Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUTAHAJUDI/MEDITATION

Wazo La Leo

Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Leo tunakwenda kujifunza juu ya Tahajudi/Meditation. Tafadhali fuatana name.

Meditation au taamuli ni kitendo ambacho wengi ambao wamejifunza mambo mengi ya hekima, nguvu ya akili katika maisha ya mwanadamu, sayansi, na Imani mbalimbali, wamekuwa wakivutiwa na kufanya meditation. Mojawapo ya changamoto ya kwanza ambayo wengi wamekuwa wakikutana nayo ni akili kuhama sana kwenye meditation. Kupitia Makala hii, nitajaribu kuelezea njia mbalimbali ambazo unaweza kuzifanya katika kuhakikisha akili inatulia sehemu moja na kuongeza nguvu ya umakini na utambuzi wa hali ya akili yako.



Mwanzo

Meditation au kwa jina la kiswahi Taamuli ni kitendo cha kutazama hali (nature) ya akili na kuongeza utambuzi na umakini. Wengi wanaofanya meditation ni kwa lengo la kuituliza akili kutoka katika stress, msongo wa mawazo, kuongeza hekima, kuongeza umakini na utambuzi juu ya mtu binafsi na jinsi alivyo. Pia wengine hufanya meditation kuachana na addictions na mazoea na kuongeza willi-power. Na wapo wanaofanya meditation kuongeza uwezo wa sheria ya usumaku (law of attraction) na wengine hufanya meditation kuongeza umakini, ubunifu (mfano wachoraji, wanamuziki, wasomi n.k). Kuna sababu nyingi ambazo kila mtu binafsi anaamua kufanya meditation.



Akili ni kitu ambacho ni kitu Tata sana (very complex). Ni sehemu ya mwanadamu ambayo haijagunduliwa vyema jinsi ifanyavyo kazi na hakuna mtu anayeweza kukusaidia kufikiri au kujua jinsi akili yako ifanyavyo kazi. Mara nyingi tumekuwa watumwa wa akili zetu bila kutambua kuwa tunaweza kutawala akili zetu na kuamuru akili iwaze nini, isiwaze chochote au kuamua kuweka umakini katika jambo Fulani kwa jinsi utakavyo wewe. Akili ukiweza kuiongoza utakusaidia lakini ukishindwa utakuwa mtumwa wake utakuwa mtumwa daima. Ndipo utakuta hali kama addictions, mazoea mabaya, umakini, hekima na uvumilivu tunashindwa kuwa navyo kwa sababu hatuwezi kutumia akili zetu ipasavyo.



Tatizo linalosababisha akili kutotulia

Kwa kawaida tangu unapoamka na mpaka unapoenda kulala akili inafanya kazi. Kila wakati utawaza hichi, kisha utawaza kingine, na ukitaka kujua hilo chukua kalamu na karatasi na saa. Andika kwenye karatasi kila kitu au wazo au hisia itakayopita akilini. Mfano ukiwaza kuhusu kazini andika kwenye karatasi “kazini”, ukimuwaza mtu andika jina lake, andika kwa ufupi ili upate muda wa kuandika. Hakikisha umeandika kila kitu na kisha baada ya dakika kumi utaona ni mawazo au hisia nyingi zimepita akilini. Huo ni mfano tu kuwa kwa kawaida akili huwa haitulii. Itawaza hichi, itakumbuka ya jana, utakuwa na hisia Fulani, na kila hali inakuja na kupita. Ndivyo tulivyozoea maishani.



Meditation na Akili.

Kwenye meditation unajifunza kuitawala na kuingoza akili kwa dakika Fulani. Mfano meditation ya Samadhi Meditation ambayo unaiweka akili katika umakini mmoja tu; ni kitendo cha kuelekeza akili katika jambo moja au kitu kimoja mfano kwenye pumzi tu. Kila saa na kila dakika tunapumua, lakini hatuweki akili zetu kwenye pumzi kwa sababu haina umuhimu kutazama pumzi kila saa. Hivyo meditation ya kuongoza akili inatumia pumzi kwa sababu ni hali ambayo wakati wote tunayo, haiitaji kuwasha mshumaa au kutazama kitu Fulani. Kuweka akili kwenye pumzi ni cheap/rahisi na haiitaji chochote. Ni mtu tu mwenyewe kutumia pumzi na kujaribu kuiweka akili sehemu moja kwa dakika chache. Unaweza kufanya meditation kwa kuweka akili yako kwenye mshumaa, kutazama bahari, kutazama chochote unachokiamini n.k. Kwa hapa leo nitazungumzia kuitawala akili kwenye pumzi.



