Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NGUVU NA MUDA WAKO UNAUWEKEZA WAPI?

Wazo La Leo

Karibu tena msomaji wa Makala

Naamini umewahi kujiuliza na kama bado basi endelea kufuatana nami juu ya  mada yetu ya leo isemayo Nguvu na muda unauwekeza wapi?

Kimsingi kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingine kuna mahali anawekeza muda na nguvu zake.

Nini namaanisha nini nisemapo kuwekeza muda na nguvu?

Kimsingi chochote ufanyacho lazima utumie muda na nguvu pia. Hii ndio naita kuwekeza.

Hebu niachane na sehemu ambayo wewe huwekeza muda na nguvu zako, nami nijikite kwenye uwekezaji wenye tija.

Kujiendeleza

Kama kuna kitu ambacho mwanadamu amefumbwa basi ni eneo la kujiendeleza (Pesornal Development).

Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini umekuwa hupigi hatua? Au kwa nini umekuwa mtu wa uhitaji kila mara na kuzungukwa na madeni mpaka umegeuka kituko utazani unafanya maagizo barabarani maana  kwa jinsi ugeukavyo mara umuonapo mdeni wako Joti atasubiri sana.

Wewe tunayekuona siye wewe. Wewe mwenyewe yuko ndani yako. Maana yake mko wawili wewe wan je na wewe wa ndani. Inafahamika pasi shaka yakuwa wewe wa ndani ni jemedari aliyelala. Akiamka huna shida tena. Shida ulizonazo na kutofanikiwa kwako usimtafute mchawi, mchawi ni wewe mwenyewe unayeendelea kumfanya wewe wa ndani aendelee kulala kama si kukoroma.

Sasa nini suluhisho? Hakuna njia ya mkato, wewe wa ndani anaamshwa kwa kumlisha maarifa kupitia usomaji wa vitabu kwa asilimia kubwa angalau nusu saa kwa siku japo muda wa mtu aliyechoshwa na haya maisha hutenga waalau masaa matatu kwa siku kwa lengo la kujisomea na huku akiwa na kinoti buku cha kuandika pointi zimgusazo ili akiwa ametulua aweze kujikumbusha.

Pili ni kupata mawazo mbalimbali yenye tija kama ilivyo kararakana ya ubongo.

Tatu kuwasilikiliza watu waliofanikiwa ambao wewe binafsi unawakubali.

Tatu kuhudhulia semina ikibidi hata kulipia pesa lipa.

Nne kuwa na mtu wa kukuongoza (Kocha). Hii ni muhimu sana.

Na mengine mengi ambayo waweza endeleza lakini mimi nimekudadavulia hayo ya msingi.

Naomba nikukuhakikishie, iwapo utawekeza muda na nguzvu zako katika endeo hili nakupa mwaka mmoja maisha yako lazima yabadilike sana. Mimi ni shahidi.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza.

Seth Simon Mwakitalu

Entrepreneurship Consultant and Lifestyle Trainer.

Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836

Email: ssmwakitalu2013@gmail.com

Website: www.qls.com

Be Ready To Learn/Karakana Ya Ubongo.

We empower people:-

1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.

2. Acquire life changing business skills.

3. Prepare for retirement.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...