Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Siri ya Maisha ni nini?

Siri ya mafanikio inaishi wapi?
Wewe unajitambua?
Muda wako wa kujiweka huru umefika.
Ninakuweka huru kuanzia sasa.
Je, uko tayari?
Anza na maswali haya:
1) Huwa unalisha tumbo lako kila siku?
2) Huwa unalisha ubongo wako kila siku?
3) Huwa unalisha moyo wako kila siku?
Ninakuweka huru kwa kukulipa sarafu yenye pande tatu kwa majina yake ni:
#1. Jana yako
#2. Kesho yako
#3. Sasa yako
Mwendo wa jaribio (experiment) Kwanza.
Leo ni leo.
Anza kutembea kuelekea kwenye mafanikio yako.
Unaijua njia?
Anza kutembea kwa miguu yako miwili. Kama huna miguu na uanze kufanya kile unachoweza utoke hapo ulipo hadi sehemu nyingine.
Tembea kama vile maisha yako yote yanategemeana na kutembea huko.
Kiuhalisia kutembea kwako ndo muujiza wa kujiweka huru.
Unashangaa?
Ni hivi:
Miili yetu inashibishwa sumu kibao kwa hewa tunayopumua na vyakula tunavyokula. Hewa ina Carbon dioxide kutoka kwenye moshi wa magari (pollution) na viwanda.
Vyakula vina dawa za mimea(pesticides).
Itapendeza kama tutaweza kuzitoa sumu hizo kwenye miili yetu.
Mazoezi ni sehemu ya kuondoa sumu mwilini.
Ukitembea kwa miguu yako ni zoezi moja zuri sana linalofahamika.
Kutembeza damu mwilini mwako kwa kufanyisha moyo mazoezi......kuhema ili damu itembee ni jambo linaloshauriwa hata na madaktari bingwa wa mambo ya ubongo.
Hewa ya Oxygen inapotembea kwa wingi akilini mwako ni jambo zuri maana inakufanya unapata ile mihemko hisia yenye faida na dopamine za kutosha kufanya kazi kwa ufanisi.
Nguvu za akili yako (attention span) ndo zinazoshikilia dunia ya mafanikio yako kwa pamoja. Nguvu zako za mwili zinapelekwa pale damu yako inapoelekezwa. .
Nguvu za damu yako zimeenda wapi?
Kwenye Ubongo?
Kwenye sehemu za siri?
Hebu jikague!
Nguvu ya damu yako jinsi inavyotembea mwilini mwako ndo zinasababisha ufanye yale unayofanya sasa nyingine bila wewe kujua.
Kutembea kwako kwa miguu au mazoezi mengine ya viungo vya mwili yanapotembeza damu yanasababisha ufanisi wa ajabu ndani ya maisha yako( high energy perfomance comes from motion).
Sarafu inayoitwa Ubongo inazo pande tatu kwa majina yake ni:
#1. Jana yako
#2. Kesho yako
#3. Sasa yako
Jana yako na Kesho yako ni pande mbili zinazoonekana ndani ya moyo wako. Sasa yako ni pande sarafu inayoitwa ubongo wako inapodondoka chini bila kuangukia upande wowote yaani Jana yako au Kesho yako.
Unajikuta hujujui wewe ni nani, maana jana yako haipo na wala kesho yako haijulikani.
Kuna wakati mwingine, jana yako inaonyeshwa na wakati mwingine kesho yako inaonyeshwa pia.
Lakini muda wote sasa yako haitabiriki.
Imefichika maana hujui sasa yako itakuwaje ikishapita au itakuwa nini baadaye.
Sasa yako ni mlango. Kwa kupitia mlango wa sasa yako unakutana na mambo mazuri yaliyobeba mafanikio yako.
Sasa yako inawezaje yote hayo?
Unaweza kuamini ya kuwa sasa yako ni mazingira uliyomo?
Kupitia sasa yako unaweza kuwasha moto wa mafanikio yako tena usiozimika tena.
Hata uje upepo na mvua za radi ya aina gani, sasa yako ina nguvu ya kuendelea kuchochea kuni ili huo moto usizimike.
Kitu cha msingi ni kuifanya sasa yako iwe na mapenzi ya kweli na wewe.
Kivipi?
Matamanio yako unaweza kuyafanya kuwa sehemu ya maisha yako.
Matamanio yako ni nini?
Kazi nzuri?
Mke mzuri?
Mume mzuri?
Watoto wazuri?
Nyumba nzuri?
Gari nzuri?
Utajiri wa mali?
Kila kitu humu Duniani ni mwanga. Ili uone vizuri usiku wa jana yako au kesho yako lazima taa yako iwe ni sasa.
Zaidi ya hapo, taa yako sasa ni jicho lako.
Je, umefunga macho yako ukitarajia kuona mafanikio yako?
Kama umefungua macho yako vizuri, sasa yako itaonekana bila
shida yoyote.
Kama umefunga macho, sasa yako haitaonekana na matokeo yake, jana yako na zaidi kesho yako itakuwa ni giza tororo.
Jicho lako likipendana na sasa yako, tena kwa mapenzi ya dhati kabisa, utashangaa kesho yako inatiririka kama mfereji wa maji.
