Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 18)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 18

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI.
.
1. AKILI YA KUHAMAHAMA – Kama kuna kitu cha kushughulikia kuondokana nacho basi ni hii hali ya mtu kutotulia kubaki kutangatanga yaani kutokuwa na jambo au kitu maalum kukifanya bali ni kushika hiki na kukiacha kisha kukimbilia kingine. Watu wenye tabia hii ni vigumu hata kujua wanasali wapi maana hawaachi kuhama hama mara leo huku kesho kule  na inaathiri hata kutulia kituo kimoja cha kazi ni kila wakati kubadili sehemu ya kazi na hata ukifuatilia sababu za kuacha kazi hapa na kwenda pale utakuta hazina mashiko. Kifupi hii ni roho inayomwendesha mtu kumuongoza kutotulia au kuwa na maisha yasiyo mipaka, maisha yasio na mwelekeo au kusuduo.
Tabia za watu wa aina hii ni mbili kuu:-
i. Hawana mahali maalum – Ni watu wa kutangatanga kutoka eneo moja hadi linguine kila mara.
ii. Watu wa kutumia tu pasi kupanda – Hula kila kitu nkilicho mbele yao bila kupanda au kuzalisha.

Mwanzo 12:1- 4

1 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
4 Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.


Abraham baba wa Imani alikuwa nayo tabia ya njinsi hii ya kuhamahama, lakini Mungualimwita na kumpandisha daraja ili kubadili historia ya maisha yake. Kamwe huwezi kufanikiwa ukiwa mwenye akili za kutotulia (kuhamahama).

Abraham ilimpasa kuachana na akili za kutotulia ili aweze kumiliki nchi aliyoahidiwa na Mungu. Abraham ndiye mtu wa kwanza kwenye biblia kuweza kununua ardhi na kulipa pesa taslimu.

Pamoja na kwamba alikuwa na ahadi ya Kaanani, lakini bado alinunua ili kuwa na umiliki kamili.

Mwanzo 12:5-9
Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.
BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu BWANA aliyemtokea.

Mstari wa saba unatuonesha ahadi ya Mungu kumpa Abraham ardhi kama alivyoahidi kutupa sisi ‘utajiri wa watu wabaya’. Hata hivyo Mwanzao 23:1-20 inatupa mwanga zaidi
Mwanzo 23:17-18
[17]Basi shamba la Efroni lililokuwa katika Makpela kuelekea Mamre, shamba, na pango iliyokuwamo, na miti yote iliyokuwamo shambani, iliyokuwa katika mipaka yake pande zote, vyote viliyakinishwa
[18]kuwa mali yake Ibrahimu, mbele ya wazawa wa Hethi, mbele ya watu wote waingiao katika mlango wa mji wake.

Kama ilivyokuwa kwa Abraham – pamoja na kuahidiwa ardhi ilimpasa naye kutenda iliyo sehemu yake kwa kuamua kunua ardhi pasipo kubweteka ati nina ahadi ya Mungu kunipa ardhi.

Vivyo hivyo nawe pamoja na ahadi ya Mungu kukufanikisha, kumbuka una sehemu yako ya kufanya ili uweze kukabidhiwa mafanikio yako.

Hebu tuweke mbali akili ya kuhamahama ikiwa ni hatua muhimu ya kwanza.

2. Akili za Kutumia – Aina ya pili ya sumu juu ya uwekezaji ni kufikiria kutumia tu katika maisha. Kila upatapo wazo pekee linalokusumbua ni kuzitumia ulizozipata mpaka ziishe utafikiri una pepo la chuma ulete. Hili ni suala la pili kuhakikisha unaondokana nalo. Aina hii ya watu kamwe hawana wazo lolote juu ya kuweka akiba na kuwekeza.

MITHALI 21:20

[20]Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima;
Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.

Kutumia vyote upatavyo pasi kwanza kuwa na wazo la kuweka na kuwekeza ndio dalili ya kwanza kukuelezea ya kuwa wewe ni MJINGA na milango ya mafanikio kwako imejifunga. Tabia hii ya utapanyaji au kuzitumia pesa mpka zikutambue zimeishia kuwaacha watu katika aibu, umasikini, kuishiwa (ukata) na ugumu wa maisha.

Siri kubwa ya utajiri wa misri wakati wa njaa ulitokana na hekima ya Mungu kupitia Yusuf.

Yusuf ndiye aliyemshauri Farao juu ya uwekaji akiba na uwekezaji kwa kumtaadharisha juu ya tabia ya ulaji tu pasi kukumbuka kwanza kuweka akiba na uwekezaji. Ushauri wa Yusufu ulikuwa kwa kila kitakachozalishwa 20% ihifadhiwe kwa lengo la kuja kuwekeza. Hebu soma hapa chini

MWANZO41:33-36

 Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba.
 Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji.

Aibu yako ya siku zijazo itafunikwa iwapo tu utaanza leo kuachana kabisa na tabia ya kuanza kutumi kila upatacho. Kanuni ni kuwa upatacho kinacho takiwa kuja kichwani ni 10% peleka kanisani kama Dhaka na kama si muumini wasaidie wenye uhitaji au wape mashirika yanayowahudumia watu waishio kwenye mazingira magumu na 20% hakikisha unaweka akiba ili ikufikishie kiwango cha kuweza kuanzisha uzalishaji kwa upande mmoja na upande mwingine pasi kusahau kuwekeza.

Hivi umewahi jiuliza Mungu aliumba dunia yenye madaraja au aliumba dunia moja tu. Ukweli ni kwamba Mungu aliumba dunia moja tu na si vinginevyo. Sasa iweje leo wengine waitwe dunia ya kwanza na wengine ya tatu? Jibu ni rahaisi dunia ya tatu uchumi wake uko chini ya matumizi kitwakimu na ulimwengu wa kwanza uchumi wake uko juu na matumizi yako chini.

Nikuombe jambo moja anzisha ulimwengu wako wa kwanza kwa kuzingati upatapo tu pesa iwe ni zawadi au ujira au kuzalisha tenga 30% na kinachobaki banana nacho na usiweke mawazo katika pesa uliyoitenga na ni vyema uiweke sehemu ambayo sir ahi kuifikia. Kama hujanielewa vizuri nitafute tuelezane hapa pana siri kubwa ambayo huna budi kuijua.


Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...