Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 15)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 15

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya Laana.
Kama ambavyo tumejifunza katika Makala zilizotangulia, umasikini ni roho na pia laana. Hakuna jinsi ya kukwepa kuuelezea umasikini pasipo kuhusisha nyanja ya roho.
Ninachotaka ukijue pasi shaka ni kwamba baadhi ya umasikini ni kutokana na laana.

‘Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.
Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,
Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.’ KUMBUKUMBU LA TORATI 28:15-20

Uturehemu Bwana! Umeona jinsi ambavyo maisha ya watu yanavyoathiriwa na laana za umasikini! ‘Kwanini mwanadamu asimtii Mungu na kusababisha madhara yote tuliyoyasoma hapo juu? Hili ni swali ambalo yeyote aweza jiuliza. Jibu lake ni rahisi kabisa. roho ya umasikini humshawishi mwanadamu kwenda kinyume na maagizo na njia za Mungu ili umasikini uendelee kumkandamiza

‘Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.’ MWANZO 3:17-19

Kutokutii kwa mwadadamu na dhambi ya Adam vilileta laana kwa mataifa yote. Kuishiwa, ugumu wa maisha, na umasikini ukifuatilia kwa makini kwa kuisoma biblia utagundua ya kuwa umasikini hakuwapo kabisa katika bustani ya edeni na dunia nzima hadi pale mwanadamu alipoamua kutomtii Mungu.

‘Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.
Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.’ MWANZO 8:20-22


Mbegu ya kujitoa iliyokuwamo ndani ya Noah ilimfanya aweze kuivunja laana katika nchi.
Mbegu ilikuwamo ndani ya Noah na kusabaisha kuivunja laana ilileta kanuni ya milele juu ya kuvunja laana inayojulikana kama ‘KUPANDA NA KUVUNA’
Mungu alianzisha kanuni hii ya kupanda na kuvuna ikiwa ni njia ya kumuwezesha mwanadamu kuondokana na laana ya umasikini lakini kutokuitii kumefanya laana hii iendelee.

- Ni roho ya umasikini ikufanyayo uwe mchoyo si tu kwa Mungu bali hadi kwenye ufalme wake.

- Ni roho ya umasikini ndiyo inakufanya ushindwe kuitii kanuni ya Mungu ya mafaniko.

- Ni roho ya umasikini ikufanyayo kutokuwa mwaminifu kwa Mungu, neno lake na njia zake.

- Ni roho ya umasikini ikufanyayo uringe na kuwa na kiburi juu ya wasaidizi wako.

- Ni roho ya umasikini inakufanya na kuendelea kuwa mvivu.

- Ni roho ya umasikini ndiyo inakukimbiza mbali na taarifa unazotakiwa kuzijua ili historia ya maisha yako iweze badilika. Hivyo inakufanya uridhike na ujinga.

Umasikini ni laana na ni lazima ivunjwe.

‘Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.’ Wagalatia 3:13-14


Habari njema ni kwamba Yesu Kristo alikwisha lipia kutunasua kwenye laana na tupoamua kufanya agano la kuwa watoto wa Mungu, laana ya umasikini inakuwa haina nguvu ya aina yoyote kutuendesha na kututumikisha ISIPOKUWA pale tunapoamua kuialika na kuiruhusu iturudie katika maisha yetu kupitia ujinga, kutokuwa waaminifu,uvivu, kiburi,dhambi, kutotii na kuendekeza vitabia vyenye kualika laana, mitizamo hasi na mifumo mibaya ya maisha.

‘Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.’ Mhubiri 10:8

Kila mtoto mwenye agano la kumtumikia/kumuishia Mungu ana ngome maalum yakutoguswa na laana zilizochambuliwa hapo juu ila inapotokea mwanadamu akaivunja tunakuwa tumemruhusu adui atutawale
Itunze kinga ya Mungu na laana ikae mbali nawe.
Wengi ni masikini kwasababu tu wako chini ya laana.

Utakumbuka ya kuwa hadi sasa tumekwisha jifunza juu ya  aina sita za laana zinazotesa dunia na kabla sijaelezea kisababishi cha mwisho kinachosababisha umasikini, napenda kusisitiza tena kuchukulia kweli zote kwa kumaanisha na kufanya maamuzi ya kumuishia Mungu kikamilifu kwa kumpa maisha yako, si kwa kubaki katikati yaani kuendelea kumpenda Mungu na wakati huo huo kumpenda shetani. Hili huna budi kulizingatia kwa sababu ni hatari kwa kuuelewa ukweli na ukaupuuza.
Pambana na ujinga bila kuchoka.
Pinga uvivu kwa nguvu zote
Epuka kutokuwa mwaminifu kama ambavyo unaepuka magonjwa ya kuambukizwa.
Epuka kiburi kama ambavyo unaepuka magonjwa ya kuambukiza.
Kataa kutokutii pasi kuchoka.
Usitoe nafasi tena kwa laana kuanzia sasa.
Yafanye niliyokufundisha na historia yako itabadilika.
Acha kwa leo niishie hapa. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...