Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UNAFANYA NINI NA PESA YAKO?

Wazo La leo

Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Kama ilivyo safari ya umbari wa kilometa 10 huanza na hatua ya kwanza. Hivyo kamwe usiidharau hatua ya kwanza kwani ni mwanzo wa mwendo mrefu.

Hivyo safari yako ya mwenendo wa pesa huanzia na shilingi moja unayoikamata. Ninachomaanisha hapa kama unatamani uwe mtu wa kumiliki billions of money basi ni muhimu kujua mambo makuu mawili:-

1.       Namna gani waweza kutumia uwezo mkubwa uliko ndani yako au ni kwa namna gani utaanza kuutumia uweza wa ajabu uliko ndani yako kidogokidogo kwa kuongezeka kila siku hadi kufikia hatua ya juu kabisa ya uwezo wako.

2.       Kwa nini utumie rasilimali zako zote.  Rasilimali ambazo twaweza kuongelea leo ni mbili tu, nazo ni MUDA na PESA. Ila mimi kwa siku ya leo nitajikita sana kwenye pesa na hasa pesa uipatayo kama zawadi au kwa kuitolea jasho.

Watu wengi ukitaka kuwafundisha kanuni za kuwa pepari kwa kidogo walicho nacho, utawasikia ningalikuwa na pesa nyingi labda ningeweza kukusikiliza ila pesa nilizo nanzo  ni za kuganga njaa maana zote huishia kwenye matumizi.

Naamini hata wewe msomaji wa makala hii una mawazo ya jinsi hiyo.

Ngoja nikuambie kitu cha muhimu rafiki yangu. Uchache au wingi wa fedha si kitu cha maana kwamba kitakusukuma kuwa na mipango mizuri ya pesa hadi ukafikia hatua ya kuwa bepari, la hasha.

Jambo la muhimu kuliko yote ni mpango wa fedha au kirahisi kanuni ya pesa. Ndugu msomaji, pesa ina kanuni na ni mpaka uielewe  kanuni ya pesa basi utakuwa na uwezo wa kuzalisha pesa, kuzifanya pesa zisikukimbie na mwisho kuendelea kuzirudufu na hivyo neno kufilisika kwako litabaki kuwa historia.

Sasa nije moja kwa moja kwenye kanuni kuu ya pesa (Unayozawadiwa au unayoitolea jasho) maadam inaingia kwenye mkono wako ni LAZIMA UITUMIE KWA KUFUATA KANUNI.

Tabia ya kupata pesa nyingi na kutumia kwa fujo mpaka ziishe si kanuni njema na haitakuacha salama.

Kanuni ya pesa inasema chochote upatacho basi kiingize kwenye kanuni ya 70/30. Maana yake ni nini? Maana ya hii kanuni ni kwamba kamwe usitumie zaidi ya 70% ya pesa uipatayo.

Mfano ukipata TZS 100,000 basi kwa matumizi yako ya kila siku yaani sadaka, chakula, mavazi, kodi ya nyumba na mengine mengi basi YASIZIDI TZS 70,000. Ni bora ule maharage badala ya nyama ili mradi matumizi yako ya juu yasizidi TZS 70,000.

Sasa unafanya nini na hiyo 30% ambayo ni sawa na TZS 30,000. Igawe hiyo pesa katika mafungu makuu matatu:-

1.       10% (TZS 10,000)- Toa Dhaka/au saidia taasisi yoyote inayotoa huduma za kijamii kama vile taasisi za watoto yatima, taasisi za kusomesha watoto wasio na uwezo, namaanisha wazazi wao wameshindwa kumudu gharama, kusaidia wazazi wako kijijini maana huna haja kuanza na wengine kama wazazi wako wanakutegemea kuwatunza. Basi hili liwe fungu lao n.k

2.       10% (TZS 10,000) – Weka akiba kwa lengo la kupata mtaji wa kuanzisha mradi. Mfano unahitaji kuanzisha shughuli za saloon na mtaji ni TZS 300,000, basi weka akiba ya kila 10% ya mapato yatakayo pita mkononi mwako hadi ufikishe huo mtaji. Akiba ikitimia tu TZS 300,000 unaitoa hapo ulipoweka na kufungua saloon.

Ukisha anzisha saloon haimaanishi ndio mwisho wa kuweka akiba, la hasha. Unaanza tena kuweka akiba ila sasa pesa ya akiba itatokana na biashara ya saloon, shughuli zako za kila siku na zawadi utakazo kuwa ukipokea. Swali utafanyia nini? Unatakiwa uwe na wazo lingine la biashara au kufungua saloon nyingine.

Tuseme sasa unataka kufungua mgahawa wa TZS 500,000 basi utaweka akiba na ikifika TZS 500,000 unafungua mgahawa.

Safari ya kuweka akiba ni endelevu, maana kila wakati lazima uwe na mawazo ya kuzalisha na kiwango unacho hitaji ili kuifanya hiyo biashara inayofuata, utaweka akiba ikifika unaanzisha na kamwe usiache hii tabia na kila shughuli yako lazima ichangie 10% kwenda kwenye akiba yenye lengo la kuanzisha miradi mbalimbali. Hivi ndivyo akina mengi, Bakhresa, Aliko Dangote na wengine wengi walivyoanza na sasa hawana shida tena na pesa.

Nashauri anza kumfundisha mwanao na mwambie ni mwiko kutumia pesa yote unayopewa. Mwambie kanuni inakuruhusu kutumia 70% ya chochote upatacho lakini 10% weka kwenye  kibubu na waza mradi wa kuzalisha. Utashangaa mtoto ana mradi wa kufuga kuku, mara anaajili mtu wa kuuza magazeti mara ice cream nk. MFUNDISHE MTOTO AWE NA MSINGI MZURI JUU YA PESA.

3.       10% TZS 10,000 (Investment/Wekeza) – Kiwango hiki cha pesa wape wafanyie kazi wengine na uwe unapokea faida ya pesa yako. Mfano kama ndio unaanza basi anza na UTT kwa kuwekeza kwenye umoja fund ila mambo yakianza kuwa mazuri basi nunua hisa kwenye makampuni. Anza kujizoesha kuwa muwekezaji.

Kesho Mungu akipenda nitawaletea somo la UWEKEZAJI.

Nimalize kwa kukuasa ‘Kama utabadika kutekeleza haya niliyodadavua basi kila kitu maishani mwako kitabadilika’

Naona niishie hapa kutiririka. Mwenye kuelewa na aelewe. Mabadiliko huanza na wewe.

Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia. Pamoja tunaweza



Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
                 :www.bereadytolearn.org
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...