Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SEMINA YA KIMYA KIMYA

Wazo La Leo

Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Leo nimeonelea vyema nigusie ushiriki wa semina ya kimya kimya ambayo ni muhimu sana kushiriki kwa kila asomaye Makala hii.

Somo hili nimejifunza kwa undani kutoka kwa moja wa mentors wangu Mr. Jim Rohn ambaye kwa sasa ni marehemu japo anaishi.

Waweza niuliza kivipi anaishi? Kazi zake zinaendelea kubadilisha maisha ya watu siku hadi siku.

Sasa turudi kwenye mada yetu ya semina ya kimya kimya itakayokusaidia kubadili kabisa maisha yako kama unataka. Maana bado uchaguzi ni wako, name kamwe siwezi kukulazimisha zaidi ya kukueleza.

Semina ya kimya kimya ni hii:

UFUNGUO MKUBWA JUU YA MAISHA YAKO BORA YAJAYO NI WEWE (The MAJOR key to your better future is YOU).

Ninakuomba kama una gari, basi chapisha haya maandishi na uyaweke sehemu ambayo utalazimika kuyasoma kila wakati ukiwa kwenye gari yako.

Kwa kufanya hivyo utakuwa unaendelea kujipatia semina kimya kimya.

Kwa wale wasio na magari, basi chapisha hilo andiko na weka sehemu chumbani kwako itakayo kulazimu uwe unaiona semina yako ya kimya kimya kila wakati. Yaweza kuwa kwenye frigi au kabati la nguo au kitandani. Bado wewe ni muamuzi wa wapi pa kuweka.

Nasisitiza kila mmoja ashiriki semina hii ya kimya kimya na baada ya miezi sita tuletee ushuhuda nini kimetokea kwenye maisha yako.

Wengi hushangaa, umesomaa na jamaa chuo kimoja na wote mnasota kwenye foleni kuelekea ofisini na cha ajabu wote mko ofisi moja lakini mshara wenu unatofautiana pamoja na vyeti ufaulu ni sawa.

Mwenzako analipwa TZS 1,000,000 na wewe unalipwa TZS 200,000. Sababu ni nini?

Si tu kwenye ajira, hata nje ya ajira mwenzako mliyemaliza darasa la saba pamoja na kukosa ufaulu leo hii ana kipato mara kumi ya kwako. Nini tofauti?

Wengine wamejawa na visingizio ati mwenzangu ana muda mwingi. Hebu acha hadithi za sungura. Muda kwa kila mwanadamu ni masaa 24 hakuna wa kuongezewa na hivyo suala la mimi sina muda na yule ana muda ni ujinga tu wa kupangilia vipaumbele.

Kikubwa si muda bali thamani upelekayo sokoni ndiyo inayoamua nani alipwe zaidi na nani alipwe kidogo.

Hiyo ni kanuni ya dunia. Weka thamani kubwa kwenye soko na pokea ujira mkubwa. Suala la muda hapana. Sababu ni kwamba huwezi ongeza muda bali waweza jiongezea uthamani wako kwenye soko na watu wakapanda dau wenyewe hata kabla hujasema kitu.

Sasa unaniuliza: Je na mimi naweza pata mara kumi zaidi ya sasa? Jibu ni ndio iwapo…..

Maisha yetu yajulikana kwa IWAPO utaamua KWANZA kushughulika na WEWE mwenyewe. Maana WEWE ndio tatizo. Uthamani wako ukiongezeka tu, kila kitu kitabadilika.

Naona niishie hapa. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.
Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza. WASAMBAZIE NA WENGINE WAJIFUNZE.
Je unataka kuwa mmoja wa watu wapendao kujifunza? Kundi la watsApp lijulikanalo kwa jina la KARAKANA YA UBONGO ni jibu lako.
Kundi lina watu wasiopungua 200 ambao hubadilishana mawazo yenye tija kila siku.
Kujiunga na kundi hili bofya hapa: https://chat.whatsapp.com/AVwbS3re0jECObi2VK5uzm


Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
                 :www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...