatuzioni hizo fursa?
Kwa nini wengi wetu hatuna furaha?
Tumia neno lako la akaunti yako na neno la siri ili uweze kuendelea kusoma.
Du! Mazingaombwe ya kujisomea yameanza mara hii?
Hilo ni jaribio (Experiment).
Umegundua nini?
Tafadhali chukua hatua ya kuwa Mwanachama hai wa Karakana ya Ubongo ili uweze kunufaika zaidi. Vinginevyo utajikuta unakosa maarifa. Kama una chochote cha kusema, tafadhali njoo nione inbox.
Mara nyingi sana akili zetu hazijatulia kwa sababu tunafanya mambo mengi sana.
Fursa zipo nyingi na tunajaribu kuchangamkia kila fursa badala ya kuchagua fursa chache ili tuweze kuweka mkazo pale panapotakiwa. Tukijaribu kuzichangamkia fursa zote tunajikuta tunafanya Mazingaombwe yasiyotufurahisha hata kidogo.
Sasa tufanye nini ili tupate yale Mazingaombwe yanayotufurahisha?
Kwanza inabidi tutambue umuhimu wa kufanya majaribio (Experiments).
Hilo halina mjadala. Hata yale tunayojifunza lazima tukajipige msasa tuone yanaleta faida gani.
Mara nyingi katika maisha tunapigana hata wakati mwingine tunakutana na kile kinachotuumiza au kutukwaza.
Angalia matamshi ya Trump yalivyokwaza watu wengi. Karibu kila mtu anayalalamikia hayo maneno. Kama siyo kulalamika ni kuyakimbia na kuumia moyoni. Kwa lugha nyingine ni ‘fight or fly’.
Katika maisha ya kawaida kukimbia au kupigana na maumivu yako siyo jambo jema.
Maumivu ni sehemu ya maisha katika furaha ya wanadamu. Kisayansi ya Bayolojia maumivu ni sehemu ya mrejesho au feedback inayotuambia kwamba kuna kitu hakifanyi kazi.
Hata simu yako muda wote inaita ndo maana iko hewani.
Japo haipigi kelele kwa milio yake, wale walioitengeneza walijuliza maswali tufanye nini ili kelele ya masaa yote inapokuwa on isiwasumbue watumiaji? Majaribio (Experiments) kibao zikafanyika. Nyingi sana zikashindwa na kutupwa kapuni.
Experiment au jaribio lililoshinda likawa ni kutumia mwanga wa saa kuashiria inaita bila sauti kuonyesha iko hewani. Mtu akikupigia itaita dakika chache ambazo siyo usumbufu mkubwa kama ingekuwa inaita masaa 24! Tuko pamoja!
Bahati mbaya sana yale magonjwa yanayonyemelea watu bila kelele au maumivu kama pressure na kisukari ni hatari sana kama hatupimi afya zetu. Ni tofauti na ugonjwa wa kuharisha ambao utaona kuna kitu hakiko sawa kwa sababu ya safari za maliwatoni na utachukua hatua.
Hata mtoto mdogo akishika wembe vibaya utamkata maana hakuna ishara ya kumuonya kama vile ambavyo stovu ya kupikia itamfanya aungue, akimbize mkono na siku nyingine hatarudia tena. Hapo anakuwa amejijengea tabia kwa sababu ya yale maumivu aliyoyapata.
Kwa maana nyingine maisha yako kama ni ya furaha muda wote utaishia kufanya makosa mengi sana maana ile mirejesho ya maumivu ya kukusaidia kujirekebisha inakuwa haipo.
Lakini ukipata maumivu ya hapa na pale kama Kocha wako ninavyoumia kuona zaidi ya watu 160 lakini waliojiandikisha bado hawajafika hata kumi, ninaendelea kuitumia hiyo kama mrejesho na inanitia moyo na kunipa changamoto ya kufanya kitu kubadili hiyo hali. Matokeo yake ninazidi kuimarika viwango vyangu vya kuishi maisha yenye furaha maana nimejaribu. Nitaendelea kufanyajaribio (experiment) hadi kieleweke.
