Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA / SHEKELI (SEHEMU YA 13)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 13

https://www.instagram.com/p/B825rFVplbT/?igshid=2e3wb6kv1jq1

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya kujisikia utoshelevu kutokana na mafanikio au kujisikia kutokanako na ujuzi maalum unaokufanya ujione si wa kawaida, kifupi hali hii inajulikana kama kiburi yaani kujivunia ulivyonavyo iwe ni mafanikio au ujuzi wa kipekee miongoni wa jamii inayokuzunguka. Kwa walio wengi huambatana na mabadiliko hata ya jinsi ya kutembea na hata ongea yao huwa ya tofauti. Mungu tusaidie.

Nimeshuhudia watu wengi wakiwa hawana kazi za kufanya. Kiburi ni mojawapo ya sababu ya umasikini kwa maisha ya walio wengi.

Watu wenye kiburi hawafundishiki na hukataa kufuata maelekezo ambayo yangeweza kuwaepusha na uharibifu.
Watu wenye kujisikia hufanya kosa moja la msingi hasa pale wanapojiona wao ni bora kuliko na kusababisha hata koti wazivaazo kushindwa kuzikata kwa saizi za kimo chao na kulingana na aina ya kitambaa.
Watu wenye kiburi hujitahidi kuepuka kujishughulisha au kuanzisha shughuli ndogo ndogo au kuanzia pale walipo kutokana na kujidangaya kwa kujiona wao ni watu wa matawi ya juu. Acha kujidanganya aliye matawi ya juu ni Mungu peke yake maana Yeye mali na dhahabu ni vyake.

Usidanganyike utakapo nyazifa za juu kama ukurugenzi ni lazima uwe na vyeti vyenye ufaulu na sifa sitahiki na sio tu kujiona ati unafaa. Huo ni wendawazimu.

Hebu tuangalie moja ya vitabu vyenye hekima jinsi kiburi kinavyoshughulikiwa

‘Amsingiziaye jirani yake kwa siri, huyo nitamharibu. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, huyo sitavumilia naye.’ Zaburi 101:5

Mungu kamwe hawezi kumvumilia mtu mwenye kujisikia kwa namna yoyote kwani mtu wa jinsi hiyo milango ya baraka za kimungu imefungwa.

‘Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali’ Zaburi 138:6’

Jambo la kuzingatia ni kuwa Mungu huwatambua wote wenye viburi na kuwaweka mbali na mafanikio. Usitegemee kuwa na mafanikio na huku u mwenye kiburi. Kwa Mungu sahau kabisa labda kwa shetani.

‘Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu, Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.’

Wenye kiburi huishia katika aibu ya kuwa masikini. Hubakia tu na historia - enzi zake yule…

‘Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.’ Mithali 13:10

Kiburi hakiwapi chochote kizuri kwa wenye kiburi. Laiti wangalijua mwisho wao si mzuri wangejirudi na kumrudia Mungu.

‘Bwana ataing’oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane.’ Mithali 15:25

Hata ikitokea watu wanaojisikia wakafanikiwa katika kujilimbikizia mali; Mafanikio hayo kamwe huwa hayadumu kwani Mungu huwashusha hadi kufikia hatua ya chini kabisa ambayo hapo awali wao waliiona kama kinyaa na ndipo huishia.

‘Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu.’ Mithali 16:5

Kuruhusu kiburi moyoni ni kumfanya Mungu akuchukie na haijalishi unafanya nini, mwisho wake huwa ni aibu. Mungu huwapenda wanyenyekevu na kuwapinga wenye kiburi. Ndugu zangu tujifunze unyenyekevu na kudumu huko iwapo twahitaji mafanikio yenye misingi ya Kimungu. Mungu atusaidie.

‘Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.’ Mithali 18:12

Mwonapo mtu mwenye kiburi jua kwa hakika anaelekea kwenye uharibifu.

‘Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.’ Mithali 29:23

Kiburi humshusha mtu chini, na hii ndiyo sababu ya kwa nini kiburi ni chanzo cha umasikini

‘Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?

‘Ujapopanda juu kama tai, ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; Asema Bwana.’ Obadia 3-4

Du! Ni hatari kiasi gani kiburi husababisha kwa mwenye nacho. Kiburi ni udanganyifu na kama tulivyoona hakuna namna kwa mwenye kiburi kuepuka umasikini. Mungu atusaidie.

‘Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Na dunia inapita, pamoja na tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyae mapenzi ya Mungu adumu milele.’ 1Yohana 2:15-17

Kiburi si cha Mungu bali ulimwengu, na Mungu hana la kumsaidia kwa chochote mtu mwenye kiburi.

‘Kwa hiyo hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.’ Yakobo 4:6.’

Mungu yu kinyume na humpinga mwenye kiburi. Unapokuwa mwenye kiburi, Mungu huwa kizuizi cha wewe kufanikiwa au kuendelea, na kama Mungu yu kinyume nawe, ni nani atakaye kusaidia. Mwenye ufahamu na aelewe hili.

‘Jidhilini mbele za Bwana, Naye atawakuza.’ Yakobo 4:10

Hekima hukuhitaji ukatae kiburi katika ujumla wake na jinyenyekeze ili Mungu aweze kukukweza/kukuinua na kukupandisha hadi kwenye eneo la utele.

Acha kwa leo niishie hapa. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.

Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la WhatsApp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...