Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Unaulisha nini mwili wako?

Unakula chipsi na soda kila siku?
Umeacha kula mboga za majani?
Tabia zako zikoje linapokuja suala la lishe?
Acha kula Msosi usio na virutubisho.
Unaulisha nini ubongo wako?
Hili ndo suala nyeti kuliko lishe.
Acha kusoma magazeti ya udaku!
Acha kutumia Dopamine zako vibaya.
Unaweza kusema wajinga wapumbavu huliwa na wajinga werevu.
Ukiangalia magazeti ya udaku yakishapambwa na picha na vichwa vya habari vya mambo ya udaku, basi kila mtu atakimbilia kulinunua.
Cha kufurahisha zaidi mara nyingi tunachoambulia ni kuangalia picha na umbeya usio na maana yoyote.
Hata msomaji haongezeki thamani hata kidogo.
Tunatumia muda mwingi kusoma magazeti kwa sababu tunataka kujuzwa mambo. Je, ni lazima tujizwe kila aina ya uchafu kama dodoki?
Ni lazima tuwe zoa zoa kama dodoki?
Tunapojuzwa vitu visivyo na maana ni kwa faida ya nani?
Huo muda tunaopoteza nani anatulipa?
Vitu vingi vinavyoandikwa kwenye magazeti ya udaku havidumu. Ukizingatia jinsi ambavyo teknologia imerahisisha mawasiliano, mtu yeyote anaweza kutengeneza na kusambaza habari za udaku.
Ubora wa habari za namna hiyo nayo ni shida nyingine.
Hivi umeshawahi kushangaa na kujiuliza aina ya habari unazoulisha ubongo wako?
Unacholisha ubongo wako ndicho hicho hicho utakachokitoa wakati wa kuongea na pia kuwa na mijadala mbalimbali.
Jiulize, hiki ninachokisoma kitanijenga? Kitanisaidia?
Mfano unapotumia kemikali ya dopamine kumsoma Msanii fulani kafumaniwa inakuongezea chochote?
Mjinga mwerevu anayetengeneza Gazeti la udaku yeye hata akisoma anatengeneza hela.
Ni wajibu wake alisome ili watu wamuone wadanganyike fulani ana mafanikio na kila siku namuona akisoma Gazeti fulani la udaku.
Acha kudanganyika.
Fanya mageuzi.
Soma kitu ambacho kitadumu ndani yako kwa wiki au mwezi au hata zaidi.
Una sababu gani ya kusoma kitu ambacho kinaishia kuwa kama karatasi laini ya chooni (toilet paper)?
Huyo anayeandika habari za udaku ni mjinga mpumbavu anayeuza heshima yake ili apate vijisenti vya kula.
Kwa nini atuharibie yale tunayoweza kufanya?
Leo hii tumezungukwa na taarifa nyingi kiasi kwamba ni lazima tujifunze kuwa makini na uchaguzi wa kitu chenye ubora kwa manufaa ya maisha yetu ya baadaye.
Kuna changamoto nyingi sana leo hii kutokana na jinsi tunavyolishwa udaku na mambo ya aina hiyo:
#1. Kasi ya kusambaza habari kwa njia mbalimbali kama vile copycat zimeongezeka.
Zamani ilikuwa unasubiri hadi gari inayotoka mjini ifike ndo tusome gazeti.
Leo gazeti la umbeya linasafiri kwa sauti au mtandao dunia nzima tena kwa dakika moja. Kuna kila aina ya dhana kama breaking news, alerts na kila takataka inayotumika kuharakisha kupeleka umbea na udaku.
Dopamine tunazitumia kujizawadia mambo ya hovyo hovyo.
#2. Gharama za uzalishaji wa habari zimeshuka kwa kiasi kikubwa.
Kuna watu wanaandika tena bure ili kutangaza biashara zao kwenye magazeti ya udaku kwa sababu yanauzwa bei rahisi na yanapendwa.
Mti wowote ule una mizizi, shina, matawi na majani yake. Ili mtu apate maarifa ni lazima awe kama mti.
Ili maarifa yadumu na yaonyeshe matokeo ni lazima ule virutubisho uweze kustawi vizuri.
Usiishie kulishwa chakula kinachoishia kwenye matawi ya mti ukasahau matawi, mashina na mizizi ya mti wako.