Mara nyingi muda wa kufa ukifika watu wengi tunajutia yale ambayo hatukufanya kuliko yale ambayo tulijaribu tukashindwa.
Nikukumbushe tena Tarehe 28.01.2018 ni siku ya Karakana ya Ubongo kufanya jaribio (experiment).
Haijalishi tutakuwa wangapi. Hata kama nitakuwa mwenyewe kama Kocha, najua nitaumia ila nitajifunza kitu.
Chonde chonde weka hiyo tarehe maanani na fanya zingaombwe lolote lililo kwenye uwezo wako.
Sijamaanisha ukaribishe maumivu ya aina zote kwenye maisha yako. Beba yale maumivu yenye thamani ambayo itakujenga.
Mimi na jaribio (experiment) yangu ya wenye uhitaji ni kitu cha muhimu kwangu.
Pia Karakana ya Ubongo napata shida kulipia Wataalamu wangu waweke mambo hewani ila ninajua haya maumivu yananibariki kufanya kitu ninachopenda.
Ni suala la muda wana-Karakana wataona kwa kweli Kocha anajiongeza tugeuke ama tuwe gurudumu, injini au hata kioo cha gari ya Karakana ya Ubongo.
Tunataka kufikia malengo.
Wazo la Leo ni lengo langu nimejiwekea. Kuna wakati ninatingwa kupita maelezo.
Inabidi nifanye shughuli nyingine hadi hapo Karakana ya Ubongo itakapoweza kusimama yenyewe.
Hadi itakapofika japo inabidi kuumia. Ila nimeanza kujijengea tabia ya kuandika makala zaidi ya moja ya Wazo la Leo ili kuondoa maumivu ninapotingwa.
Hata pale unapojifunza mbinu na ujanja wa kujiondolea maumivu, mfano Karakana ya Ubongo ifike mahali ife kwa sababu wanachama bado labda hawajaona thamani, unakumbana na mrejesho inbox unaonitia moyo sipotezi muda wangu. Kuna kitu kinatokea. Ni lazima tujikubali kwa yale tunayopitia. Hili suala la Wahitaji lilinigusa siku moja nilipopewa changamoto na Mchungaji nilipoenda kuuaga mwili wa jamaa yangu.
Ninasisitiza kwa sababu sisi binadamu tunapumbazwa na matangazo tunayoona na pia mashuleni tulimopitia kwamba sisi ni bora zaidi ya wengine kwa hiyo hatuna sababu ya kupitia maumivu ya wengine. Tunaweza kudharau na kuendelea na maisha kama kawa. Ponda maisha kufa kwaja.
Leo hii baadhi ya matajiri wa California ambao walikuwa hawajali hali ya hewa ni nini (climate wether) wameanza kuwa wadogo.
Kiwango cha hewa ya Carbon dioxide na kupanda vina vya Bahari ilikuwa haiwahusu kwenye maghorofa yao.
Moto uliowaka California mwaka 2017 umewabadilisha matajiri hao bila kupenda na sasa wameanza kuelewa, tena baada ya kupoteza mali zao. Nayo makampuni ya Bima yameona faida zao zikipungua kwa hiyo inabidi wacheze Mazingaombwe mapya ili kuwe na mshikamano wa kuondoa maumivu waliyoshuhudia ya mwaka 2017.
Yanapotokea majanga kama hayo ya moto huko California hakuna cha vibaka kuiba wala cha maandamano. Watu wanakuwa katika harakati za kuokoa wenzao na mali. Matokeo yake ni kujenga mshikamano wa matabaka yote ya watu. Hakuna cha tajiri wala mwenye uhitaji.
Tunapoelewa maumivu ya wengine hata bila kuyapitia ni njia mojawapo ya kuleta mabadiliko kwa kile unachoweza kukifanya.
Mazingaombwe ya kugeuza maumivu kuwa furaha inakupasa ujue kusudio lako katika maisha haya. Pia utambue furaha inakutembelea pale unapokuwa umeondoa maumivu ya wengine kwa namna moja au nyingine.
Kwa lugha ya wenzetu kuna kitu wanaita pain points.
Katika mazingira ya kiafrika watu bado wanatumia pombe za kienyeji. Hiyo ni pain point.
