Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 04)


Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 4

Habari za Leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli. Bado sijapata mtu aliyenitumia majibu ya maswali niliyoyauliza jana. Hata hivyo leo nimeona vyema tuelezane juu ya ‘WATU WENGI HUTAZAMA BALI WACHACHE WANAONA’

Hakuna kitu kinafurahisha na kuburudisha pale masikini anapotamka ‘Mimi si masikini’.Watu wengi huelezea umasikiti na utajiri wakioanisha na fedha ambazo mtu humiliki na kupoteza kabisa maana ya ndani ya hilo neno.

Je wewe ni masikini?

Wengi huelezea masikini kuwa ni kinyume cha:

a.       Kuwa na siha njema (afya) pamoja na mali na fedha lukuki. 
b.      Pia wengine wanasema ni kuwa na fedha nyingi na umiliki wa mali mbalimbali

Hivi ndio wengi hutafsiri umasikini na pia utajiri. Naamini unakumbuka somo letu la kwanza ambapo tulijifunza ya kuwa ili mtu kujiita au kuitwa ana mafanikio ni lazima awe amekidhi idara muhimu saba. Kwa wewe unayesoma Makala hii kwa mara ya kwanza nakuomba upitie maelezo yafuatayo ili uweze jua fika ya kuwa mafanikio ni utimilifu wa idara 7 zifuatazo:-


1.      Imani katika Mungu - Agano binafsi la kushikamana na Mungu kupitia mwanae mpendwa Yesu Kristo ndio kiini cha mafanikio ya kweli na uhakika kinyume na hapo ni sawa na kujenga nyumba hewani, kamwe haitakuja kukamilika.
Hivyo mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote kupitia Yesu Kristo ndipo sasa utashangaa jinsi mambo yako yatakavyokuwa. Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na mengine yote utazidishiwa.

2.      Mahusiano ya kimkakati - Kuwa na fedha mithili ya mchanga bila kuwa na nyumbani ni upuuzi. Sasa ninaposema nyumbani ni zaidi ya matofali, mbao, mabati nk. Nyumbani maana yake ni sehemu inayokufurahisha, sehemu unayoweza kuishi, kufurahi, na kujifunza.  Ni mahali unapopendwa, unapoheshimika, na kujaliwa. Nyumbani ni mahali moyo wako hutulia. Mtu aweza kuwa na nyumba lakini akakosa nyumbani.

