Wazo La Leo
Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Majengo, biashara kubwa, viwanja vizuri vya mpira na mengine mengi ambayo wengine huita maajabu ya dunia ni matokeo ya mawazo.
Ninachotaka kusema ni kwamba kila mtu ana mafazo ambayo akiyafanyia kazi maisha hayatakuwa kama yalivyo sasa.
Mtihani mkubwa ni jinsi ya kuyapata mawazo yako ambayo yako ndani yako mithili ya madini.
Wote tunatambua madini si rahisi kuyapata ni mpaka nguvu ya ziada itumike maana hukaa chini sana na mengi ya madidini kama sio yote yako chini ya miamba.
Watu hulazimika kununua mitambo ili tu waweze kufikia madini. Kifupi si lelemama.
Vivyo hivyo kwa mwanadamu ili kukutana na mawazo kuntu yaliyomo ndani yake, ni lazima afanye kazi ya ziada.
Yawezekana umejaribu mawazo mengi kufanyia kazi lakini mambo bado hayajabadilika. Hii haimaanishi ya kuwa wewe huna mawazo yatakayoishangaza dunia. Endelea kupakua mawazo na kufanyia kazi. Acha kusua sua. Hakuna wazo baya bali wengi hawajui uthamani wa mawazo.
Baadhi ya watu hufanya biashara ya kuuza mawazo na watu wakiyatumia hufanikiwa ajabu. Kuna nchi zingine zimeajiri watu kazi yao ni kufikiri kwa ajili ya nchi na kuleta mawazo mapya serikali iweze fanyia kazi.
Sasa wengi ni wavivu wa kufikiri. Na nikuambie kwa uhakika kazi ya kufikiri ina siri kubwa.
Matatizo uliyonayo ni kielelezo tosha ya kwamba wewe ni mvivu wa kufikiri.
Kila tatizo unalolijua wewe lina lina suluhu yake nayo iko ndani yako. Shida hujishughulishi kufikiri. UTAPATA TABU SANA.
Utaratibu/njia zitakazo kusaidia kupakua mawazo ni hizi zifuatazo:-
1. Nunua kinoti buku chenye ukubwa wa kuingia kwenye mfuko wa shati na kwa akina dada/mama iwe na uwezo wa kukaa kwenye pochi. Yaani popote ulipo ni lazima uwe na noti buku na peni.
2. Moja ya njia rahisi sana ya kupakua mawazo inaitwa kwa lugha ya wenzetu ‘PRIME HOUR’ ambayo nikitafsiri Kiswahili ni ‘SAA MOJA MUHIMU’. Hii inamaanisha nini. Katika ratiba yako ya kutwa nzima ambayo wewe unaijua vizuri ina mchanganyiko wa shughuli. Sasa kanuni hii inasema katika hizo shughuli chagua baadhi ya shughuli utakazo zifanya kwa kutumia kanuni hii ya PRIME HOUR.
Mfano ratiba yangu ya leo iko hivi:
· Kumshukuru Mungu kuniamsha salama
· Kutahajudi
· Kusoma biblia
· Kunywa maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na limau
· Kuandaa Makala ya wazo la leo
· Kuoga na kuvaa
· Kupata kifungua kinywa
· Kuelekea Kanisani
· Kupata Lunch
· Kikao na mkurugenzi wa kampuni X
· Kusoma Kitabu
· Kumtembelea rafiki yangu
· Kupata matunda (Dinner)
· Kukaa nusu saa nikiwa peke yangu ili kutafakari siku ilivyo isha na kupanga mambo ya kesho (TO DO LIST).
· Kusikiliza video za mentor wangu Less Brown
· Kuoga na kulala
Sasa kwa lengo la kupakua mawazo nachagua KUANDAA MAKALA YA LEO, KUSIKILIZA IBADA, KIKAO NA MKURUGENZI NA KUSOMA KITABU.
Hapo nimechagua shughuli nne na kila moja nitaifanya kwa saa moja isipokuwa kanisani ni masaa matatu. Hivyo kwa leo nitakuwa na PRIME HOUR zangu 6.
Kivipi? Nitakapokua nikiandaa Makala yangu ya leo, nitazima simu, kama kuna paka nitamtoa nje, nitakaa mahali ambapo hakuna mtu wa kuniingilia. Hivyo mawazo yangu yote, yatabaki kwenye kuandaa Makala tu. Sitokuwa na kitu kingine cha kuingilia nifanyapo shughuli yangu.
Nimalizapo kuandaa Makala nitachukua noti buku na peni na mawazo yataanza kutoka name nitayaandika. Nitafanya vivyo hivyo kwa shughuli zangu zote za leo. Maana yake masaa 6 yangu ya leo ni PRIME HOUR. SIJUI WEWE LEO UNA PRIME HOURS NGAPI?
Naona niishie hapo kutiririka nitaendelea kesho na Makala hii. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.
Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
:www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni
Chapisha Maoni