Kwa maana nyingine ukiweza kuing'ang'ania sasa yako, ukayatumia macho yako kuiona sasa yako, ukaweza kuwa mpenzi mwaminifu kwa sasa yako, utaona mageuzi ya ajabu ndani ya kesho yako.
Lakini ukaanza kuangalia jana yako, kesho yako na papo hapo sasa yako kwa mpigo, mwanga wa jicho lako utafifia. Hutafikia viwango vya kuboresha penzi la sasa yako. Matokeo yake hata kesho yako itakuwa haionekani kwa sababu ya mwanga hafifu au giza kabisa.
Inakubidi ujue ya kwamba mwanga wa sasa yako ni kuchukua tahadhari kubwa (undivided attention) kuzuia mwanga usitapanywe sehemu nyingine yeyote.
Kila kitu hapa Duniani kimetengenezwa kwa mwanga.
Usishangae hata sehemu ambazo hazina umeme maendeleo yako nyuma. Sembuse wewe mwanadamu. Mwanga wako ni macho yako ya Ubongo.
Kwa hiyo, utaona vizuri zaidi mafanikio na matamanio yako kama utanzia na sasa yako (tangible) ndo mengine yafuate (intangibles) ambayo ni kama jana yako na kesho yako.
Kuishi kwa lugha ya wenzetu ni live.
Unaweza kuishi maisha mazuri au mabaya. Ukilisoma hilo neno kuishi (live) kwa kurudi nyuma utakutana na neno shetani au ibilisi yaani evil.
Kwa hiyo maisha mabaya tunayoishi ni ukosefu wa mwanga. Pasipo mwanga, hakuna kinachoendelea maana ni giza.
Giza ni kinyume cha mwanga.
Macho ya Ubongo yanakuwa yameshindwa kuona.
Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza.
Mwili wenye magonjwa ni mazingira ya uwepo wa giza. Penye mwanga ugonjwa haukai.
Giza linakuwa ni Gereza lako mwenyewe. Mwili wenye afya ni nyumba ya Nguvu, taa ya Ubongo inamulika na Akili zako zinafanya kazi unayotaka.
Chagua na dhamiria kuitumia sarafu ya Ubongo wako.
Tumia mwanga wa macho yako ili jana yako na kesho yako isikupunguzie mwanga wa kuiona sasa yako vizuri.
Sasa yako ndo inakutengenezea kila kitu unachokitamani kwenye maisha yako. Usiogope hata kama ni kitu gani, miujiza ya mikono isiyoonekana itajileta kwako itakapogundua sasa yako iko tayari kufanya miujiza.
Sisimizi wanajileta wenyewe ukiacha sukari bila kuifunika.
Mikono isiyoonekana ni sisimizi wanaopita katika mwili wa mwanga (light) wakitafuta sasa yako iliyokamilikamilishwa na utamu wa sukari wa matamanio yako ili ikusaidie kufurahia.
Mazingira ya sisimizi kupenda sukari iliyoachwa mahali ndo hata Ubongo wangu na wako unaita sisimizi ambao ni mikono isiyoonekana.
Jifunze! Jipange! Mwaka 2018, tutajifunza na tutaona mabadiliko.
Mwanafunzi akishakuwa tayari Mwalimu anaingia darasani.
Karakana ya Ubongo na Be Ready To Learn ni mahali pa kukutengeneza uwe mwanafunzi ili Mwalimu akija akukute uko tayari. Utaniuliza Mwalimu ni nani?
Anaweza kuwa ni kitabu fulani, mtu fulani, hata Wazo la Leo la siku za nyuma au usoni.
Mwalimu atajitokeza muda wowote wewe utakapokuwa tayari.
Inawezekana Mwalimu wako yuko tayari anapiga hodi lakini umeng'ang'ania sarafu ya jana yako au kesho yako wakati yeye anataka aanze kukumulikia uone sarafu za kutumia kwenye sasa yako.
Tulia kwenye sasa yako kwanza. Hakuna cha kuwahi wala kuchelewa.
Matokeo ya kesho yako yanapokuja jinsi ulivyotarajia au hata kinyume chake huna sababu ya kufurahi wala kukasirika maana umevuna ulichopanda kwenye sasa yako.
Ni sawa na kujiangalia kwenye kioo chako. Utajiona mwenyewe jinsi ulivyo.
Dunia ya leo inasonga mbele kwa kutumia watu wanaoitambua sasa yao inayotengeneza jana zao kama urithi (legacy) na pia kesho zao. Kazi kwako.
Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia, maana najisikia vizuri sana ninapoweza kuwa msaada kwa mtu. Mimi ni mtumishi wenu. Na kwa vile umeamua mwenyewe kunifuatilia, huna budi kujisajili ili upate mengi zaidi.
Kama unalo jambo la kujadili binafsi au kwa pamoja na kufikia suluhisho muafaka kwa maisha yetu unakaribishwa.

Maoni

  1. asante kwa ushauri ntaanza leo

    JibuFuta
  2. Nafraishwa sana na maka yenu wadau

    JibuFuta
  3. Nimefurahi na kujifunza katika makala yenu nitatumia macho yangu Kama mwangaza wa sasa,na kesho katika mafanikio yangu

    JibuFuta
  4. Nimefurahi kwa mafundisho yako na nitayafanyia kazi

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...