Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ONGEZA UFANISI

Wazo La Leo:

Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Moja ya jambo linalofanya wengi wachelewe kufikia mafanikio ni suala zima la ufanisi.

Leo nitagusia maeneo machache yatakayokusaidia kuongeza ufanisi wa kila utendacho.

1.       Jua kupangilia vipaumbele vyako. Waweza kuwa na mambo kumi ya kufanya leo. Unachotakiwa kufanya ni kuanza na kile kilicho muhimu yaani ukifanyapo kinakusogeza kwa sehemu kuelekea lengo lako, kisha kinachofuata kwa umuhimu hadi unafikia cha mwisho. Hivyo utafuata mpangilio uliojiwekea hadi siku yako inakwisha. Ukijizoeza kufanya hivi kila siku, utaona mabadiliko katika maisha yako ya utendaji.

2.       Jiambie mara kwa mara ya kwamba kwako msamiati wa kushindwa haupo. Ni kupambana mpaka kieleweke. Maisha si rahisi kivile. Dunia huzawadia majemedari na si walegevu/wachovu/wakata tamaa. Ni majemedari tu ndio hufanikisha maisha. Acha kabisa kuongelea kushindwa au kusema vyuma vimekaza. Hakuna kipindi kizuri kupata pesa kama tulicho nacho iwapo utaishughulisha akili. INAWEZEKANA SONGA MBELE.

3.       Jipe nidhamu wewe mwenyewe. Maisha ya mtu asiye na nidhamu atasubiri sana. Nini maana ya nidhamu. Didhamu ni kufanya kile ulichojiambia utafanya bila kuangalia unajisikiaje, wewe  ni kufanya tu. Kwa kawaida mwanadamu ni mvivu. Hiyo ni asili ya kila mmoja wetu. Sasa namna nzuri ya kushughulikia uvivu ni kupangilia mambo yako siku moja kabla na ukiamka unafuata mipango yako na kutekeleza. Achana na kuingiliwa, mara ebu fungua watsapp nimekutumia kitu. Muda wa kusoma watsapp kama zina umuhimu panga na sio kila wakati upo kwenye watsapp. Kufanya hivyo kutakusaidia sana kukuongezea ufanisi.

4.       Fanya mazoezi kila siku ya kujitathmini. Ikifika jioni mara baada ya shughuli. Jitenge peke yako pasipo makelele ya aina yoyote na anza kutathmini siku yako ilivyoisha na jiulize unatakiwa uboreshe nini. Fanyia mazoezi kila siku na utaona unavyo badilika kiutendaji.

5.       Jifunze kusema HAPANA. Maisha ya kufurahisha watu yamepitwa na wakati na pia haioneshi ukomavu. Jifunze kusema hapana na achana kufanya mambo ili uonekane mwema. Tabia ya kupenda kufurahisha watu haitakuacha salama.

6.       Okoa muda kwa kukasimisha shughuli zako. Anza kupitia shughuli ulizopanga iwapo ni lazima uzifanye wewe mwenyewe au waweza mtuma mtu afanye hata kwa ujira kidogo. Mfano nataka kwenda kulipia bima ya gari langu Posta nami niko Mbezi mwisho. Swali la kujiuliza ni kweli hakuna kabisa mtu wa kumpa shughuli hii mpaka mimi mwenyewe niende? Mara nyingi tunajishughulisha na vitu ambavyo tunaweza kukasimisha na kuokoa muda kufanya mambo yenye tija. Anza leo kujiuliza na ukiona iko namna ya kukasimisha basi usifanye.

7.       Unazungukwa na nini nyumbani kwako, ofisini kwako, gerejini kwako nk. Jenga tabia ya kuchambua vitu unavyohitaji na sio kujaza vitu vingi visivyohitajika. Gawa au tupa kama havifai kugawa na baki na eneo lenye kuvutia na hewa sawi inayokuhamasisha kufanya zaidi.

8.       Kuwa bora wewe mwenyewe. Moja ya jambo litakalokusaidia ni aina ya watu wanaokuzunguka. Chagua watu wenye kukuongezea kitu. Achanana kupendelea kila wakati kuzungukwa na watu wanaokutegemea wewe. Kila mara kukusifia yaani hawakufanyi ufikirike bali wewe ndiye mfalme wao. UNAJICHELEWESHA. Zunguka na watu unaopenda maisha yao na yumkini siku moja ufikie hatua waliyo nayo.


Naona niishie hapo kutiririka nitaendelea kesho na Makala hii. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza



Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
                 :www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...