Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 10
Habari za Leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza Nyanja za umasikini au kwa lugha nyingine ningeweza kusema vipimo vya umasikini.
Umasikini una Nyanja mbalimbali, lakini kuu ni hizi zifuatazo.
Leo tunakwenda kujifunza Nyanja za umasikini au kwa lugha nyingine ningeweza kusema vipimo vya umasikini.
Umasikini una Nyanja mbalimbali, lakini kuu ni hizi zifuatazo.
1. Umasikini wa kifedha – Hii ni tafsiri ya jumla kwa walio wengi pale mtu anapokuwa na ukame wa fedha. Wengine hupenda kuielezea nyanja hii wakiwaweka watu wote wanaoishi chini ya TZA 2,300 (Dola moja) basi hutafsiriwa ya kuwa ni masikini.
2. Umasikini wa kifikra – Huu ni umasikini wa kimawazo. Hii hutokea pale mtu anakuwa na fedha lakini hana mawazo ya kuzifanya fedha hizo ziendelee kuwa mikononi mwake na hatimaye kujiongezea, kwa kawaida watu wa jinsi hii huishia kupoteza fedha zote wazipatazo. Hakuna umasikini wa kutisha kama utasa wa mawazo na ufahamu juu ya fedha. Mungu atusaidie.
3. Umasikini wa kimahusiano – Kuwa na fedha na wakati huo huo kutokuwa na mtu au watu wa kufurahi nao kwa uwepo wa fedha ulizo nazo ni kuchanganyikiwa. Maisha yenye utasa au umasikini wa mahusiano bora ni maisha ya kuchanganyikiwa (Maisha yasiyo maana au mwelekeo). Hivyo unaweza kuona suala la kuwa na fedha zinazokunyima kufurahi pamoja na mtu au watu wanakuzunguka nao ni umasikini. Rekebisha mahusiano yako, hakuna faida ya kumiliki fedha na kutofurahia. Hii ni hatari. Muombe Mungu usije angukia eneo hili la umasikini.
4. Umasikini wa kimaumbile – Kuishi ukiwa katika hali mbaya kiafya ni umasikini wa kimaumbile. Afya ni utajiri. Ukosefu wa afya kufurahia maisha ni umasikini. Kama ningepata muda wa kukushauri ni kuhakikisha uko makini na kuhakikisha unakuwa na afya iliyo njema kwa kuzingatia mambo yakufanyayo kuendelea kuwa na afya njema kama vile kucheki afya kila baada ya miezi sita au mwaka, kuwa mtu wa mazoezi yaani kuwa na mwili ulio na ukakamavu, kula chakula chenye kuzingatia aina muhimu za vyakula (Balanced diet), kupata muda mzuri wa kupumzika, kuzingatia uwiano wa urefu wako na uzito na mengine mengi. Tembelea hospitali na ongea na madaktari na hata kuwa na muda wa kujisomea mambo yahusiyo afya.
5. Umasikini wa kutosonga mbele (Siku zote uko pale pale) – Kuishi maisha yasiyo na maendeleo yaaani yenye kupiga hatua ni maisha haramu. ‘Alizaliwa. Aliishi na hatimaye kufa’. Maisha yasiyoacha alama yaani hakuna mtu anayejua kama ulikuwapo. Uwepo wako na kutokuwepo vyaonekana ni sawa ni umasikini mbaya sana. Tafuta kusudi la wewe kuweza kuwepo katika sayari hii na ukaliishi kusudi hilo ili kuleta radha ya maisha. Mungu atusaidie.
6. Umasikini wa ujinga – Ukosefu wa maarifa, taarifa na ujuzi wa kukufanya uweze kupiga hatua maishani nao ni umasikini. Kutokuwa na taarifa ni kujimaliza na ni haramu ya mabadiliko.
7. Umasikini wa Kiroho – Kutokuwa na Imani na Mungu (Yesu Kristo) na kukosa agano la uhusiano na huyo Mungu ni umasikini. Tukumbuke kuna maisha baada ya kufa. Hivyo kufanikiwa nje ya Yesu Kristo ni maisha ya utupu na ndio umasikini wa kutupwa. Kwa taarifa yako kiini cha utajiri wa kweli ni Yesu Kristo maana anabainisha ya kuwa alifanywa masikini ili sisi tuwe matajiri. Ni Imani katika Mungu kupitia YESU KRISTO PEKEE NDIO KITU CHA KUSHIKAMANA NACHO NA SINA LUGHA NYINGINE YA KUSISITIZA. Salimisha maisha yako kwa Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Maneno matakatifu yanasema wazi kabisa ‘Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki zake na mengine utazidishiwa’.
Je wewe ni masikini? Naamini sasa watambua vyema kama wewe ni masikini au la. Watu wengi ni masikini na wanabaki kuwa masikini kwa sababu tu hawajui kwanini wao ni masikini. Inapotokea watu hawajui ni nini kimesababisha kuwa masikini, huendelea katika ujinga na kubaki kuwa masikini.
Kuendelea kuishi kama ambavyo umekuwa ukiishi miaka nenda miaka rudi na kutegemea mabadiliko ni ukichaa. Haya shime tujibidishe kuvitambua visababishavyo umasikini tuweze kujikwamua. Mabadiliko huanza na wewe.
Acha kwa leo niishie hapa. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.

Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni
Chapisha Maoni