Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 11)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 11

Habari za Leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza ‘UMASIKINI HAUHESHIMU MTU, UMRI, RANGI, CHEO, SEHEMU AISHIYO AU DINI YAKE.’

Nikuombe sasa tusafiri pamoja kwa njia ya kuwazua. Hebu fikiria mtu aliyenunua pasi ya umeme na kuanza kuhangaika kupasia nguo kwa pasi ya umeme pasipo kuiunganisha kwenye switch ili pasi ipate moto na kuweza kupasia nguo; Lakini cha ajabu kuishika tu pasi kazi ya kupasia ikaanza mara moja na huku akiendelea kustaajabu ni kwa nini nguo hazisikii pasi ambayo kwa uhakika ni nzuri kwa muonekano.

Jitihada ziliendelea hata kutumia vitufe vya kubadili kiwango cha joto kwenye pasi lakini pasi mafanikio.

Baada ya mahangaiko ya kutosha ndipo aliamua kukisoma kijitabu kilichoambatana na hiyo pasi na kugundua ya kuwa kuna hatua muhimu na ndio ya kwanza ilipuuzwa ambayo nikuunganisha plug ya pasi kwenye socket ili kupata moto na kuweza kupasia mara moja. Ni kivipi waweza tumia pasi ya umeme pasipo kuiunganisha kwenye socket ya umeme. Plug ya pasi ikiwa imeunganishwa kwenye soketi juhudi zote za kupasia nguo zitazaa matunda.

Ninachotaka ukijue siku ya leo ni kuwa juhudi za kupasia nguo hazikuwa mbaya lakini zilishindwa kutoa matokeo chanya kwa sababu moja kuu kutounganishwa kwenye socket ambako ndio upatikanapo moto wa kuwezesha kupasia.

Wengi wetu ni kama huyu mtu, Tunafanya kila tuwezayo kuyafanya katika maisha kuboresha maisha yetu lakini cha ajabu tunabaki tukiwa masikini ni kwa sababu hatutajiunganisha na yale yawezayo kubadilisha kabisa historia zetu na kupuuzia kijitabu cha taarifa ya jinsi gani juhudi zetu zaweza zaa matunda.

Ili tuweze kuwa matajiri ni muhimu kwanza kujua kwanini tu masikini.

Hebu tafakari haya maswali mawili muhimu ambayo kila siku tujithamini na tuone kwanini moja ya swali si vyema kujiuliza na linguine ni jema.

NIFANYE NINI KUWEZA KUWA TAJIRI – X
KWA NINI MIMI SI TAJIRI - √

Wengi wetu tumejitaabisha na hata kufanya utafiti wa nini tufanye ili kufikia utajiri badala ya kujiuliza kwa nini tu masikini kwani kwa kufanya hivyo tutagundua vipingamizi ambavyo tutaweza pambana navyo na kujinasua kwenye dimbwi la umasikini.

Bila kujali unaishi wapi umasikini ni matokeo ya sababu zilizo chini ya mambo 7 muhimu ambayo ukiyajua basi itakurahisishia kupambana na umasikini.

Acha kwa leo niishie hapa. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.

Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...