KARAKANA YA UBONGO
SOMO NAMBA 5
SOMO NAMBA 5
Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 5
Habari za Leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli. Katika Makala yangu ya 03 niliomba kila msomaji ajaze kipima joto na kunirudishia lakini hadi leo ni mtu mmoja tu aliyenirudishia. Ninakutumia tena ujaze na kunirudishia. Angalia hapa chini
JARIBIO LA KUJUA UELEWA WAKO JUU YA MASUALA YA FEDHA (FINANCIAL INTELIGENCE TEST (F.I.T)
Tafadhali weka alama ya vema mahala sahihi
Mfano
√
Ndio

Hapana
Sifahamu
•MAELEZO • NDIO • HAPANA SIFAHAMU
1 Je wajua hali yako ya kifedha kwa sasa au je wajua utajiri wako una thamani gani
2 Je umeridhika na hali uliyonayo kifedha?
3 Je wajua namna rahisi ya kuongeza kipato chako?
4 Je unayo akiba toshelevu kwa angalau kuendesha maisha yako ya kila siku kwa miezi sita iwapo itatokea kuachishwa kazi au shughuli iliyokuwa ikikuingizia kipato kufilisika?
5 Je una utaratibu wa kuweka akiba kila upatapo pesa?
6 Je tabia ya kuweka akiba imeshakuwa sawia na tabia ya kusafisha kinywa asubuhi? Nina maana hauhitaji kukumbushwa mara upatapo pesa mara moja unaweka akiba. Je umefikia hatua hiyo?
7 Je una malengo mahususi kuhusiana na fedha umbao uko katika maandishi?
8 Je una account bank?
9 Je Kila mwisho wa mwezi unadai bank statement ili kuangalia kama fedha zako ziko salama?
10 Je unaweka kumbukumbu ya mapato na matumizi yako?
11 Je unajua kiasi gani cha pesa unatumia kila mwezi?
12 Je umefikia nidhamu ya kuhakikisha unatumia kidogo kuliko kipato chako?
13 Je una makadirio ya matumizi ya nyumbani kila mwezi?
14 Je huwa unakwepa manunuzi makubwa kwa njia ya mkopo?
15 Je huwa unazitumia akiba zako kwa fursa za uwekezaji zinazojitokeza?
16 Je una uwekezaji wa aina yoyote unaokusaidia kupunguza machungu ya maisha?
17 Je umewekeza sehemu tofauti tofauti kiasi kwamba sehemu moja isipozalisha unafajiwa na sehemu zingine za uwekezaji?
18 Je umeridhika na kipato mupatacho kutokana na uwekezaji wako kiasi kwamba huoni sababu ya kuendelea kuwekeza?
19 Je unahisi kujisikia vizuri kwa kuwa una mshauri mzuri au washauri wazuri juu ya fedha?
20 Je unadhani una bima toshelevu ya maisha?
21 Je una mpango unaoeleweka juu ya elimu ya wanao chuoni au chuo kikuu?
22 Je unamiliki nyumba?
23 Je una mpango wa kustaafu ukiwa na kila kitu pasi kusumbua watoto au ndugu?
24 Je umeandaa wosia wako iwapo ikatokea ghafla ukatoweka duniani?
25 Je una udhibiti mzuri juu ya fedha kwa siku zako za mbele?
26 Je umeridhika kwa mchango wako ulioufanya katika jamii?

Leo nataka tuangalie kwa umakini neno umasikini na tulielewe kwa undani.
1. Umasikini ni laana
Maelezo niyatoayo kuelezea maana ya umasikini yaweza onekana ni ya kiroho au ya kidini, lakini ukweli wa mambo ni kweli umasikini ni laana.
Wengi ni masikini leo na wataendelea kubaki kuwa masikini kwa sababu tu wanaishi wakiwa chini ya laana. Laana inakuwezesha uwe mtu wa kushindwa kwa chochote utendacho, hivyo unapokuwa ukitumikishwa na laana hii kila ufanyacho haijalishi unatumia maarifa na nguvu kiasi gani, kwako kutofanikisha inabaki kuwa sehemu ya maisha yako na kila uwekezaji hauendelei ni kama vile unachimba shimo na kufukia.
Utashangaa yaani unaona kabisa mafanikio sasa tayari yako nchani na ghafla kufumba na kufumbua ni kama kiini macho unakuta kila kitu kimeharibika na kujikuta umepata hasara kubwa. Yaani unafikia hatua unaona kabisa kwako kufanikiwa haitakuja kutokea kutokana na unayopitia maishani katika kujishughulisha kwako. Unachoshangaa ni mfululizo wa matukio ya kukukatisha tamaa, vikwazo kibao, kutofanikisha chochote ukianzishacho ni kana kwamba kuna mtu anahakikisha hupati chochote yaani ni kunyang'anywa tu.
Yote hayo ni tabia za mtu kuwa na laana ya umasikini, sema vyovyote kama mara kuishi chini ya laana au wewe na laana mnakua mapacha hamhachani. Mungu tusaidie kuwa na macho ya rohoni kwani kufanikiwa ni haki yetu ya urithi.
Ninamaanisha kuna mshikamano wa mtu na laana ya umasikini. Tatizo roho hii ya umasikini haiheshimu umri wa mtu, nafasi ya mtu, rangi ya mtu, ufaulu wa mtu, cheo au wapi anaishi.
2. Umasikini ni roho
Maisha ya mtu kuongozwa au kutawaliwa na roho ya umasikini. Utashangaa miaka nenda miaka rudi mtu anazidi kudorora kiuchumi, anazidi kuchakaa, anazidi kuwa hoe hae. Yote hii ni kwa kuwa roho ya umasikini imeweka kitako ndani yako yaani imeshikamana nawe kuhakikisha huchomoki.
Haijalishi ni Marekani au England roho hii ya umasikini ikikukamata na kufanya makao ni lazima utadhihirisha ya kuwa u masikini.

Ndugu yangu naomba mimi ninawe mikono kwa kukuambia ukweli - kabidhi maisha yako kws Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu maana yeye ni Bwana wa vita, anasema mwizi anakuja ili kuiba, kuchinja na kuangamiza bali mwana wa Adam (Yesu) alikuja ili tuwe na uzima tele.
Namaanisha uzima wenye utele (mafanikio). Kumbe chimbuko la mafanikio ya kweli lipo ndani ya Yesu Kristo mwenyewe maana alifanywa masikini ili sisi tuwe matajiri.
Nimalizie kwa kusema 'Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na mengine utazidishiwa
Kwa kusema hivi simaanishi ya kuwa hakuna mafanikio kwa mungu mwingine (Shetani). Mafanikio kwa shetani yapo tena ya kumwaga ila lazima utumikishwe kufanya mambo ya kishetani yatakayokufanya uishi bila amani maana kuna wakati utatakiwa kuua mama yako, au mtoto na mengine mengi ya kafara.
UCHAGUZI NI WAKO ILA MIMI NA NYUMBA YANGU MAISHA YETU TUMEYAKABIDHI KWA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU.
Endela kunifuatilia katika Makala zangu nitakuwa nikitiririka juu ya elimu ya fedha na lengo nikukufikisha mahala uweze kuzitawala na zisikutawale, na ujue jinsi ya kuzitunza na kuzifanya zijiongeze kila iitwapo leo.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni
Chapisha Maoni