Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 3
Habari za Leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli. Leo nimeona vyema nikupeleke maabala ili kujua hali yako kifedha ili nijue namna ya kukuhudumia.
Tafadhali jaza vizuri jedwali tajwa hapo chini na unirudishie niweze kujua namna ya kuendelea kuelimisha na namna ya uelimishaji ili mwisho wa siku uweze kunufaika nah ii elimu ya fedha.
JARIBIO LA KUJUA UELEWA WAKO JUU YA MASUALA YA FEDHA (FINANCIAL INTELIGENCE TEST (F.I.T)
Tafadhali jibu kwa kuandika mojawapo ya maneno yafuatayo kwa kila swali mahali sahihi
Mfano
Ndio
Au
Hapana
Au
Sifahamu
1
Je wajua hali yako ya kifedha kwa sasa au je wajua utajiri wako una thamani gani?
2
Je umeridhika na hali uliyonayo kifedha?
3
Je wajua namna rahisi ya kuongeza kipato chako?
4
Je unayo akiba toshelevu kwa angalau kuendesha maisha yako ya kila siku kwa miezi sita iwapo itatokea kuachishwa kazi au shughuli iliyokuwa ikikuingizia kipato kufilisika?
5
Je una utaratibu wa kuweka akiba kila upatapo pesa?
6
Je tabia ya kuweka akiba imeshakuwa sawia na tabia ya kusafisha kinywa asubuhi? Nina maana hauhitaji kukumbushwa mara upatapo pesa mara moja unaweka akiba. Je umefikia hatua hiyo?
7
Je una malengo mahususi kuhusiana na fedha umbao uko katika maandishi?
8
Je una account bank?
9
Je Kila mwisho wa mwezi unadai bank statement ili kuangalia kama fedha zako ziko salama?
10
Je unaweka kumbukumbu ya mapato na matumizi yako?
11
Je unajua kiasi gani cha pesa unatumia kila mwezi?
12
Je umefikia nidhamu ya kuhakikisha unatumia kidogo kuliko kipato chako?
13
Je una makadirio ya matumizi ya nyumbani kila mwezi?
14
Je huwa unakwepa manunuzi makubwa kwa njia ya mkopo?
15
Je huwa unazitumia akiba zako kwa fursa za uwekezaji zinazojitokeza?
16
Je una uwekezaji wa aina yoyote unaokusaidia kupunguza machungu ya maisha?
17
Je umewekeza sehemu tofauti tofauti kiasi kwamba sehemu moja isipozalisha una sehemu zingine za uwekezaji?
18
Je umeridhika na kipato upatacho kutokana na uwekezaji wako kiasi kwamba huoni sababu ya kuendelea kuwekeza?
19
Je unahisi kujisikia vizuri kwa kuwa una mshauri mzuri au washauri wazuri juu ya fedha?
20
Je unadhani una bima toshelevu ya maisha?
21
Je una mpango unaoeleweka juu ya elimu ya wanao chuoni au chuo kikuu?
22
Je unamiliki nyumba?
23
Je una mpango wa kustaafu ukiwa na kila kitu pasi kusumbua watoto au ndugu?
24
Je umeandaa wosia wako iwapo ikatokea ghafla ukatoweka duniani?
25
Je una udhibiti mzuri juu ya fedha kwa siku zako za mbele?
26
Je umeridhika kwa mchango wako ulioufanya katika jamii?

Endela kunifuatilia katika Makala zangu nitakuwa nikitiririka juu ya elimu ya fedha na lengo nikukufikisha mahala uweze kuzitawala na zisikutawale, na ujue jinsi ya kuzitunza na kuzifanya zijiongeze kila iitwapo leo.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: KARAKANA YA UBONGO
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni
Chapisha Maoni