Ruka hadi kwenye maudhui makuu

PATO LAKO KAMWE HALIWEZI KUZIDI UPEO WAKO

Wazo La Leo

Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Watu wengi hujidanganya kwa kujituma sana ili wafikie mafanikio pasipo kuelewa mafanikio yana namna yake na usipoielewa hiyo namna yake itakuwa sawa na kujenga nyumba hewani (Building a castle in the air) au kutwanga maji kwenye kinu.

Ukweli wa mafanikio ni upeo (Personal Development). Una upeo kiasi gani? Au una maarifa kiasi gani kwenye Nyanja zote ambazo unataka kuyaona hayo mafanikio.

Mfano Nyanja ya pesa. Una upeo kiasi gani juu ya pesa. Kiwango ulichonacho kinatueleza upeo ulio nao juu ya pesa. Kamwe huweza kuwa na pesa kuzidi upeo wako na huo ndio ukweli.

Hakuna njia ya mkato, ongeza upeo juu ya pesa na pesa zitaongezeka. Usipoongezeka upeo, sahau kuongeza pato.

Kifupi mafanikio hayatafutwi bali yanavutwa. Ni kama sumaku. Upeo wako utavuta kwa uwiano. Upeo mdogo kila kitu kidogo, upeo wa kati, kila kitu kwa wastani na upeo uliokithiri vivyo hivyo. Hii ndio naita changamoto endelevu. Kadri unavyo lenga makubwa huna budi kuongeza uelewa (maarifa) na utashangaa utakapotengeneza kiu ya kujifunza.

Kadri unavyo weka juhudi kujifunza, kutendea kazi unayojifunza na kufundisha wengine, inabaki suala la muda tu kuona mabadiliko yako.

Ushauri wangu wa bure ‘Acha kujichanganya na mambo. Amua unataka ujazwe na nini (uelimike kwa mambo yapi) ili uweze pata matokeo uyakusudiayo. Basi weka mkakati wa kujifunza hayo mambo na kusahau makelele mengi ya dunia na ukijifunza yaiishi.

Kumbuka kujifunza peke yake hakusaidii kama si mtendaji na utendaji unataka nidhamu. Vinginevyo leo unaanza na kesho unaacha. Badiliko hutokea pale mtu anapozingatia faida na sio kujisikia.

Mimi ni mwandishi na najua faida ya uandishi ni kusaidia kundi kubwa la watu. Hivyo nisipojisikia kuandika NAANDIKA. Nikijisikia kuandika NAANDIKA TU. Hivyo kujisikia au kutojisikia hakunifungi mimi kutenda nililoamua kutenda. Ukiwa na huu msimamo, nakupa miezi sita maisha yako yatachukua sura nyingine.

Mtu mmoja aliwahi sema ‘ Ikitokea pesa azote za dunia zikikusanywa na kugawiwa kwa wanadamu wote duniani kwa usawa, haitochukua muda zitarudi kwenye mifuko ile ile na wale walio kuwa hawana watabaki hawana’.

Tatitizo ni nini? Upeo wa kuwa nazo usipoongezeka utabaki ulivyo.

Furaha kamili haitokani na unachopata bali furaha kamili hupatikana kwa jinsi unavyongezeka (Groth/Personal Development).

Naona niishie hapa. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza. WASAMBAZIE NA WENGINE WAJIFUNZE.

Je unataka kuwa mmoja wa watu wapendao kujifunza? Kundi la watsApp lijulikanalo kwa jina la KARAKANA YA UBONGO ni jibu lako.

Kundi lina watu wasiopungua 200 ambao hubadilishana mawazo yenye tija kila siku.

Kujiunga na kundi hili bofya hapa: https://chat.whatsapp.com/AVwbS3re0jECObi2VK5uzm



Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
                 :www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...