Wazo La Leo
Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Ninapoanza kuongelea neno falsafa naona vyema nikatoa tafsiri ya hili neno kama ambavyo nimesoma kwenye kamusi.
Neno falsafa limetokana na neno la kigiriki na tafsiri sahihi na ambayo ndiyo tutaitumia katika mada yetu ya leo ni kanuni inayolinda tabia au mwenendo. Yaani mwenendo wako au tabia zako ni kutokana na kanuni ongozi na hivyo maisha yako yana kuwa katika namna fulani ya kuishi maana unaongozwa na falsafa ulizozikubali na kuzitumia katika maisha.
Wiki zima hii nimekuwa nikisiliza video ya Jim Rohn na kwa hakika nimejifunza falsafa mbali mbali kutoka kwake ambazo ndizo zilibadilisha kabisa maisha yake.
Hii inamaanisha ya kuwa hata wewe na mimi tukitumia falsafa hizi zitatusaidia kuboresha maisha yetu.
1. Falsafa ya 1: FAIDA AIPATAYO MTU KATIKA KUFANYA BIASHARA NI BORA MARA DUFU KULIKO MSHAHARA.
Falsafa hii inasisitiza umuhimu wa kuwa na biashara hata kama una ajira kutokana na ukweli kwamba faida ni bora kuliko mshahara.
Sababu ya kwanza mshahara huwa haubadiliki hata ujitume vipi. Labda kwa mbali mara moja kwa mwaka tena asilimia ndogo hata 5% haifiki, lakini kwa upande wa biashara ukiwa mbunifu mauzo huongezeka na vivyo hivyo faida huongezeka.
Utafiti umedhihirisha ya kuwa faida apatayo mtu kutokana na biashara ndiyo imfanyayo mtu kuwa tajiri na siyo mshahara.
Ushauri anaoutoa Jim Rohn ni kuhakikisha unakuwa na biashara hata kama umeajiriwa. Ukitoka kazini unafungua biashara yako na jiwekee lengo la kwanza la kuwa na faida sawia na mshahara.
Inaelezwa ukiwa unapenda kujifunza namna bora ya kufanya biashara itakuchukua miezi sita kuanza kupata faida sawa na mshahara.
Ukizidi kujifunza zaidi kufanya biashara haitakuchukua muda utapata faida sawa na mishahara miwili. Yaani biashara uifanyayo kwa muda wa ziada inauwezo wa kukupa mara mbili ya mshahara.
Naamini hakuna mtu asiye penda fedha za ziada, hivyo tukiweza kuishi falsafa hii isemayo Faida ni bora kuliko mshahara na hivyo kuhakikisha una kuwa na biashara hata kama una ajira.
2. Falsafa ya 2: MAISHA YAKO YAJAYO HAYATEGEMEI MATUKIO YANAYOJITOKEZA SASA BALI MUITIKIO WAKO KUTOKANA NA MATUKIO NDIO KINACHOANGALIWA ZAIDI.
Mabadiliko ya uchumi kila mmoja yanampata. Kinachomtofautisha mtu mmoja na mwingine ni namna utakavyoitikia mabadiliko ya uchumi.
Hii inatoa tafsiri kwa nini sasa hivi watu wamebaki wakilalama ati vyuma vimebana ati hali waliyoizoea haipo tena na hivyo kusababisha maisha kuwa magumu.
Chakushangaza katika hali hiyo hiyo wengine kama akina Seth tunaona vyuma vimelegea.
Mwitikio wako juu ya maadiliko ndicho hukutofautisha na wengine.
Hii ni sawa na kusema mawimbi au upepo kamwe hautakuamulia mwisho wa safari yako bali namna utakavyoilengesha mashua yako kutokana na upepo au mawimbi ndicho kitamua kituo chako cha safari.
Wanakarakana tujiangalie kauli zetu za kurudia rudia ati vyuma vimebana, hii itasababisha mtumwa (akili isiyo tambuzi) apokee amri na kuhakikisha kweli vyuma vinabana. Hebu tuwe chanya siku zote.
