Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 14)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 14

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya KUTOTII.

Ni nani awezaye kuwa na mtu aliye mwajiri asiye pokea maagizo yote ampayo, asiye tii taratibu zote mahali pa kazi, anayeishi na kufanya apendavyo yeye, na bado ukaendelea ukampandisha cheo katika kampuni yako? Ni nani awezaye kufanya hivyo? Tafakari. Nina mashaka hata wewe unayesoma hii makala kama unaweza fanya hivyo kwa mwajiriwa wako. Kama mfanyakazi asiye tii hawezi kamwe pata kupandishwa cheo; Vipi sasa umtegemee Mungu kukubariki ukiwa humtii?
Kutokutii kumewatenga wengi kufikia eneo la mafanikio. Kuna Nyanja mbili za kutotii ambazo zimewagharimu wengi kutofikia mafanikio:-

1. Kutotii amri na maagizo ya Mungu.
2. Kutofuata kanuni na sharia za kukufikisha kwenye mafanikio ‘Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.’ ISAYA 1:19-20

Kuna masharti mawili yamwezeshayo mtu’kula mema ya nchi.’



KUBALI na KUTII. Nimeshuhudia wengi wakikubali bali wachache ndio hutii. Kukubali tu haitoshi kabisa. Ni lazimautii sharia na kanuni zitakazokusababishia ‘ule mema ya nchi’.

‘Kama wakisikia na kumtumikia, watapisha siku zao katika kufanikiwa, na miaka yao katika furaha. Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga,  nao watakufa pasipo maarifa.’  Ayubu 36:11-12


Hapa pia twaweza ona masharti mawili ‘KUSIKIA NA KUTII’
Wengi wanasema wanamtumikia Mungu lakini ni kutokana na tafsiri zao na si Mungu awaonavyo. Kuwa makini kufurahisha binadamu na kumchukiza Mungu. Moyo wa mwanadamu una tabia ya kufisha ni nani awezaye kuujua. Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo – uyawazayo na kuyatenda yashabiane kwani Mungu huuangalia moyo. Nini msukumo ukufanyao ufanye unacho fanya. Je ni sifa? Au uonekane? Jiepushe na unafiki Mungu wetu ni wa haki.
Wengi huamua kutofuata maagizo ya Mungu yawafanyao wasijisikie vizuri katika nafsi zao. Kumtumikia Mungu pasipo utii ni kosa kubwa sana na kujipotezea muda maana hakuna mbingu ya wasiotii. Kumsikia na kumtii Mungu hukufanya kuwa mmojawapo ya watu watakao ufikia mji wa mafanikio na kuishi maisha ya furaha. Kutii ni ufunguo wa Baraka za Mungu.

‘Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidi, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote duniani; Na Baraka hizi zote zitakujia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana Mungu wako.’ KUMBUKUMBU LA TORATI 28:1-2

Nikuombe kwa wakati wako endelea kujisomea mstari wa tatu hadi wa kumi na nne upate kuona orodha ya Baraka ambazo Mungu ameziahidi kwa wale wote watakao tii maagizo yake. Kama kuna kitu kisichowezekana kwa mwanadamu awaye yote nikimaanisha hata wewe unayesoma, haiwezekani mtu akawa mtii na wakati huo huo akawa masikini. Kamwe vitu hivi viwili havikai pamoja. Ukitii maagizo ya Mungu mafanikio ni urithi wako.

‘Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.’ KUMBUKUMBU LA TORATI 28:15

Nikuombee sasa uendelee kusoma mstari wa kumi na sita hadi mwisho wa mlango huu wa 15 ushuhudie orodha ya laana za kutisha zitazoambatana na wasiotii katika maisha yao. Haiwezekani kuendelea kuishi maisha yasiyo na utii na huku utegemee maisha yenye Baraka na mafanikio toka kwa Mungu.

‘Naye Samwel akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu sawasawa na kutii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya bebeeru. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.’ 1SAMWELI 15:22-23

Nakushauri usome sura nzima ya kumi na tano ya 1SAMWELI ili uweze jipatia picha ya safari ya kutokutii kwa Sauli. Ni bora kumtii Mungu kuliko kumuhonga na uyapatayo ndani ya kutokutii kwako.
Wengi hujidhania ni watii lakini ni kwa sababu hawayajui haya:-

Kuchelewa kutii ni kutokutii
Kutii kwa sehemu nayo ni kutokutii
Kutii kiaina nako ni kutokutii
Kutii kwa sehemu nako ni kutokutii

‘Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, Yasikieni maneno ya maagano haya; ukaseme na watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; ukawaambie, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu asiyeyasikia maneno ya maagano haya, niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuru ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu; ili nipate kukitimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi ijaayo maziwa na asali, kama ilivyo leo hivi. Ndipo nikajibu, nikasema, Amina, Ee Bwana. Naye Bwana akaniambia, Hubiri maneno haya yote katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ukisema, Yasikieni maneno ya maagano haya, mkayafanye.’ Yeremia 11:1-6

Tii na ufurahie upaji wa kimaagano na baraka kutoka kwa Mungu Muumbaji.
Je unatii amri na maagizo ya Mungu ambayo yenye mahusiano makubwa na mafanikio ya upatikanaji wa fedha/shekel? Je wewe ni mtiifu usiyekumbushwa kumtolea Mungu fungu la kumi bali ni jambo ambalo hulifanya kama vile uamkapo na kusafisha kinywa bila kuambiwa au kushurutiwa? Je wewe u mtoaji wa kujitoa (sacrifice giving) katika maisha yako? Namna unavyoyaishi haya yakupasayo kuyatenda yanakuamulia ya kuwa uwe mwenye kufanikiwa au la. Ukiyavunja maagano ya Mungu nayo yatakuvunja.

Kama unaona vyuma kwako vimekaza na kujikuta umeingia kwenye maisha ya kubangaiza, jichunguze je  umwaminifu katika utoaji wa fungu la kumi? Na kama una ukata wa fedha, jitathimini maisha yako ya utoaji.

Wengi ni masikini kwa sababu tu hawatii kanuni na sheria za kibiblia za kiuchumi.


Acha kwa leo niishie hapa. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.

Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...