Utakauka hata kabla ya kiangazi. Hata wanaokuandalia chakula hawana muda wa kukupikia vizuri maana wako kila mahali wakisubiri maskendo ya watu mbalimbali yatokee.
Bila kusahau ushindani unasababisha washiriki kushusha viwango na kuharakisha utoaji wa habari za hovyo hovyo
#3. Wanayasansi wana tabia ya kufanya jaribio (experiment) na wanyama hususan Nyani.
Dopamine ya Nyani inachezewa ndio tunagundua mambo mbalimbali.
Hawa wazalizaji wa habari za udaku wanachezea dopamine zetu kama vile Nyani wanaofanyiwa utafiti.
Wanajua wakiweka picha ya Msanii fulani akiwa amevaa namna fulani, ukurasa wa mbele basi mambo ni kuuza Gazeti kwenda mbele.
Tumekuwa watumwa ilijali tuna uwezo wa kutawala mazingira yetu. Unakuta Boss anasimamisha gari kijana muuza magazeti anajua kazi yake, anaficha Gazeti la udaku Ndani ya Daily News ili Boss asionekane kanunua Gazeti la umbea. Kazi kweli kweli!
Kali zaidi hawa Wajinga werevu wanajua namna ya kutuvuta masikio kwa kuunganisha vipande vya habari ili kuwe na muunganiko wa gazeti au toleo lijalo.
Unaachwa kwenye suspense. Hamu ya kusoma toleo lijalo kwa namna yoyote ile.
Kwa mtindo huo wa kutumia dopamine zako kusubiria toleo lingine la udaku, huna nafasi ya kufikiria mambo mengine ya maana.
#4. Watoa habari wengi wanatoa habari za bure na zisizo na mafunzo yeyote kwa sababu ya ushindani.
Ushindani huo unahusisha kompyuta zinatumia umeme, kuna watu na ile mikono ya Kocha isiyoonekana na mambo mengine ya kuhakikisha Wazo la Leo lina ubora unaotakiwa.
Kuna mifumo mingine ya biashara ya matangazo kwa kusambaza habari ambayo inafanya kazi.
Lakini hapa Karakana ya Ubongo na Be Ready To Learn tuna kila sababu ya Kuwa tofauti. Hata tukipata mdhamini tutasema lakini ubora utakuwa pale pale.
Hatutamsulubisha mtu kwa matangazo badala ya mafunzo.
Siku hizi biashara imekuwa ina ushindani kiasi kwamba ili taasisi ziweze kuishi utakuta mwajiri anamlipa mwandishi wa habari ambaye ukurasa wake umesomwa na watu wengi zaidi.
Kadhalika hata mashuleni, Mwalimu analipwa zaidi kwa idadi ya A na B za wanafunzi wake.
Matokeo tunafanya kazi kwa mbinu ambazo siyo sahihi. Tunafaulisha watoto wanaojua kumeza na kutapika kwenye vyumba vya mitihani lakini uelewa ni mdogo.
Hii ni hatari sana.
Baathi ya Makampuni makubwa ya habari yanajua unachokifanya kwenye mtandao. Kama unajifunza namna ya kulea mtoto ukatumia mtandao kujielimisha, siku nyingine unashangaa unaletewa matangazo ya aina hiyo.
Tumeanza kuchezewa na kufanyiwa majaribio (experiments) kama tunavyowafanyia Nyani.
Inabidi tuanze kuamka. Tujue kinachoendelea ni nini?
Kuna siku tutaongea kwa kirefu zaidi ili ujue hakuna free lunch.
Unapewa taarifa unaambiwa usilipie huku nyuma unaacha barua pepe.
Umefika muda wa kuelewa ya kwamba habari za udaku na umbeya hazitakusaidia kufanya maamuzi sahihi.
Habari za aina hiyo hazitakusaidia kujua jiografia ya dunia yetu na wala hazitakuongezea uelewa wa aina yoyote.
Hata akili hisia haitaongezeka.
Kitu pekee ambacho utafaidi ni mihemko ya hisia ambayo inaweza kunadili tabia zako nzuri kuwa mbaya. (Negative influence)
Jenga tabia ya kusoma vitabu zaidi. Makala chache zilizofanyiwa kazi kama Wazo la Leo zitakupa mwanga.
Tuna utaratibu wa kusoma kurasa kumi kila siku hapa Karakana ya Ubongo na Be Ready To Learn.
Soma kitu kinachokuelimisha na kukufanya tufikirie zaidi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...