Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAISHA NI VITA

Wazo La Leo

Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Maisha ni vita na hivyo bila ya kuwa na kiongozi aliye jemedari na mbinu wengine huita mikakati basi tegemea kushindwa vita yako.

Jemedari wa vita yako kwa bahati nzuri ni wewe mwenyewe. Hivyo yakupasa kujiimarisha. Hebu pata siku ongea na wanajeshi juu ya mazoezi afanyayo askari kabla ya kutambuliwa kuwa afisa (Commissioned)

Kimsingi hakuna mtu aitwaye afisa jeshini aliye goigoi na hasa linapokuja suala la vita.

Leo nimestuliwa na mhamasishaji na mwalimu wa kimataifa ambaye niandikapo yeye ni marehemu lakini kazi zake zinaishi.

Asubuhi nimekuwa nikisikiliza moja ya video zake na ndipo nikakutana na maneno ambayo yamenigeuza sana katika msimamo wa mapambano na maisha yangu.

Jim Rohn anasema tena pasi kupapasa macho ‘USINUNUE GARI KABLA YA KUNUNUA NYUMBA YAKO YA PILI AU KABLA HUJAJENGA NYUMBA YAKO YA PILI’.

Si gari litakalokuletea utajiri bali nyumba. Na anaendelea kusema ukitaka maisha ya kusukuma siku basi nunua na kuuza nyumba lakini kama unataka kuelekea kwenye utajiri kazi ni moja tu nunua nyumba, nunua nyumba au jenga nyumba, jenga nyumba.

Huyu ni mtu mwenye kuheshimika sana duniani na hivyo asemapo kitu maana yake amekiona. Ushauri wake katika mapambano ya maisha umeniongezea kitu.

Hii habari ya kununua gari na kujenga kanyumba kamoja na akiba TZS 10,000,000 benki kumewachelewesha wengi wakizani wamekwisha kuwa maafisa hubaki wakijiita matawi ya juu. Kumbe sifa ya kwanza ya kumiliki gari ni baada ya kununua au kujenga nyumba ya pili. Hili limetulia kwangu sijui kwako.

Nimeendelea kupata mbinu za vitani – Usisahau familia. Panga muda wa kuwa na familia ikiwa ni pamoja na kucheza na watoto, kufanya nao home work. Itapendeza ukiingia nyumbani unaachana na simu, laptop, magazeti na kupata muda wa kutosha na familia zaidi.

Angalia usije ukajiingiza kwenye matatizo ya kiafya kwa kujitumikisha kupitiliza mpaka unaisahau familia kwa kujituma kwako kupitiliza na masaa mengi kiasi muda pekee ulio nao nje na kazi ni kulala. Hiyo ni hatari haitakufanya kuwa jemedari wa maisha yako. Wape familia muda nao wafurahi kuwa na mzazi mwema katika familia. Ishi maisha yenye mizania (Balanced Life)

Si kujituma kwako na kufanya kazi kwa masaa mengi kutakako kusaidia kufanisha kuwa afisa au jemedari bali ni pale utakapo fanya shughuli zako kwa kuwa smarter na juhudi kidogo. Tumia kanuni ya 20/80 yaani asilimia 20 ya shughuli zako au muda wako ukuzalishie asimilia 80 ya matokeo na sio ufanye kazi kwa asilimia 80 na upate matokeo ya asilimia 20. Hebu jitafakari. Suala si maguvu na muda mwingi wa kufanya kazi bali ni maarifa na juhudi kidogo.

Nitafurahi kufanya kazi na mtu mvivu lakini anatumia sana akili kufanya mambo yake kivivu kuliko anayejituma pasi kufikiri namna rahisi ya kufanikisha mambo. Jifunze vizuri mbinu za kuwa kiongozi bora wa maisha yako.

Njia bora na sahihi ya ewe kuwa kiongozi shupavu ni kukusanya mauzoefu ya watu mbalimbali kupitia kujisomea vitabu. Hakuna njia ya mkato. Hii tabia ya kusema huna muda ila muda wa kuangalia mpira, TV kwenda beach nk unapata ni ushahidi tosha ya kuwa hujajitambua na Mungu akusaidie maana si kwa mwendo huo.

Binafsi nimejiwekea utaratibu. Nitakuwa sina sifa ya kula chakula kama sijasoma. Hivyo asubuhi kabla ya kifungua kinywa nasoma angalau kurasa kumi na ndipo najipongeza kwa break fast. Na chakula cha mchana vivyo hivyo nikisha soma angalau kurasa kumi ndipo Napata sifa ya kula na usiku mwendo ni ule  ule. Hakika nayaona mabadiliko yangu mwenyewe.

Hebu tufike mahali tuwe tunafanya kazi kwa kujifurahisha na sio kutafuta ridhiki. Utafutaji wa ridhiki uwe ni wa muda tu. Tufike mahali tuwe tunawawazia wengine jinsi ya kuwasaidia.

Mwisho nakuomba fuata utaratibu ufuatao ukipenda:-

1.       Hakikisha unajitosheleza katika familia yako.  Na mbinu pekee ni kuweka mkakati wa kuzalisha zaidi ya mahitaji yako. Yaani kila wakati uwe na ziada.

 .

2.       Hakikisha unatengeneza mazingira mazuri kwa wazazi wako kiasi cha kupata mahitaji yao bila manung’uniko. Hata kama kwenye familia mko 10 chukulia uko peke yako ili usipate ugonjwa wa kutegea wenzio na usikubali mambo ya zamu wewe jiwekee utaratibu wa kuwatosheleza wazazi wako. Kuna siri kubwa sana wazazi wanenapo kila wakati Baraka kwako. Kumbuka biblia inasema waheshimu sana baba na mama yako ili uwe na siku nyingi za kuishi duniani.

Kuwaheshimu haimaanishi kuwapigia magoti bali kuhakikisha wako salama na mahitaji, mavazi na makazi si tatizo kabisa.  Acha unafiki wa kusaidia watu wengine wakati wazazi wako wako kwenye hali mbaya. Mzazi akikuomba ni tafsiri tosha ya kuwa wewe ni hasara na wala si faida. Jizuie hatua hiyo isikupate au isikufike kujisahau.

Ndugu zako ni nguvu kazi, weka mkakati wa kuwasaidia na wao wazalishe na kamwe usisema watajiju. Utakuwa unakosea.

Familia yako ukiweza kuisaidia na kila mmoja akabaki akikushukuru ni thawabu kubwa sana na hapo utakuwa na kibali cha kuanza kusaidia nje ya familia yako.

Maandiko yaani biblia inasema asiye jali wa kwake yaani wa ndani mwake (Familia), mtu huyo ni mbaya kuliko asiye amini na adhabu yake ni kufungiwa jiwe shingoni na kutupwa baharini.

Kusudi au lengo la mwisho la mwanadamu kabla ya kuingia kaburini ni kugusa maisha ya watu. Isitokee umefariki watu wakawa wanalia sana na wengine hadi kuzimia si kwa mema uliyoyatenda bali umekufa na madeni ya watu. Hapana hakikisha unaweka sawa mambo.

Pata muda wa kutafakari juu ya maisha yako na  jinsi ya kuyaboresha.

Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza.

 

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
                 :www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...