Hivyo mabadiliko yakitokea jukumu lako ni kufikiria namna utakayofanya ili mabadiliko yasikuathiri na si kulalamikia mabadiliko.
3. Falsafa ya 3: FURSA HUCHANGAMANA NA CHANGAMOTO.
Ni ukweli usiofichika kwamba fursa huchangamana na changamoto. Kuna wakati kuna kuwa na fursa nyingi kuliko changamoto bali pia wakati mwingine unakuwa na changamoto nyingi kuliko fursa.
Cha msingi unachopaswa kujua ni kuwa kuchangamana kwa fursa na changamoto ni asili ila wakati gani kipi kinakuwa zaidi ya mwenzake hutegemeana na majira.
Ukilijua hili halitakusumbua maana ukiona changamoto zimezidi fursa jua ni suala la wakati tu kwani kipindi kinakuja changamoto zitakuwa chache kuliko fursa na kichume chake. Hiyo kamwe haitakuja kubadilika.
Hivyo ikitokea mojawapo kuwa zaidi ya mwingine hutasumbuka maana tayari utakuwa ukiishi falsafa hii ya kuwa kuchangamana ni lazima.
4. Falsafa ya 4: Kushuka au kupanda ndio hali halisi.
Maisha tuishio usitemee kuwa na mambo yako yakiwa yamenyooka tu pasipo mabonde na milima.
Kawaida kushuka na kupanda ni sehemu ya mwanadamu awaye yeyote na huwezi kubadilisha mojawapo kutokea.
Unaposhuka iwe ni kiuchumi au jambo lolote lile basi huwa ni fursa ya kujifunza na kukomaa.
Kipindi kizuri cha mtu kukomaa ni wakati wa mambo yanaposhuka, au mauzo kushuka. Tambua ya kwamba yote hayo ni ya muda.
5. Falsafa ya 5: ILI UWEZE KUPATA MABADILIKO NI LAZIMA KWANZA WEWE UBADILIKE NA SI KINYUME CHAKE.
Kiini cha mabadiliko yawayo yoyote ni wewe. Acha kulalamikia nahodha wa maisha yako ni wewe mwenyewe.
Ukitaka maisha yako yabadilike huna budi kwanza ubadilike. Ukiendelea kufanya vilevile ulivyokuwa ukifanya siku za nyuma na kwa staili ile ile basi wewe ni kichaa maana haiwezekani upate matokeo tofauti kwa kufanya vilevile.
Hapa ndipo tunapima uwezo wa mtu kujijua. Mabadiliko yoyote huanza na wewe.
6. FALSAFA YA 6: KAMWE USIOMBEE MAMBO YAWE RAHISI BALI OMBA UWE BORA
7. FALSAFA YA 7: USITAMANI KUWE NA MATATIZO MACHACHE BALI TAMANI UWE NA UJUZI WA KUTOSHA.
8. FALSAFA YA 8: USIOMBE CHANGAMOTO ZIWE CHACHE BALI OMBA UWE NA HEKIMA
Sasa acha na mimi nije na falsafa yangu, SIJUI UTAIITA YA NGAPI: KWANZA SOMA KURASA KUMI ZA KITABU NDIO ULE. HIVYO KAMA UNAKULA MARA TATU BASI TUNATEGEMEA UTASOMA KURASA 30. HAKUNA KULA KAMA HUJASOMA KURASA KUMI. JIWEKEE FALSAFA HII NA UONE KAMA UTAKOSA MUDA WA KUJISOMEA.
Kwa kumalizia naomba ieleweke ya kuwa mwanadamu anauwezo wa kufanya mambo makubwa na yenye kuonekana bila kujali yuko katika hali gani na mazingira gani maadamu tu akinua kubadilika. INAWEZEKANA.
Naona niishie hapo kutiririka nitaendelea kesho na Makala hii. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.
Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
:www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni
Chapisha Maoni