Unaishi karne ipi?
Uko karne ya 19 au karne ya 21?
Muda wa kujitambua ni sasa?
Hebu tuambatane kwa pamoja Leo.
Sitaki nikuache nyuma.
Leo ninakuwa mkali kidogo.
Ninataka tuamke.
Ninataka tuingie kwenye Bongo zetu tufikirie kwa makini. Hiyo ndiyo kazi yetu hapa Karakana ya Ubongo na Be Ready To Learn.
Ubongo ulio nao ndo kifaa au zana pekee yenye nguvu kuliko computer nyingine yoyote ile unayoijua.
Ubongo wako ndo unaokuwezesha kufanya mambo yote muhimu katika maisha yako. Mifano iko mingi kama vile:
1) Inawezesha mawasiliano, uumbaji wa vitu kama fikra, kufanya tathmini na kupanga.
2) Pia kuna watu ambao wameweza kujifunza na kugeuza Bongo zao kwa kubadilisha jinsi ambavyo ubongo ulikuwa ukifanya kazi karne ya 19 hadi unavyotakiwa kufanya kazi karne ya 21.
Ili uweze kuishi vizuri karne ya 21 ni lazima kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na mazingira yanayotuzunguka.
Ni lazima uweze kutafuta mtu sahihi ambaye kwa pamoja mtaweza kutengeneza siyo tu familia bali mazingira mapya na mazuri zaidi kwa ajili ya kuendeleza kizazi chenye uwezo wa kuondoa maradhi,
ujinga na umaskini.
Leo hii ukisikiliza baadhi ya nyimbo, mashairi na hata mahubiri unaweza kushangaa ni kwa nini mambo ya karne ya 19 bado yanaendekezwa.
Inanisikitisha. Ni lazima tupeleke vichwa vyetu kwenye Karakana za Ubongo ili mambo yarekebishwe.
Tufike mahali tuweze kuyatawala mazingira yetu. Tuondoe hatari zote zilizopo katika mazingira tuliyomo haswa zile za karne ya 19.
Bongo zetu mara nyingi ndo mazingira yetu ya kwanza kabisa.
Je, mazingira yamekaa kaaje?
Yamekaa kishari shari?
Umebeba visasi, visa, hasira, wivu, masengenyo, chuki, hofu na mengine kama hayo?
Kama ndivyo yalivyo mazingira ya ubongo wako basi unatafuta majanga (trouble).
Hata karne ya 19, mazingira ya aina hiyo yalikuwa ni majanga na maafa yake yanafahamika kupitia historia za vita, majanga ya njaa, utumwa na ukoloni.
Kuna gharama kubwa sana ya kuishi katika mazingira yasiyotufaa. Tunakuwa tunaishi kwenye vifungo vya magereza yaliyomo ndani ya mazingira tuliyojitengenezea wenyewe ndani ya vichwa vyetu.
Tunatumia muda mwingi sana kuishi katika mazingira yasiyofaa. Tunatumia muda mwingi sana kufikia mambo yasiyo na tija. Tunatumia muda mwingi sana kuishi kwenye hofu.
Hili Wazo la Leo ni sehemu ya mkakati wa majaribio (experiments) ya uhakika ninayofanya kama Kocha kujiletea mabadiliko yangu binafsi na timu yangu.
Nimeanza kuona mafanikio kwa hatua ninazochukua.
Mfano, nimeanza kupewa fursa nyingi zaidi za biashara.
Kadhalika ukiyafanyia kazi ninayofundisha mabadiliko na mafanikio yatakutafuta wewe.
Haijalishi uko wapi kwenye maisha yako.
Haijalishi umepigika au haujapigika kimaisha maana matumaini ya kupata mafanikio yana nguvu kuliko mafanikio unayoyatafuta.
Leo hii kama lengo lako ni kupata Baiskeli, ukishaipata, ubongo unaanza kufikiria pikipiki, bajaji, taksi, lori hadi Ndege kama umeangalia YouTube ikimwonyesha Reginald Mengi kutoka nyumba ya udongo hadi kumiliki Ndege.
Hivi unajua namna ya kugeuza kelele zilizoko kwenye karakana ya gari kuwa muziki kwenye masikio yako? Muulize Fundi wa Magari atakueleza siri maana yeye anafurahia aina ya huo muziki ambao wewe unaona ni kelele.
