Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 09)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 9

Leo tena imekuwa siku ya kutiwa moyo sana kutoka kwa mmoja wa wafuatiliaji wa makala zangu za fedha/shekeli kwani ameweza kuniandikia ushuhuda ambao nimeona vyema nawe uweze kuusoma huenda ukaongeza kitu katika safari hii ya kujifunza.


Ushuhuda huu umenifanya niuchukue kama Makala na hapo ndipo namalizia.
Endela kunifuatilia katika Makala zangu nitakuwa nikitiririka juu ya elimu ya fedha na lengo nikukufikisha mahala uweze kuzitawala na zisikutawale, na ujue jinsi ya kuzitunza na kuzifanya zijiongeze kila iitwapo leo.

NA HUU NDIO USHUHUDA WANGU KATIKA MAKALA ZAKO

Habari baba ,na nahisi neno habari haitoshi kuonesha heshima ya salamu kwako ,naomba niwe mwafrika  kabisa ,Kama sio mswahiili ,
SHIKAMOO BABA ,,
Na utaelewa mwishoni maana ya SHIKAMOO yangu kwako.

naam nakuandikia ujumbe huu nikiwa mwenye tabasamu kubwa na furaha ,na kadri utakavyosoma ujumbe huu utaelewa chanzo Cha furaha yangu .

Nimekuwa  nikikufuatilia Sana makala zako ,na Mimi nimekujua MWAKA huu wa 2020 ,ila nimekusoma katika makala zako karibu asilimia 60 hivi ,na naendelea kusoma ,

Makala za mfululizo wa pesa au fedha napenda Kaneno ka shekeli.
Maswali na homework unazoacha zimekuwa zenye nguvu Sana katika akili yangu .Namna napaswa kuwa mwenye nidhamu ya pesa ,mipango ,na uataratibu wa akiba na mpangilio au mgawanyo wa kipato ,ndivyo vilivyo nipiga butwaa ,ndio
Ni Kama nilikuwa naishi gizani hivi kiasi ya kusema kuwa NILIKUWA WAPI ,NA INGEKUWA VIP NISINGEUPATA UJUMBE HUU .Sitamani hata kuwaza ingekuwaje .

Nikukumbushe tu baba yangu kuwa sio Kama sijasoma nimesoma ,lakini mbona Kama mambo haya nimageni ????
Aaa hapana ,sio mageni ila nimegundua kuwa ,na hasa ile MAKALA YA CHUO KIKUU CHA MAISHA ,kuwa elimu ya darasani huenda isikupe mbinu na silaha kamili ya kupambana na MAISHA ya mtaani ,NA HAPA NDIPO MAKALA ZAKO ZINANIPA MBINU MPYA KABISA ZA KUPAMBANA NA MAISHA .

Daa nisamehe Sana baba kwa kuandika maneno mengi ,ila nashindwa kuzuia hisia zangu ,inabidi tu nikwambie , Somo la kuweka akiba ndilo limenishangaza zaidi ,yaani jinsi ya kufanya mgawanyo wa pesa yangu ,KWENYE KUWEKA AKIBA ,MATUMIZI ,Akiba inayoguswa na isiyoguswa KABISA .niliyopata Somo hilo ,sikuchelewa hata kidogo kumwambia mke wangu ,kwani mara nyingi mke ndani ya familia ndo anajenga au kubomoa ,msingi wa uchumi .usiku ulipofika baada  ya chakula Cha jioni na kukiwa na utulivu ,hapo ndipo ikabidi nimuelezee kuhusu MAAJABU YA MAKALA ZAKO . Sikuwahi kabisa kumwelezea mambo ya Makala zako na KARAKANAYAUBONGO ,ila kwa point hii sikuchelewa ,nikamwambia aisome makala moja baada ya nyingine na kuichambua ,
Hakika baada ya hapo Ni historia  ,

Nimavyozungumza tayari tumejiandikia ratiba ya mwezi mzima ya tutakavyo punguza MATUMIZI ,na kuongeza kipato chetu.
Na suala la benk yaani wiki ijayo tunaenda kufungua Account ya akiba na malengo.
Sasa Nina amani kuwa mke wangu kashajua ukweli juu ya Fedha .niseme Nini Mimi ,
Baba nikuhakikishie panapo majaliwa mwezi December ,nakuja na ushuhuda Kama sio kuongeza biashara na kuwa na kakiwanja ,sijui ,ila kwa mbinu hizo nilizojifunza nimenyanyua mikono
MARK MY WORLD ,"IAM FUTURE BILLIONAIRE"Kwa jina la Mwenyezi Mungu .

Baba samahan nimekuchosha haitoshi kuandika hapa ,nakukaribisha nyumbani kwangu ,tafadhari tutembelee baba ,nahisi kuna SIRI ZA AJABU UNAZO JUU YA MAISHA NA UCHUMI .
Nikiwa Kama mwafrika ,kwa heshima kabisa na taadhima
SHIKAMOO BABA , SHIKAMOO BABA , SHIKAMOO BABA

UBARIKIWE BABA.

Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...