Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UPINZANI ULIOPO KATI YA UBONGO NA MOYO

Wazo La Leo

Habari ya   leo rafiki na msomaji wa mtiririko wa Makala za kila siku zijulikanazo kama wazo la leo.

Leo nataka niongelee kidogo juu ya upinzani uliopo kati ya ubongo  na moyo.

Ninapoanza kuelezea naomba nikuulize kitu kitogo: Je unajua kwa uhakika wewe una kitu kisicho cha kawaida ndani yako kiwezacho kubadili kabisa maisha yako na mengine yakawa stori?

Kama hujui naomba nikuambie ya kwamba maisha unayoishi sasa mfanano wake ni tone ndani ya bahari.  Huna haja ya kuwa tone kwani wewe ni bahari.

Sababu moja kubwa inayokufanya ushindwe kuishi kwa viwango vya juu ambapo ni haki yako ni ukinzani uliopo kati ya moyo na ubongo.

Unaweza kuona jambo linafanywa na mtu na ukajisemea  moyoni ya kuwa nami naweza kufanya lile afanyalo yule (MOYO). Ghafla unaanza kujiongelesha hivi nitawezaje (UBONGO)? Yaani unaanza angalia uwezakano wa wewe kufanya na ukiendelea kutafakari unajiambia siwezi. Sasa ubongo       umesema huwezi lakini na unakuuliza utawezaje. Sasa usipojua kinachoendelea ndani yako utabaki hapo hapo hata miaka ishirini ukitafakari ivi mimi kivipi naweza kuwa kama Bakhresa, Mengi, Mohamed   Dewji au  Aliko Dangote.

Ukweli ni kwamba chochote unachokiona mwanadamu mwingine anakifanya nawe unauwezo na kuzidi, tatizo hujui jinsi ya kushikamana, moyo unakwamishwa na ubongo ukijaribu kutafari ni kwa jinsi gani waweza na matokeo yake hata kuthubutu unashindwa.

Kimsingi ukitaka kuamsha uwezo  ullio nao kuna siri unatakiwa uijue nayo ni hii:-

·         Kaa chini ukiwa na notibuku yako. Kisha anza kuandika kila kitu unachohitaji ambacho moyo wako umekuwa ukitamania. Angalizo: Nimekuambia orodhesha sasa wewe unaanza kujiuliza hivi si nitaonekana kichaa mtu  akisoma ati nimeandika V8 kweli mimi naweza miliki V8 (UBONGO). Hapo utakwama na inawezekana hata zoezi la kuorodhesha mambo yote  utamanio ukaacha. Siri  ni moja itendayo kazi hutakiwi hata siku moja kujiuliza utafanyaje kupata ulivyoviorodhesha kwa sababu namna gani si kazi yako, bali kazi yako ni kuusikiliza moyo unataka nini.

Kama hujawahi fanya hili zoezi, naomba leo nikusihii nunua kakauntabuku kenye kava ngumu maana utakuwa na kicho kikaunta buku kwa maisha yako yote. Utakachoshangazwa ni tiki za kukamilishwa kwa yale uliyoorodhesha kila baada ya kipindi.

Sasa nakuambia iwapo pesa si tatizo je ungependa kuwa/kumiliki nini? Orodhesha idadi angalu 100 ya uyatakayo iwapo pesa ingalikuwa si tatizo. Hivi ndivyo watu wawezavyo kuorodhesha ndoto za maisha yao.

·         Orodha hiyo ipitie kila  siku asubuhi na jioni na unapoipitia tafadhali ipitie kwa hisia. Mfano ukifika  kwenye V8 unaweza ukapozi huku ukifikiria utakavyokuwa ukiiendesha alafu unaisikia mpaka harufu ya upya wa gari ukiwa umo ndani. Fanya hivyo asubuhi na jioni kila siku. Utashangaa kwa jinsi utakavyoanza kupata kimoja baada ya kingine. Kifupi ni kwamba kivipi utaweza hiyo inakuja yenyewe wewe  usitoe nafasi ya kuzuiliwa kuandika matamanio yako ati itawekana vipi. Nikuambiacho ni kwamba INAWEZEKANA KUWA ZAIDI YA DANGOTE NA WENGINE UNAOWAFAHAMU.Njia hii ni moja ya njia chache za kumstua jemedari wewe  UNAYEKOROMA. Kama utapata shida njoo inbox au panga tukutane tupanuane mawazo.

Nimalizie kwa kusema, namnukuu Less Brown (My mentor) – Kuzaliwa kwako kulisababisha vifo vya ndugu zako wapatao 399,999,999 . Kifipi? Mchakato wa wewe kuzaliwa ulikuwa hivi: baba yako aliachia mbengu zipatazo 400,000,000 na zikaanza mbio kukimbilia yai kwa mama yako na mbegu yako ilikuwa na kasi Bombadia itasubiri na kuwai  kushikamana na yai la mama yako kitendo hicho kikasababisha ndugu zako 399,999,999 wauwawe wewe jemedari uzaliwe.  Fikia kwa kina – Mungu hakuwa mjinga kukuruhusu wewe uje.  Aliona makubwa na ya kutisha utakayoyafanya duniani. Wewe ni faida si hasara naomba nikuhakikishie hilo.

Shida makelele yamekuwa mengi hadi unashindwa kujitambua. Naomba nikupe ushauri wa bure:-

·         TV ni mcheleweshaji wa kufika utakako punguza muda wa kuiangalia upate muda wa kufanya mengine ya maana na kama utaweza kama mimi achana nayo kabisa.

·         Tafuta marafiki wa maana

·         Amusha kiu ya kujifunza. Haigharimu chochote kwa mshumaa unaowaka kuuwasha uliozimia. Utaanza kuamka taaratibu kupitia mafunzo mbalimbali.

·         Kusoma vitabu  fananisha na kula chakula. Ukisema huna muda wa kusoma je muda wa kula unatoka wapi?

·         Ondoka kijiweni, maongezi ya ushabiki, siasa, mpira kuongelea watu HAVITAKUSAIDIA.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza.

Seth Simon Mwakitalu

Entrepreneurship Consultant and Lifestyle Trainer.

Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836

Email: ssmwakitalu2013@gmail.com

Website: www.qls.com

Be Ready To Learn/Karakana Ya Ubongo.

We empower people:-

1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.

2. Acquire life changing business skills.

3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...