Kwa nini tusifanye kitu?
Wazungu wamebadilisha vifuniko vya mvinyo, zamani kufungua chupa ya mvinyo ilikuwa ni pain point.
Usijaribu kuzuia maumivu uliyo nayo, Bali angalia namna ya kuyakubali kwanza halafu angalia pain points kama maumivu yako.
Fikiria sasa mbinu za kuyaondoa.
Kila mtu ana kusudio, haijalishi wewe ni nani.....Baba, Mwalimu, Mwekezaji, n.k
Ni bahati mbaya hayo makusudio yetu yanaharibika kwa namna ambayo tumejengewa mifuko ya kazi na usakaji wa fedha.
Maisha yenye furaha ni kile kitu unachoweza kukifanya kwa furaha bila hata kulipwa fedha. Anayeweza kufanya hivyo ni yule anayejua kujipanga.
Ukiangalia baadhi ya watu wa aina hiyo kama Bill Gates, Michael Dell na Mark zuckerberg wote walianzia kwenye mabweni yao.
Ili ujue vizuri kusudio lako anza kujiuliza maswali ni kwa nini unafanya unachokifanya. Kwa mfano, kama unafanya kazi ili upate hela, jiulize hiyo hela ukishaipata ni ya kufanyia nini? Matumizi ya familia au kusaidia wenye uhitaji?
Mathalani maswali ni maisha. Maswali ni uhai, utajikuta unagundua kusudio lako. Ili uwe na uhakika maumivu unayopitia ndo yatakayokupeleka kwenye kusudio lako jitengenezee tabia stahiki. Pia ondoa vizingiti kimoja baada ya kingine. The pain points.
Kuna vitu kama umaarufu. Hizi ni tabia ambazo haziwezi kuwa kusudio. Umaarufu huja wenyewe kutokana na mambo uliyofanya kufikia kusudio lako.
Mara nyingi watu wenye uhitaji wanasahaulika kwa sababu mbalimbali. Mojawapo ni mimi na wewe tunajifungia kwenye maghorofa ya miili yetu. Maghorofa ya mikono tuliyo nayo hata kama hatuioni. Ubinafsi wetu na mengine kama hayo. Tunazo nguvu za kubadilisha haya mambo tukiamua.
Mfano mzuri, ni kujitengenezea tabia za kujali wenye uhitaji. Tukifa mahali tufanye kile kidogo tunachoweza kufanya.
Tarehe 28.01.2018 ni siku maalum pale Muhimbili Karakana ya Ubongo itafanya kitu kwa ajili ya Wahitaji.
Katika maisha kuna mitizamo mingi na tofauti. Unaweza kudhania uko sahihi kutokana na imani na mazingira uliyokulia. Mazingira yanachangia mambo mengi sana katika kumfanya mtu awe alivyo. Mbinu pekee inayoweza kukuokoa ni kufanya majaribio (experiments) mbalimbali ambazo zitakupa fursa ya kujifunza na kukomaa zaidi.
Tangu utotoni tumefundishwa kitu gani ni sawa na kipi si sawa. Hata kama hukufundishwa na wazazi au walezi, mazingira yaliyokuzunguka yalifanya hivyo.
But in reality, the only way you’ll ever improve your life is to throw into doubt what you already know. Umefika wakati wa kupambana na uhalisia wako. Huwezi kujibadilisha kuwa na maisha bora zaidi kama hujitambui pale ulipo.
Fanya majaribio (experiments) mbalimbali.
Jiulize maswali na usiishie hapo. Jichanganye na watu wanaofanya mambo ya kila aina kujenga tabia stahiki.
Kwa hitimisho, ni vizuri kukabaliana na kutokuwa na uhakika (uncertainity) kwa kupuuza yale mawazo kwamba tutajua kitu fulani kwa asilimia zote. Utajikuta unapokea utayari wa kupambana na hali yako.
Mabadiliko yanawezekana. Mabadiliko ni lazima.
Kumbuka hakuna aliyeng’ara na kufikia ndoto yake duniani kwa kujilimbikizia mwenyewe na kuwa mchoyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...