Ukiwa unafanya meditation

Ukiwa unafanya meditation unakaa mkao ambao utakuwa huru na utaweza kukaa kwa dakika chache bila kuhama. Unaweza kukaa kwenye kiti lakini usilale kwa sababu unaweza ukasinzia kutokana na uvivu. Pia kama unaweza kukunja miguu kwa muda mrefu pia unaweza kukaa vizuri chini, juu ya mto au kitu ambacho kitaepusha maumivu ukikaa sakafuni.



Ukianza hakikisha hutasumbuliwa na utapata muda wa dakika chache kukaa peke yako. Pia unaweza kufanya meditation na wengine kwa kukaa pamoja na kila mmoja kuangalia upande wake (ili kuwa na concentration/umakini). Kwa wanaoanza tumia dakika 10. Kila wiki unaweza kuongeza dakika 5 mfano 15, halafu wiki ijayo ukajifunza 20 na kisha zoea kutawala akili kwa dakika 20 kila siku ndani ya mwezi mmoja na baadae unaweza kutumia 30 mpaka 40, sio lazima uzidi 40, cha msingi sio dakika ni umakini ndio uongeze. chukua saa au simu ikukumbushe dakika kumi zikifika. Hakikisha umeweka simu silent, na ukiwa kwenye meditation usiangalie zimebaki dakika ngapi, dedicate kuwa na subira mpaka muda utimie.



Ukianza weka akili kwenye pumzi, vuta pumzi taratibu na weka break kisha toa pumzi taratibu. Yaani unavuta pumzi, unakaa kidooogo kisha unaitoa taaratibu huku ukitazama jinsi hewa inavyoingia puani na kifua kikitanuka na hewa ikitoka na kifua kikishuka taaratibu. Ukigundua akili haipo tena kwenye pumzi usijali wala usijilaumu au kuona umekosea, ni kitendo cha kawaida akili kuhama bila kujijua. Cha msingi irudishe tena akili kwenye pumzi kama mwazoni. Endelea hivyo hivyo. Akili ikihama unairudisha kwenye pumzi. Ukiona kama unarelax na unahisi mwili umetulia sana huwa kuna kama raha Fulani unaihisi au umeme/waves Fulani ya relaxation unaiona unakuzunguka achana nayo na usiweke akili kwenye raha inayokujia ukiwa unafanya meditation wewe endelea kuweka akili kwenye pumzi na ile raha itaendelea kuwepo. Ukiiwaza utapotea, ni kama mtego.



Akili ikiwa haitulii.

Samahani kwa kuanza kuelezea mengi kwa sababu hapa ndipo kwenye mada kuu. Nilipenda kutoa introduction kwa ambao hawajui ili wafahamu na tuende sawa.



Akili huwa kwa mara ya kwanza kufanya meditation inahama sana. Sio tatizo ni hali ya kawaida. Ni uthibitisho kuwa akili inahitaji kutulizwa. Kuna njia mbalimbali ambazo unaweza kufanya. Unaweza kuhesabu pumzi inapoingia. Ukahesabu Moja….mbili…tatu na kufika kumi kisha rudi tisa, nane, saba, sita….. mpaka sifuri kisha anza tena moja, mbili…na kuendelea.



Njia nyingine, ukiona akili inahama, mfano unawaza kuhusu jambo Fulani, sema kwa taratibu “akili najua unawaza kuhusu masuala ya kazini, rudi kwenye pumzi”. Kusema hivyo sio kwamba unaongea na akili bali inakupa mazoea ya kujua kinachoendelea akili na kukifanyia maamuzi. Ukiona unawaza kuhusu kitu Fulani mfano pesa zako ulipoziweka sema “akili najua unawaza pesa zangu, rudi kwenye pumzi” kisha endelea kuweka umakini kwenye pumzi.



Baada ya kufanya meditation mara kwa mara utaona kuhama kwa akili kumepungua na unaanza kuona raha kufanya meditation. Pia baada ya meditation utakuwa unahisi Amani na kama ulikuwa umeshusha mzigo mzito akilini. Pia katika maisha utakuwa makini na kinachoendelea akilini mwako na kukusaidia kujitambua vyema.

Naona niishie hapa na nikaribishe maswali na michango mbalimbali. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza



Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
                 :www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

  1. Ninaswali kidogo kwako mtoa makala hii,
    Kadri unavyozidi kufanya tahajudi huweza kumfanya MTU kuwa na utambuzi?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...