Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAISHA YAKO NI MATOKEO YA UCHAGUZI WAKO

Wazo La Leo

Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Maisha tuishio ni matokeo ya maamuzi ya kila siku ndiyo yametufikisha hapa tulipo.

Je umekuwa unapendelea nini zaidi kati ya kujishughulisha na jambo la kufurahisha na lililo rahisi au jambo la kukufikirisha na gumu.

Nimesikia mara nyingi watu wakiambiana njoo ufanye huku nkwani ni rahisi kuliko huko.

Naomba utambue vizuri kanuni ya dunia ifanyavyo kazi.

Rahisi huwa havidumu na vigumu ndivyo hudumu. Jambo lolote linalokufanya ufikiri linakukuza na kinyume chake linakudumaza.

Wakati tukiendelea na mada yetu ya uchaguzi, najaribiwa kukuambia jambo hili:-

Kujua jambo litakalo kuletea matokeo mazuri ni jambo moja na kulitenda ni jambo linguine.

Ndio maana kuna tuna makundi ya waliofanikiwa na wasiofanikiwa.

Kujua kufanikiwa ni kufanya yale wayafanyayo na waliofanikiwa. Na yampasayo mtu kufanya ili afanikiwe ni rahisi, lakini pia kitu rahisi kufanya ni rahisi pia kutofanya.

Kuachana na mazoea imekuwa mtihani kwa walio wengi. Namanisha kutengeneza tabia mpya si jambo dogo ndio maana wengine uanza na kuishia njiani.

Wengi wamechagua kufanikiwa ila imekuwa shida kufikia mafanikio.

Adui mkubwa wa chaguzi zetu ni pale tunaporuhusu hisia zitutawale.

Unakuta mtu anasema leo sijisikii najisikia kuchoka nitafanya kesho. Kwa namna hiyo utasubiri sana.

Unatakiwa uongozwe na faida uipatayo kwa kufanya iwe unajisikia vizuri au vibaya wewe fanya mpaka iwe tabia yako pasipo kutaabika kuifanya.

Kimsingi inamchukua mtu siku 21 kuitambulisha tabia mpya na kuwa sehemu yako na kumfanya mtumwa (subconscious) ashughulike.

Kuchagua kufanya jambo jipya kunahitaji nidhamu.

Hebu nikushirikishe machache upasayo kufanya. Uchaguzi unabaki kuwa ni wako – Kufanya au kutofanya.

1.       Ishi ukijua kwa hakika unaelekea wapi? Ninamaanisha jua kwa hakika malengo yako au kule utakako kufika. Na kimsingi akili hufanya kazi vizuri iwapo malengo yako utayaandika tena kwa ufasaha kiasi cha kila mtu asomapo hukuelewa pasipo maswali na siyo yabaki kichwani. Malengo yasiyoandikwa ni ndoto. Ni mpaka pale utakapo amua kuyaandika ndipo huitwa malengo. Kumbuka kama hujui uendako basi njia yoyote inakufaa.
2.       Tengeneza ubao wa malengo sehemu ambayo ni rahisi kuyasoma asubuhi unapoamka na jioni ulalapo. Hii itasaidia sana mtumwa (subconscious mind) kuyapokea na kusababisha utendaji hatimaye kukamilika kwa  malengo moja baada ya linguine.
3.       Jenga tabia ya kupata matokeo na sio kufanya tu kazi pasipo kujua mwisho wa siku ukimali za kazi uifanyao matokeo itakuwa nini. Wengi wamefanya mambo mengi nusunusu na hakuna kilichokamilika na uhishia kuchoka na kulala na mke wake mzungu wanne na hakuna tokeo hata moja lilokamilika. Sababu kubwa ni kugusakugusa na kuacha.
4.       Acha kuwa mtu wa kuzunguka zunguka ili uwafurahishe watu. Tabia ya jinsi hii si nzuri. Ongea kwa uwazi ukijielekeza kwenye pointi iwe muhusika atafurahi au kukasirika. Acha kufunika funika. Mwambie mtu hili ni koleo na sio kijiko kikubwa. Itakusaidia na kukurahisishia.
5.       Hakikisha unajinoa vya kutosha juu ya ufanyacho ili uwe mahiri katika shuguli zako. Ikibidi kutoa pesa ili kunolewa fanya hivyo. Kuwa mahili ni safari na si kituo maana mambo huenda yakibadilika.

Naona niishie hapa. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
                 :www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...