Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA/ SHEKELI(SEHEMU YA 06)


Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 6
Habari za Leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo nataka ufikirie jambo moja na ndilo litatusaidia katika safari yetu ya Makala kuhusiana na pesa. Jambo lenyewe ni ‘KIASI GANI TOKA UZALIWE KIMEPITA KATIKA MIKONO YAKO?’. NA NI KIASI GANI BADO UNACHO AU UMEWEKEZA NA SASA UNAKULA MATUNDA YA KUWEKEZA. Naomba nijibiwe hili swali. Nakuomba uje inbox tujadili. Na kama swali hili limekuuzi ni Dhahiri kuwa huna ujuzi wa kucheza mchezo wa fedha na ndio maana umekasirika maana kila ukipatacho lazima kiishe na kuanza mahangaiko tena na baadhi yetu ukiwa na fedha mtaa mzima watajua. Hiyo ni hatari. Mungu atusaidie kuujua na kuucheza vizuri mchezo wa fedha.
Mchezo wa fedha hautofautiani na michezo mingine unayoifahamu mfano mpira wa miguu, mpira wa vikapu, kukimbia mbio n.k.
Siri ya kila mchezo ni kujirudia rudia. Nina maanisha nini. Ukitaka kuwa mchezaji bora wa mpira wa miguu basi ondoa kujihurumia. Itakupasa kujituma mazoezini na hata wengine wakipumzika wewe unakwenda mazoezini. Wako wachezaji wengine lazima kila siku wapande milima na kushuka. Si kazi ndogo maana kama kawaida ya mwili hautaki shida na mara zote ukimsikia mtu anaongea sijisikii au nimechoka, hapo jua ni sauti ya mwili na yeye amejikuta anatoa ushirikiano na kushindwa kutekeleza alichotaka kutekeleza kwa kusalimu amri kwa mwili unavyoongea. Huku tunaita ni kuishi kwa kuongozwa na hisia na sio faida.
Naomba nikuibie siri moja na labda unaijua. Mimi ni mtoto wa mkulima na mama yangu alikuwa akitulazimisha kwenda shamba hadi tukapenda baada ya kwenda mara nyingi.
Sasa kuna wakati tulikuwa tunamaliza shamba letu na wengine wakiwa bado na hivyo tukawa tunafanya vibarua kujipatia pesa. Vibarua hivyo vya kulima kuna namna unapimiwa, vipimo hivyo huitwa mraba.
Sasa naikumbuka siku niliyadhamiria kulima miraba mitatu badala ya miwili niliyozoea. Kuzoea hujenga tabia. Nilipomaliza tu miraba miwili mwili ulinipa taarifa ya kuwa hapa haendelei mtu nami kwa kuwa niliitaka pesa ya miraba mitatu nikajilazimisha huku nikiwa nimechoka na mwili hautaki ni kana kwamba nilianzisha vita na mwili wangu mwenyewe na baada ya kuendelea kwa shida ghafla nikashangaa uchovu umetoka na kazi nika piga utadhani ndio kwanza naanza kulima. Kitendo hicho hadi leo kimenijengea tabia ya ajabu. Mimi siku yangu huanza saa kumi asubuhi. Na kazi niifanyao kwa sasa kwa siku moja mwingine huifanya kwa siku tatu. Sijui kama unajifunza kitu. Ukweli wa mambo ni kuwa ile nguvu iliyofichika ukiibua lazima itakupa utofauti wa maisha.
Hiyo ndiyo siri ya watu wote wanaoitwa mastaa kwakuwa wanajiongeza wakati wengine wakijihurumia.
Sasa turudi kwenye mchezo wa fedha.  Mchezo wa fedha unaitwa mchezo wa kujirudufu. Mchezo huu ukiuelewa hutaisahau hii Makala maishani mwako. Nini maana ya kujirudufu. Mfano umepata TZA 200 tunategemea kuna siku utatuambia una 40,000 hii imejirudufu yaani 200x200. Lakini ipo siku tutakusikia una 16,000,000,000. Mbona kama viini macho. Usikose kunifuatilia siku ya kesho ila ninasikitika sijapata wanafunzi makini wanaonifuatilia kwani zoezi nililolitoa ni wawili tu wamerudisha majibu. Kweli mchezo wa pesa utauweza? Kama unapenda kujaza na kunirudishia nitashukuru, maswali yapo hapa chini:-
JARIBIO LA KUJUA UELEWA WAKO JUU YA MASUALA YA FEDHA (FINANCIAL INTELIGENCE TEST (F.I.T)
Tafadhali weka alama ya vema mahala sahihi
Mfano
Ndio
Hapana
Sifahamu
MAELEZO
  •NDIO   •HAPANA •SIFAHAMU •
1 Je wajua hali yako ya kifedha kwa sasa au je wajua utajiri wako una thamani gani
2 Je umeridhika na hali uliyonayo kifedha?
3 Je wajua namna rahisi ya kuongeza kipato chako?
4 Je unayo akiba toshelevu kwa angalau kuendesha maisha yako ya kila siku kwa miezi sita iwapo itatokea kuachishwa kazi au shughuli iliyokuwa ikikuingizia kipato kufilisika?
5 Je una utaratibu wa kuweka akiba kila upatapo pesa?
6 Je tabia ya kuweka akiba imeshakuwa sawia na tabia ya kusafisha kinywa asubuhi? Nina maana hauhitaji kukumbushwa mara upatapo pesa mara moja unaweka akiba. Je umefikia hatua hiyo?
7 Je una malengo mahususi kuhusiana na fedha umbao uko katika maandishi?
8 Je una account bank?
9 Je Kila mwisho wa mwezi unadai bank statement ili kuangalia kama fedha zako ziko salama?
10 Je unaweka kumbukumbu ya mapato na matumizi yako?
11 Je unajua kiasi gani cha pesa unatumia kila mwezi?
12 Je umefikia nidhamu ya kuhakikisha unatumia kidogo kuliko kipato chako?
13 Je una makadirio ya matumizi ya nyumbani kila mwezi?
14 Je huwa unakwepa manunuzi makubwa kwa njia ya mkopo?
15 Je huwa unazitumia akiba zako kwa fursa za uwekezaji zinazojitokeza?
16 Je una uwekezaji wa aina yoyote unaokusaidia kupunguza machungu ya maisha?
17 Je umewekeza sehemu tofauti tofauti kiasi kwamba sehemu moja isipozalisha unafajiwa na sehemu zingine za uwekezaji?
18 Je umeridhika na kipato mupatacho kutokana na uwekezaji wako kiasi kwamba huoni sababu ya kuendelea kuwekeza?
19 Je unahisi kujisikia vizuri kwa kuwa una mshauri mzuri au washauri wazuri juu ya fedha?
20 Je unadhani una bima toshelevu ya maisha?
21 Je una mpango unaoeleweka juu ya elimu ya wanao chuoni au chuo kikuu?
22 Je unamiliki nyumba?
23 Je una mpango wa kustaafu ukiwa na kila kitu pasi kusumbua watoto au ndugu?
24 Je umeandaa wosia wako iwapo ikatokea ghafla ukatoweka duniani?
25 Je una udhibiti mzuri juu ya fedha kwa siku zako za mbele?
26 Je umeridhika kwa mchango wako ulioufanya katika jamii?
Endela kunifuatilia katika Makala zangu nitakuwa nikitiririka juu ya elimu ya fedha na lengo nikukufikisha mahala uweze kuzitawala na zisikutawale, na ujue jinsi ya kuzitunza na kuzifanya zijiongeze kila iitwapo leo.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
                
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...