3.      Umiliki wa vitu - Mtu kuambiwa ana utajiri pasipo umiliki wa vitu mbalimbali bado kunakuwa na mapungufu. Hata imani yako na Mungu lazima ithibitishwe kwa matendo kwani imani bila matendo imekufa. Mungu anapenda uweze kumiliki vitu vizuri lakini kamwe hapendi vitu vizuri vikumiliki. Mungu anapenda uwe na gari zuri lakini hapendi gari likumiliki hadi unaanza kusahau kumwabudu ati tu sasa una gari zuri misafara isiyo na ratiba kibao hadi kanisani umeadimika, kwenye maombi huonekani wala mazoezi ya kwaya. Hapo sasa ni tatizo. Ni mpango wa Mungu wewe kumiliki vitu vizuri lakini vitu vizuri na kamwe visikumiliki. Hapa ndipo penye mtego. Mwenye kuelewa na aelewe.
4.      Fedha – Ni kweli kwamba ni vyema ukamiki vitu vizuri, lakini pia kuwa na fedha ni muhimu sana katika suala zima la utajiri. Waweza kuwa na vitu vyenye thamani sana lakini inapotokea ukakosa fedha, hapo sasa inakuwa janga.
5.      Udhoefu wa maisha – Je umewahi sikia ‘udhoefu ni mali’? Haijalishi umepitia magumu kiasi gani au mazuri kwa kiasi gani. Ukweli wa mambo ni kuwa kamwe udhoefu uliopata kamwe huwezi kuununua kwa fedha. Udhoefu wa leo ni hekima ya kesho.
6.      Maarifa na ujuzi – Sijui kama unajua ya kuwa wengi ya waliokwisha fanikiwa kazi yao kubwa ni kufanyia biashara maarifa na ujuzi wao.
7.      Afya – Ni mpumbavu tu ndiye anayeweza kata ukweli ya kuwa ‘AFYA NI UTAJIRI’. Ukiwa umepatwa na ugonjwa usiotibika ndipo utajua ukomo wa hela kwani haijalishi una fedha kiasi gani maadam fedha zako kamwe haziwezi kukuponya ndipo utatia akili ya kuwa afya ni mali. Umewahi jiuliza moyo wako una gharama kiasi gani au figo zako ni za thamani kiasi gani? Ikiwa una siha njema na ukajiita u masikini basi wewe ni jua wa kutupwa. Makala hizi zinazokujia kila siku zimelenga kukuelimisha utajiri si tu pesa na vitu ambavyo mtu anamiliki, la hasha bali utajiri kwa maana ya utajiri ni mambo yote saba niliyoyaelezea kwa ufaa na ndivyo nitakavyo upate uelewa mpana juu ya mafanikio.
Hivyo mimi nikiuliza kama niko kundi gani, jibu ni kwamba tayari niko kwenye mchakato kuufikia utajiri wenye tija maana tayari nina vitu viwili vitatu kati ya hivyo saba na hivyo mimi si masikini na niko mbioni kukamilisha vitu vyote saba.
Kumbuka jambo moja; hali uliyo nayo kwa sasa si hatima ya maisha yako, ukweli ni kwamba uko kwenye mchakato wa baadhi ya hayo mambo saba na wengi wetu tayari tunayo kwa sehemu hivyo wewe ni tajiri mtarajiwa, songa mbele.
Umasikini ni fikra na ni hali mbaya sana maana ndicho kinachowaangamiza wengi kufikia kutumia kila fedha waipatayo kisa wakidai ati wao ni masikini na fedha haitoshi. Dhana hii ikikushika kwenye ufahamu na ukaiamini basi umeharibu maisha yako mwenyewe.
Labda nikutajie mchawi wa maisha yako. Nakuomba nenda mbele ya kioo chako na tazama kwenye kioo na huyo unayemuona ndio tatizo kuu la wewe kutokuwa na mafanikio maana huyo jamaa amejawa na vilio kila wakati mara vyuma vimekaza, mara mimi masikini hela haiwekeki na visingizio vingi. Na kama matokeo huishi kutokana na ukiri wake. Kuwa mwangalifu sana kwa kile uongeacho kwani huumba.
Nataka nikuambie si mpango wa Mungu wewe kuwa masikini na vivyo hivyo si mpango wa Mungu wewe kuendeshwa na mali bali Mungu hufurahi ukimiliki mali na sio kumilikiwa kiasi cha kuondoka katika utaratibu wenye afya.
Mawazo ya umasikini yamewafanya wengi kudidimia.
Mfano unamuuliza mtu kati ya TZA 1,000,000 na kuwekeza TZA 200 inayojirudufu kila iitwapo leo yaani leo una 200, kesho 40,000, kesho kutwa una 160,0000,000… Mwenye mawazo ya umasikini atachagua TZA 1,000,000 na kuacha kuwekeza TZA 200 inayojirudufu ila mwenye mawazo ya uwekezaji atachagua TZA 200 na kuacha TZA 1,000,000 na hapo ndio tatizo linapoanzia mawazo yetu – tunawaze? Kitajiri au kiumasikini?
Endela kunifuatilia katika Makala zangu nitakuwa nikitiririka juu ya elimu ya fedha na lengo nikukufikisha mahala uweze kuzitawala na zisikutawale, na ujue jinsi ya kuzitunza na kuzifanya zijiongeze kila iitwapo leo.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325;  +255 714 051174;  +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...