Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ACHA VISINGIZIO

Wazo La Leo: Acha Visingizio

Habari za leo mpendwa msomaji wa wazo la leo.

Karibu tena kuweza  kufuatana nami katika mtiririko wa Makala mbalimbali nizitoazo kila siku ili kuweza kusaidiana katika safari yetu ya maisha.

Leo ningependa kuongelea kwa sehemu juu ya mada niliyoiita ‘ACHA VISINGIZIO’

Imekuwa jambo la kawaida kwa tulio wengi kuacha kuongea ukweli badala yake twakimbilia kutoa visingizio. Leo tutajadili baadhi ya maeneo ili tuone tunavyojidangaya.

Hebu fikiria mtu asemaye siku moja nitafanya hiki na kile. Sentensi hii japo haijasema ni kisingizio bali ni kisingizio tosha.

Siku moja hiyo iko wapi? Na kwani nini siku hiyo moja. Usidanganyike siku sahihi ni leo. Hebu boresha maisha yako kwa kuchukua hatua. Leo ni siku njema mno kufanya kitu. Acha uzembe na binafsi nachukuia watu wazembe. Inuka katende ulitakalo.

Ni vizuri tukajua jinsi ya kupambana na hofu katika maisha zitupelekazo kutoa visingizio. Ufumbuzi sahihi ni kuhakikisha una kitu cha kufanya mbele yako. Hakikisha si mtu wa kijiweni yaani asiyejua la kufanya zaidi ya kuongelea siasa, masihala na sasa kuna janga la watu kuzama ziwani basi utazani wewe ndiye mbunge maana unavyochambua uzembe uliosababisha na kuonesha masikitiko utadhani u mtu wa maana, lakini ukweli unatwanga maji kwenye kinu. Sijui ukimaliza kutwanga utapata nini. Tafadhali jishughulishe.

Pia nitaongelea suala la nani hupenda kuwa naye mara nyingi. Yaani ni akina nani twaweza sema ndio marafiki zako wakubwa. Hapa pana ukweli kwamba ukichukuwa watu watano walio karibu sana nawe na ukajumlisha vipato vyao kwa mwezi na ukagawa kwa 5 jibu utakalopata ndio kipato chako kwa mwezi na huwezi zidi hapo. Sasa unakazana kusema mambo hayakunyookei sijui nini tatizo maana kuhangaika unahangaika lakini maisha hayaendi.

Sikiliza, chagua kipato utakacho na kisha orodhesha wenye kipato hicho utamanicho, kisha tafta namna utakavyooanza kuhusiana nao. Mahusiano ni kila kitu maishani. Chagua marafiki kwa uangalifu wengine ni shida.

Nikiwa naelekea kumalizia Makala yangu naomba kukushauri - PUNGUZA KAMA HUWEZI KUACHA KUTAZAMA TV ili upate muda wa kusoma vitabu. Hii tabia ya kusema unashindwa kusoma vitabu ati huna muda ni kitendo cha kushangaza. Nani alikuambia kuna mtu anagawa muda. Muda upo kwa kila mtu masaa 24. Mipangilio yako ya kutumia muda ndio ya kuangalia. Unaposema huna muda tafsiri yake hujaona umuhimu wa kufanya kitu tofauti badala yake unasema huna muda. Kauli hiyo si sahihi. Mbona unapenda kuangalia movies na hazikupiti ila kusoma vitabu huna muda. Amka chukua hatua.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza.

Seth Simon Mwakitalu

Entrepreneurship Consultant and Lifestyle Trainer.

Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836

Email: ssmwakitalu2013@gmail.com

Website: www.qls.com

Be Ready To Learn/Karakana Ya Ubongo.

We empower people:-

1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.

2. Acquire life changing business skills.

3. Prepare for retirement.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...