Yeye haoni shida. Hizo kelele ni burudani tosha, tena anapata nguvu zaidi ya kufanya kazi zake katika mazingira aliyomo.
Kadhalika makelele yaliyomo ndani ya ubongo wako na mazingira yanayokuzunguka huna budi kujifunza namna ya kuyageuza muziki ili upate dopamine ya kutosha kufanya kazi zako.
Katika hii karne ya 21, maisha yetu yamebadi
lika kupita kiasi. Mazingira yetu yanatubebesha malengo kibao ya upotevu.
Kwa nini?
Sababu zipo nyingi. Ila nitakayoizungumzia leo ni matumizi mabaya ya bongo zetu.
Hatujui uwezo ulioko ndani ya mazingira ya bongo zetu. Inabidi tuingie karakana ya ubongo tukarabatiwe.
Bongo zetu bado hazijafanyiwa mageuzi yanayofaa kuishi karne ya 21 kama jinsi ambavyo ile Filamu ya Matrix inavyotufundisha.
Filamu hii ya Matrix inatufundisha jaribio (experiment) zuri sana jinsi malengo ya upotevu yanavyofanya kazi katika maisha yetu.
Mhusika Mkuu wa Matrix, kwa jina Neo anaonekana ameshtukia aina ya maisha anayoishi. Maisha yasiyo na mpangilio wenye maono mazuri. Filamu hii inatuvutia sana. Tunaipenda kwa sababu bila hata kujua ni kwamba tunajitazama wenyewe kwenye kioo bila kujijua. Inatuonyesha ni jinsi gani maisha ya kisasa ya karne ya 21 yametuletea malengo ya upotevu. Tena yametufanya tumekuwa wajinga wapumbavu.
Inawezekana hukubaliani na mimi, hebu jiulize maswali haya:
1. Je, umeshaweza kuyatawala mazingira (jumuisha na ubongo wako) yako na kuwa mtu wa kiasi?
2. Je, umeshaweza kuyatawala matamanio yako?
Jiangalie kwenye mambo ya kula vyakula vyenye lishe, jiangalie kuhusu mambo ya ngono, na tamaa nyingine tulizo nazo?
Watu wengi tunajua madhara yatokanayo na aina fulani za vyakula, ngono zembe, kutokusoma na pia vinywaji vyenye sukari nyingi lakini tunavitumia bila hata kujali madhara yake kwenye miili yetu.
Tukisoma kama hivi leo, tunajisikia vibaya halafu tunasahau baada ya dakika chache. Tunakuwa huru au tunaingia kwenye mkumbo mpya wa malengo ya upotevu.
Ile dhana ya mkono usioonekana unaofanya kazi kwenye maisha yako una adui mkubwa.
Adui wa mkono usioonekana kwenye maisha yako ni malengo yako.
Lahaula! Unashangaa?
Haya siyo yale malengo uliyojiwekea.
Haya ni malengo mengine kabisa.
Malengo yasiyooneka ila ni malengo ya upotevu.
Haya malengo ya upotevu yamekuwa yakitufanya kurudia mambo tunayojaribu kuyapiga vita.
Mfano kuacha kulewa, ngono zembe, kula vyakula vibaya, soda kila siku, n.k
Hebu jiulize, ni kwa nini hiki kikombe cha mvinyo wa malengo ya upotevu hakikuepuki?
Jibu kwa wanyama kama Nyani linaweza kuwa ni Dopamine na mazingira yao ambapo hawawezi kujitawala wenyewe.
Tutaona jaribio (experiment).
Kwani sisi binadamu je?
Kwa nini tuna uwezo wa kujitawala lakini hatufanyi hivyo?
Ukitaka kujua uwezo mkubwa alionao mwanadamu juu ya kujitawala - angalia pale mwanadamu anapokuwa ndani ya basis na amebanwa na mkojo.
Anaomba basi lisimame anajibiwa hapa si sehemu sahihi ngoja tufike mbele.
Bus linakwenda kama km 5 hivi ndipo linasimama.
Muhusika anashuka na kujisaidia.
Hakuweza kukojoa ndani ya gari japo muda ulikuwa tayari.
Kwa mini?
