karakanayaubongo@gmail.com
Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 12
Habari za Leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza vyanzo 7 vya umasikini.
Uko msemo usemao ‘Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa’ na sababu ni kutokana na kuyakataa maarifa. Naaamini umewahi sikia ya kuwa maarifa ni nguvu. Kama ilivyo maarifa ni nguvu vivyo hivyo ujinga ni ufu. Watu wengi wangali katika shule ya ujinga na ni sehemu kubwa ya watu wamo kwenye umasikini sababu ya ukosefu wa maarifa.Kimsingi kuna aina 7 za ujinga zenye kusababisha umasikini:-
a. Ujinga wa kutojitabua (Wewe ni nani) – Swali hili wengi hadi niandikapo hawajitambui. Wengi wameendelea kuwa masikini kisa tu hawajajua wao ni akina nani. Najua kuna watu wanajiuliza nina maana gani. Chukulia mfano kama samaki asingejitambua ya kuwa yeye ni samaki na kuamua kuishi nchi kavu unadhani nini ingalikuwa matokeo yake kama si kifo tena cha haraka. Ninachotaka kukuhakikishia ni kwamba ukijitambua ya kuwa uliumbwa kwa kusudio lipi na ukaliishi hilo kusudio ni ngumu kuwa masikini na kuishi maisha yenye karaha. Unaposhindwa kujijua unampa shida hata Mungu kukusaidia maana itakuwa ni mchanganyiko usioeleweka. Mungu anatambua kabisa ya kuwa wewe alikuumba umtukuze kwa uimbaji na wewe uko kwenye udaktari na huna habari kabisa na uimbaji. Mungu anakujia kwenye uimbaji wewe uko kwenye udaktari. Hebu niambie hapo mambo yatakuwaje. Kama kuna jambo la msingi kwa kila mmoja wetu basi ni kujitambua ulikuja duniani kwa kusudi lipi na ukilitambua basi uweze kuliishi. Naomba nikukaribishe tarehe 29.02.2020 kuanzia saa 4 hadi saa 7 mchana tutakuwa tukifundishana namna ya kujitambua. Nitafute kwa maelezo zaidi.
b. Ujinga wa nini ulichonacho – kutojua uwezo ulio nao ni upuuzi mtupu. Wengi ni masikini na wanabaki kuwa masikini kwa kutojua uwezo walinao na hivyo kujikuta walizaliwa wakilia, wanaishi wakitaabika na kufa wakiwa wamekata tamaa.
c. Ujinga wa kutokujua cha kufanya: Unamkuta mtu analalamika nafanya sana kazi lakini hata sisongi mbele. Ukweli ni kwamba mtu hujihusisha na shughuli tofauti na anayotakiwa kuifanya ili impe matokeo mazuri. Kutokujua unatakiwa ufanye nini ni tatizo kubwa na wengi wamebaki wakichimba mashimo na kuyafukia.
d. Ujinga wa kutojua kipi ukiepuke: Kuna vitu vingi vinapigia debe ubaki kuwa masikini mfano wa fikra mbovu juu ya utajiri, tabia zisizoendana nakukutoa nafasi moja na kukupeleka hatua nyingine, mitizamo hasi na mwenendo wa hovyo. Mambo haya humuingia mtu na kujikuta hajithamini tena na wengine kuomba bora kufa kuliko kuishi.
e. Ujinga wa kanuni na mikakati ya kuutengeza utajiri – Siri kubwa imejificha kwenye vitabu, CDs, mafunzo mbalimbali ya kulipia na mengine si ya kulipia ambayo kwa uhakika umfanya mtu ang’amue vitu vingi alivyokuwa havijui. Na asikudanganye mtu mafanikio bila maarifa ni kujidanganya na huwezi pata zaidi ya ujuavyo, ukijua kwa uchache ndivyo na fedha utazipata kwa uchache na kinyume chake. Ni vyema kuweka utaratibu wa kujawa na maarifa na hakuna njia ya mkato, ni lazima ujitoe kupata muda wa kujisomea kusikiliza na kuhudhuria mafunzo mbalimbali.
f. Uvivu – Moja ya dalili ya kumjua mtu mvivu ni kwamba haishi visingizio. Unakuta mtu hana hela lakini anachagua kazi za kufanya na kuishia kuwa ombaomba na hiyo ndio alama kuu ya mtu mvivu.
i. Pia wavivu hawaishi kulaumu wengine. Usidanganyike ugumu wa maisha ulionao mchawi ni wewe mwenyewe acha kuwatafutia watu uchawi.
ii. Wavivu wakipata mpenyo wa kuiba wanaiba. Humuibia hata Mungu fungu la kumi na pia ni wepesi kujiingiza kwenye rushwa na ubadhilifu
iii. Wavivu mara nyingi hujikuta hawana la kufanya kutwa vijiweni
iv. Wavivu hupenda sana kulalala.
v. Wavivu hupoteza muda mwingi kuangalia luninga (television)
vi. Wavivu hupoteza muda mwingi kwenye vitu visivyozalisha
vii. Wavivu ni mabahili kwani hujipenda wao tu hawawafikirii wengine
viii. Wavivu hupenda sana kuairisha mambo hubaki kujisemea nitafanya kesho au siku nyingine au baadae na kuishia kutofanya
ix. Wavivu wengi ni mateja ya ulevi na madawa ya kulevya
g. Kukosa uaminifu – Umegundua ya kuwa ni vigumu sana kuwapata watu waaminifu. Hata makanisani habari hazitofautiani nako wengi si waaminifu. Wengi wamejikuta kwenye dimbwi la umasikini kwa sababu ya kukosa uaminifu. Nawajua watu wengi wenye fedha na wamekosa watu wa kuwaamini kuwapa pesa wazifanyie kazi.
i. Kutokuwa mwaminifu ni kibali cha kuyaharibu maisha.
ii. Kutokuwa mwaminifu huishia kutamani vya wengine
iii. Watu wasio waaminifu ni wabaya na wako tayari kukufanyia chochote kukuumiza
iv. Watu wasio waaminifu huishia katika mateso, kuishiwa na umasikini
v. Watu wasioaminika hawategemewi na hawaaminiki
Ni ngumu sana kupata watu waaminifu. Watu waaminifu ni adimu kupatikana. Kwa maelezo haya je unategemea mtu asiye mwaminifu kufanikiwa? Kamwe sijawahi ona jambazi akistaafu na kuuacha utajiri kwa kizazi chake. Hakika ni ngumu.
Kukosa uaminifu ni sababu tosha ya kwanini hufanikiwi.
Ikitokea umepewa madaraka hakikisha unatumika kwa uaminifu na hiyo itakusababishia heshima na mafanikio
Acha kwa leo niishie hapa. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni
Chapisha Maoni