Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Utaambulia Nini? Kwa Lugha Ya Wenzetu Ni "What's In It For Me?" Inaendelea...

Akili Hisia (emotional intelligence). Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hi inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka.
Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja?
Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo?
Hii ni sehemu ya pili kuhusu akili hisia jinsi ya kutawala mazingira ya nje kwa kutumia akili hisia kupitia watu wengine.
#4. Hatua ya nne ni Uelewa.
Kushawishi watu wengine waweze kutupatia tunachohitaji au watufanyie kile tunachotaka ni kazi kubwa sana.
Ni lazima tuwe na uelewa mpana ambao ni sehemu ya akili hisia.
Kile kitendo cha kuwa na uwezo wa kumwelewa mtu mwingine katika mazingira ya Dunia ya hisia na kuwachukulia walivyo bila mfarakano ni kazi ya kipekee.
Kwa nini iwe ni kazi ya kipekee?
Kwa sababu lazima utumie mizani kuleta usawa wa kupekee. Mizani itakapoelemea huku au kule tayari ni tatizo kubwa kupita maelezo.
Kuna watu wana hisia shirikishi. Watu hai ni kama madaktari, manesi, walimu na hata wazazi. Wanao uwezo mkubwa wa kubeba hisia za watu wengine wanapokabiliwa na matatizo. Cha ajabu ni kwamba wakizidisha hisia shirikishi kwa watu wengine, huwa wanaadhirika pia.
Katika ufanyaji wa kazi haswa zile ambazo zinahusu utoaji wa huduma, wachungaji, maaskofu, madaktari na Waalimu, hao watu wanaishia kubeba uchovu mzito wa huruma (compassion fatigue).
Hali hiyo isipofanyiwa kazi inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye maisha yao pia.
Ni lazima akili hisia itumike kuhakikisha kila mtu ana uelewa wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kwa wale watoa huduma ambao wanameza hayo maumivu (deadening) ya wale wanaowasaidia ama kwa kutokujali au kutokujua wanaweza kujikuta uelewa wa utendaji wa kuridhisha watu wanaowapa huduma unaisha au kupungua kabisa.
Utawakuta hawana hamu ya kufanya tena kazi zao.
Kuna suluhisho la matatizo kama haya. Kwa lugha ya wenzetu ni affective empathy. Inamaanisha kama mtu wako hasa ndugu au rafiki hana furaha na wewe pia unaweza kutumia akili hisia kuonyesha huna furaha ili umsaidie kurudi kawaida.
Pia, unaweza kupandisha viwango vyako kwa kutumia akili hisia kwa kumwambia mhusika ya kuwa unatambua jinsi anavyojisikia.
Unampa hisia zako bila kubeba maumivu yake. Kwa lugha nyingine ni cognitive empathy.
Kumalizia namna ya kuelewa watu kwa kutumia akili hisia unaweza pia kutumia hisia akili kwa kuelewa tatizo la mtu na ukawa na ujasiri wa kumuuliza mhusika swali, "nikusaidie namna gani?" Hii inapendeza zaidi kufanya.
Ni wajibu wa kila mtu kutumia akili hisia kujua ni mahali gani atumie uelewa wa aina gani ili kupata matokeo stahiki.
Kwa ndugu na marafiki unahitaji affective empathy. Hapo unapata fursa ya kusononeka pale ambapo mtu ana huzuni au kufurahia pale ambapo mtu ana furahia tukio fulani.
Kama uko hospitalini unaumwa tezi dume, daktari au Nesi hawezi kuonyesha masikitiko au kulia mbele ya mgonjwa. Inabidi hapo mgonjwa aambiwe kinachofuatwa kwa kutumia hisia za kuonyesha kujali mgonjwa (cognitive empathy).
Kwa kuongeza upendo na hisia akili unaweza kubadilisha hisia za mtu kama mgonjwa akajisikia vizuri zaidi. Sote tuna uwezo wa kutumia kiasi cha huruma (compassion empathy) tukafanya kazi nzuri zaidi kwa anayehitaji huduma na pia kwa mtoa huduma.
Kwa kufanya hivyo mtoa huduma hataadhirika kwa namna yoyote na ataweza kutoa huduma kwa watu wengi zaidi kama mashuleni, mahospitalini, kwenye mabenki, n.k.
Kwa maana nyingine linapokuja suala la akili hisia, kinachotakiwa kwa asilimia 100 ni compassion empathy.