Jibu ni rahisi Mungu ametupa uwezo wa kujitawala.
Sasa ngono nje ya ndoa, ulevi na mengine mengi yatoka wapi?
Jibu tumezembea kiasi cha kushindwa kuitumia silaha mshususi ya KUJIDHIBITI. KILA MTU ANAWEZA ACHA KUJIENDEKEZA DUNIA HAITAKUACHA SALAMA.
Kwanini hatujifunzi?
Moja ya sababu ni mageuzi na biashara za karne ya 21.
Kila aina ya chakula, kileo, mavazi, sigara, kondomu, n.k vinapatikana.
Haya mageuzi ya karne ya 21 yamekuja ghafla kwa usafiri wa ndege isiyoonekana kwenye rada za akili na bongo zetu. Wachezaji wa mpira wanaita goli la kisigino.
Sote tuna hisia za viwango tofauti tofauti zinazohusiana na chakula, ngono, umaarufu, ushindani, n.k. Hisia za aina hii ndo zilitumika katika mazingira karne ya 19 ili mtu afanikiwe na pia aweze kuacha watu wa kuendeleza kizazi chake.
Hisia zote hizi zina nafasi yake ya muhimu sana katika mazingira yaliyomo kwenye bongo zetu na jinsi ambavyo zinasababisha kuachiliwa kwa kemikali ya Dopamine pale ambapo tunakumbana na mazingira yenye hivi vitu mfano umekutana na chakula kinachonukia vizuri, au binti au kijana mtanashati!
Dopamine inatiririka kwenye ubongo inakusukumia malengo ya upotevu bila wewe kujitambua.
Tatizo ni moja.
Matarajio ya raha au zawadi ya ile mihemko ya hisia inayoletwa na Dopamine ni kubwa kuliko zawadi halisi kutokana na ukweli wa uwezo mkubwa tulio nao wa kuumba vi
tu kwenye bongo zetu.
Ubongo wako unaumba chochote, haujali ni kizuri au kibaya.
Inaaminika ubongo wetu ulitengenezwa hivyo ili tuwe na uwezo wa kupambana siku zote ili tutafute na kugundua mambo mapya na mazuri zaidi.
Ni kwa bahati mbaya karne ya 21 ilileta mageuzi ambayo hayakutuandaa kukabiliana nayo. Matokeo yake kumetokea madhara mengi ya kiafya, kisaikolojia, kitabia na mengineyo.
Tunaweza kufurahi, Wazo la Leo, Karakana ya Ubongo na Be Ready To Learn ni sehemu ya mchakato wa kurekebisha mambo kama hayo ili kurejesha kila kitu mahali pake. Usisahau ya kuwa Mimi Kocha na Rafiki yako, tutashirikiana ila wewe ndo una mamlaka ya kuutawala ubongo wako.
Hapa nitakupatia mbinu za kutumia.
Tumalizie na jaribio (experiment) la Nyani.
Kuna nyani walikuwa kwenye hifadhi yao wakapewa matunda wakala.
Utamu wa yale matunda ulisababisha Nyani watokwe na Dopamine kwenye akili zao.
Wale watafiti walipenda kufanya jaribio lao kabla giza halijatanda.
Kwa hiyo waliwasha taa kabla ya kuwapa Nyani matunda.
Wale watafiti wakaanza kushangaa kadri siku zilivyosogea kiwango cha Dopamine kwa wale Nyani kiliongezeka zaidi bila kuongeza idadi ya matunda.
Wakaamua kuwasha taa bila kuwapa matunda siku moja. Wakagundua wale Nyani mazingira yaliwapumbaza kuachilia Dopamine hata kabla ya tunda maana ilishakuwa mazoea kwao.
Kwa maana nyingine matarajio ya malengo yetu, matarajio ya tabia zetu yana nguvu ya kutuletea chochote tunachotaka.
Tofauti yetu na Nyani ni uwezo wa kuyatawala mazingira yetu hata kama kuna Dopamine nyingi kiasi gani.
Kwa hiyo tuwe watu wa kiasi, tunachokihitaji kikipatikana na tutumie hekima zaidi.
Madhara ya kunywa soda yanaweza kuwa mabaya kuliko hata bia. Hakuna wa kumcheka mwenzake hapo.

Maoni
Chapisha Maoni