Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NJIA ZA KUKUWEZESHA KUPAKUA MAWAZO

Wazo La Leo

Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Jana niliiishia kwa kusema:-

Utaratibu/njia zitakazo kusaidia kupakua mawazo ni hizi zifuatazo:-

1.            Nunua kinoti buku chenye ukubwa wa kuingia kwenye mfuko wa shati na kwa akina dada/mama iwe na uwezo wa kukaa kwenye pochi. Yaani popote ulipo ni lazima uwe na noti buku na peni.



2.            Moja ya njia rahisi sana ya kupakua mawazo inaitwa kwa lugha ya wenzetu ‘PRIME HOUR’ ambayo nikitafsiri Kiswahili ni ‘SAA MOJA MUHIMU’. Hii inamaanisha nini. Katika ratiba yako ya kutwa nzima ambayo wewe unaijua vizuri ina mchanganyiko wa shughuli. Sasa kanuni hii inasema katika hizo shughuli chagua baadhi ya shughuli utakazo zifanya kwa kutumia kanuni hii ya PRIME HOUR.

Mfano ratiba yangu ya leo iko hivi:

•             Kumshukuru Mungu kuniamsha salama

•             Kutahajudi

•             Kusoma biblia

•             Kunywa maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na limau

•             Kuandaa Makala ya wazo la leo

•             Kuoga na kuvaa

•             Kupata kifungua kinywa

•             Kuelekea Kanisani

•             Kupata Lunch

•             Kikao na mkurugenzi wa kampuni X

•             Kusoma Kitabu

•             Kumtembelea rafiki yangu

•             Kupata matunda (Dinner)

•             Kukaa nusu saa nikiwa peke yangu ili kutafakari siku ilivyo isha na kupanga mambo ya kesho (TO DO LIST).

•             Kusikiliza video za mentor wangu Less Brown

•             Kuoga na kulala



Sasa kwa lengo la kupakua mawazo nachagua KUANDAA MAKALA YA LEO, KUSIKILIZA IBADA, KIKAO NA MKURUGENZI NA KUSOMA KITABU.

Hapo nimechagua shughuli nne na kila  moja nitaifanya kwa saa moja isipokuwa kanisani ni masaa matatu. Hivyo kwa leo nitakuwa na PRIME HOUR zangu 6.

Kivipi? Nitakapokua nikiandaa Makala yangu ya leo, nitazima simu, kama kuna paka nitamtoa nje, nitakaa mahali ambapo hakuna mtu wa kuniingilia. Hivyo mawazo yangu yote, yatabaki kwenye kuandaa Makala tu. Sitokuwa na kitu kingine cha kuingilia nifanyapo shughuli yangu.

Nimalizapo kuandaa Makala nitachukua noti buku na peni na mawazo yataanza kutoka name nitayaandika. Nitafanya vivyo hivyo kwa shughuli zangu zote za leo. Maana yake masaa 6 yangu ya leo ni PRIME HOUR. SIJUI WEWE LEO UNA PRIME HOURS NGAPI?

Sasa leo hebu tuendelee na njia zingine za kupakua mawazo:-

1.       Mapumziko:- Ukiwa umepumzika na kutojishughulisha na chochote, mfano umelala iwe ni usiku au mchana. Yawezekana kabisa katikati ya mapumziko/usingizi ukakurupuka na ukawa na mawazo kibao. Unashauriwa hata ukilala hii noti buku (Brain Damping Note Book) ya kupakuwa mawazo iwe pembeni ya kitanda chako ili ukiamka tu uweze kuchukua na kuandika.

2.       KUTAHAJUDI (MEDITATION) – Moja kati ya njia muhimu sana na ambayo kila mwana karakana ya ubongo hana budi kuijua ni KUTAHAJUDI (MEDITATION).
Hii njia ni ya muhimu sana kwa kuwa inafaida lukuki. Panapo majaliwa kesho tutashirikishana somo hili la kutahajudi na namna ya kutahajudi. Mara nyingi ukimaliza kutahajudi mawazo hutirirka nawe kuweza kuyapakua.

Naona niishie hapo kutiririka. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
                 :www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...