Akili Hisia ni silaha ambacho Rais wa sasa wa Marekani aliweza kutumia kucheza na hisia za Wazungu wazee hadi akapata ushindi.
Trump aliweza kubeba zile hisia za wapiga kura wake kwa akili na wakamwelewa maana uchumi wa Marekani uliwasahau na wakawa wamebaki nyuma.
Washindani wake hawakuweza kuonyesha ujuzi wa aina hiyo. Ndo umuhimu wa kuwa na akili hisia na kuitumia vizuri kibunifu.
#5. Ujuzi wa Kijamii
Kujifunza kupika au kutengeneza ujuzi wako kwenye jamii iliyokuzunguka ni jambo la msingi kufikia mafanikio unayoyatafuta.
Hebu fikiria mzazi au kiongozi mwenye ushawishi kwa mtoto wake au watu anaowaongoza! Anatumia mbinu gani? Siri kubwa ni kutumia akili hisia kujenga mahusiano mazuri ili kuwe na masikilizano mazuri na pia kufikia malengo.
Ujuzi wa kijamii ni urafiki unaojengwa ili kutoa mwelekeo na kuonyesha njia ya kufikisha watu wanakotaka kufika.
Watu makini kwa kutumia akili hisia wanajua kutafuta mahali pa kuanzia kukubaliana (common grounds) wanapokuwa na makundi ya aina zote za watu.
Utapataje utaalamu au ujuzi wa kijamii?
Fungua macho yako. Angalia vitu vinavyotokea kwa watu mbalimbali(patterns).
Kama wewe ni mfanyabiashara, tazama wale wenzako waliofanikiwa wanafanya nini?
Kama wewe ni mzazi, angalia mwanao anapenda nini? Hapendi nini?
Kama wewe ni wakili, angalia namna ambavyo mashahidi wanajitetea ili maswali yako yaweze kulenga unachokihitaji.
Kufanya jaribio (experiment) la kufungua macho na kuangalia vitu vinavyotokea kwa watu mbalimbali (patterns) vinaweza kukujengea kiwango cha hali ya juu cha akili hisia.
Zaidi ya hapo, sisi tunatakiwa kujiangalia kila siku. Na Mara ngapi unakagua ratiba yako ya siku?
Kuangalia kama siku yako ilijipanga kama ulivyotaka? Umeona kitu gani kipya katika siku yako?
Umejifunza nini katika siku yako?
Kuna lolote lililotokea linahitaji kuchunguzwa au kukomeshwa katika siku yako?
Zaidi ya maswali hayo, je, kuna fursa yoyote inayoweza kujitokeza katika siku yako?
Watu uliokutana nao wapya, wanaweza kukupa fursa gani?
Wachezaji kwa mfano wale wanaoshinda kwenye Olympics, wanajiangalia kwa kila wanachokifanya kila siku wanaoamka kitandani. Kwa maana nyingine ni lazima wataona kila kitu cha kufanya au kuacha kukifanya siku hiyo hiyo kinapotokea.
Haijalishi unafanya kazi au shughuli gani, ukiweza kutengeneza utaratibu kama huo, akili hisia zako zitakuletea miujiza yako.
Hitimisho
Muda wa kuongeza akili hisia zetu ni sasa.
Watu wengi sana wamejijengea tabia za kufunga pazia siku ikikamilika.
Haijalishi kama wako kazini au mashuleni.
Tunafunga mlango wa leo yetu ili tuanze siku mpya na mambo mapya. Hebu tujiulize swali moja, tungekuwa wapi kama kabla ya kufunga mlango wa leo yetu, tungefanya mapitio ya siku nzima? Tukachukua mafundisho stahiki kwa ajili ya kesho yetu? Wahenga wanasema yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
Unaweza kutengeneza akili hisia zako upya ili uone patterns za mafanikio yako kila leo. Unajua la kufanya:
#1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua..
#2. Hatua ya Kanuni za kibinafsi au kwa lugha nyingine ni self-Regulation.
#3. Hatua ya tatu ni kujipa au kutoa motisha.
#4. Hatua ya nne ni kujiongeza kwa kujifunza na kujenga uelewa wako.
#5. Hatua ya tano ni kupika au kutengeneza ujuzi wako kwenye jamii iliyokuzunguka.
Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia, maana najisikia vizuri sana ninapoweza kuwa msaada kwa mtu. Mimi ni mtumishi wenu. Na kwa vile umeamua mwenyewe kuwemo humu basi huna budi kuhakikisha tunajadili kwa pamoja na kufikia suluhisho muafaka kwa maisha yetu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...