Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 06)


Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 7
Habari za Leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Jana tulimalizia kwa kusema:-
‘Sasa turudi kwenye mchezo wa fedha.  Mchezo wa fedha unaitwa mchezo wa kujirudufu. Mchezo huu ukiuelewa hutaisahau hii Makala maishani mwako. Nini maana ya kujirudufu. Mfano umepata TZA 200 tunategemea kuna siku utatuambia una 40,000 hii imejirudufu yaani 200x200. Lakini ipo siku tutakusikia una 16,000,000,000. Mbona kama viini macho. Usikose kunifuatilia siku ya kesho ila ninasikitika sijapata wanafunzi makini wanaonifuatilia kwani zoezi nililolitoa ni wawili tu ndio waliojaza’.
Sasa Leo tutaendelea kufafanua ni kwa namna gani twaweza kuucheza mchezo huu wa fedha na kujikuta kila pesa ipitayo mkononi mwetu inaongezeka (inajirudufu – ‘doubling’).
Kama ilivyo michezo mingine, mchezo wa pesa una kanuni ya kufuata na kama ujuavyo kanuni ili kuweza kufuatwa nidhamu ni lazima vinginevyo umaana wa kanuni unapotea.
Tunamaanisha nini tusemapo nidhamu. Nidhamu ni kufanya yale uliyojiambia utakuwa ukiyafanya iwe unajisikia au hujisikii. Hapa ndipo penye mtihani kwa walio wengi.
Mfano mwanariadha mashuhuri duniani akikushauri ya kuwa ili uweze kuwa mashuhuri inakupasa kila siku ukimbie km 5. Kwa kufanya hivyo mwili utakuwa umejiimarisha na kufanya kukimbia kuwa burudani na si ajabu na kuweza kujinyakulia medali.
Sasa shida inaanza kwa yule atakaye naye kuwa mwanariadha mashuhuri anapoanza mara amekimbia na mara ameacha. Je unategemea atakuwa mkimbiaji mashuhuri. La hasha. Kifupi kushindwa kwake ni ukosefu wa nidhamu. Naamini sasa umenielewa nisemapo nidhamu.
Sasa kanuni ya fedha mashuhuri duniani inaitwa 70/30 wengine huitamka 70 kwa 30. Hii ni kanuni mama na unaweza kuinyumbulisha upendavyo ila mtihani mkubwa ni kuitekeleza. Nini maana ya 70/30, kila 1,000 inayopitia mkononi mwako hakikisha unatoa 30% kwanza hizo hutakiwi kuzitumia hata iweje. Kwa lugha nyingine kanuni inakuhitaji kutumia 70% tu ya kila kipitacho mkononi mwako ila 30% zigawe kama ifuatavyo:-
10% - Kama wewe ni mkristo basi hiyo ni Dhaka si mali yako na kwa uaminifu kabisa itoe kanisani na kama wewe si muumini basi usile hiyo 10% bali hakikisha unaitumia kwa kusaidia wahitaji kwa uaminifu .
10% - Unaitunza mahali ambapo si rahisi kuichukua. Mabenki yana account zinaitwa account za malengo wakati mabenki kama NMB wanaita Bonus account. Lengo la account hii ni kuweka akiba pesa ili kudunduliza kufikia mtaji au kufikia kiwango cha pesa ili kutanua biashara yako.
Mfano umetamani kuwa na saloon ya kiume. Basi usihangaike. Anza kuhifadhi kidogokidogo na siku mikifikia kiwango kilizho sawia kuanzisha saloon basi unakwenda kuchuka na kuanzisha saloon. Hii inamaanisha ya kwamba viwango vyako sasa vya mapato vimeongezeka na sasa saloon nayo ikizalisha faida kanuni ni ileile utoa 30% na kuigawa inavyotakiwa na ikifikia kiwango unaanzisha biashara nyingine na unaendelea kuishi namna hiyo na hapo ndipo pesa itakuzoea na kukufanya kutopungukiwa.
10% - Hii ni kwa ajili ya kununua hisa mbalimbali za makampuni yanayofanya vizuri ili baadaye uweze kuwa unapata gawio la faida kila ukifika wakati wa kupokea.
Naona leo niishie hapa ila bado sijaridhika na kujazwa kwa jedwali tajwa hapa chini. Nikuombe ujaze na kunirudishia ni muhimu sana:
JARIBIO LA KUJUA UELEWA WAKO JUU YA MASUALA YA FEDHA (FINANCIAL INTELIGENCE TEST (F.I.T)
Tafadhali weka alama ya vema mahala sahihi
Mfano
Ndio
Hapana
Sifahamu
Na. MAELEZO NDIO HAPANA SIFAHAMU
1 Je wajua hali yako ya kifedha kwa sasa au je wajua utajiri wako una thamani gani
2 Je umeridhika na hali uliyonayo kifedha?
3 Je wajua namna rahisi ya kuongeza kipato chako?
4 Je unayo akiba toshelevu kwa angalau kuendesha maisha yako ya kila siku kwa miezi sita iwapo itatokea kuachishwa kazi au shughuli iliyokuwa ikikuingizia kipato kufilisika?
5 Je una utaratibu wa kuweka akiba kila upatapo pesa?
6 Je tabia ya kuweka akiba imeshakuwa sawia na tabia ya kusafisha kinywa asubuhi? Nina maana hauhitaji kukumbushwa mara upatapo pesa mara moja unaweka akiba. Je umefikia hatua hiyo?
7 Je una malengo mahususi kuhusiana na fedha umbao uko katika maandishi?
8 Je una account bank?
9 Je Kila mwisho wa mwezi unadai bank statement ili kuangalia kama fedha zako ziko salama?
10 Je unaweka kumbukumbu ya mapato na matumizi yako?
11 Je unajua kiasi gani cha pesa unatumia kila mwezi?
12 Je umefikia nidhamu ya kuhakikisha unatumia kidogo kuliko kipato chako?
13 Je una makadirio ya matumizi ya nyumbani kila mwezi?
14 Je huwa unakwepa manunuzi makubwa kwa njia ya mkopo?
15 Je huwa unazitumia akiba zako kwa fursa za uwekezaji zinazojitokeza?
16 Je una uwekezaji wa aina yoyote unaokusaidia kupunguza machungu ya maisha?
17 Je umewekeza sehemu tofauti tofauti kiasi kwamba sehemu moja isipozalisha unafajiwa na sehemu zingine za uwekezaji?
18 Je umeridhika na kipato mupatacho kutokana na uwekezaji wako kiasi kwamba huoni sababu ya kuendelea kuwekeza?
19 Je unahisi kujisikia vizuri kwa kuwa una mshauri mzuri au washauri wazuri juu ya fedha?
20 Je unadhani una bima toshelevu ya maisha?
21 Je una mpango unaoeleweka juu ya elimu ya wanao chuoni au chuo kikuu?
22 Je unamiliki nyumba?
23 Je una mpango wa kustaafu ukiwa na kila kitu pasi kusumbua watoto au ndugu?
24 Je umeandaa wosia wako iwapo ikatokea ghafla ukatoweka duniani?
25 Je una udhibiti mzuri juu ya fedha kwa siku zako za mbele?
26 Je umeridhika kwa mchango wako ulioufanya katika jamii?
Endela kunifuatilia katika Makala zangu nitakuwa nikitiririka juu ya elimu ya fedha na lengo nikukufikisha mahala uweze kuzitawala na zisikutawale, na ujue jinsi ya kuzitunza na kuzifanya zijiongeze kila iitwapo leo.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
                
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...