Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 19)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 19

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea aina mbili za sumu juu ya uwekezaji. Leo tunaendelea na nikuombe endelea kunifuatilia:-
.
3. KUJIHALALISHIA/DHANA YA UMILIKI – Aina hii ya tatu inapaswa kushughulikiwa na kuondokana nayo kabisa. Kujihalalishia au kujiona wewe ndiye mmiliki wa jambo fulani baya imeathiri wengi. Akili ya kujidhania/kujisikia kila wakati ya kuwa wewe ndiye mwenye kustahili kuwa na hali mbaya, kuishi maisha magumu na kujidhania ya kuwa yuko mtu anayekusababishia kuwa na hali uliyonayo na kuomba atoweke duniani ndipo utapata unafuu. Ukweli ni kwamba hakuna mtu awazaye kukufanya ushindwe pasipo wewe mwenyewe kuruhusu, hivyo chochote unachoruhusu kwenye maisha yako ndicho unachopokea. Dalili ya watu wa aina hii ni wale wote wenye kila wakati ni watu wa kutoa udhuru na kupenda kulaumu watu wengine au kuilamu serikali au mbunge nk. Kama wewe una hizo tabia ndiyo muhusika halisi wa kundi hili. Mungu akusaidie umekaa mahali si salama.
‘Ni kwa sababu mimi ni mtu mweusi’
‘Ni kwa sababu mimi ni mwanamke’
‘Ni kwa sababu nimetokea kwenye familia hoe hae’
‘Ni kwa sababu mimi ni  yatima’
‘Ni kwa sababu ya shetani’
‘ Ni  kwa sababu ya adui zangu’
‘Ni kwa sababu sijasoma’
‘Ni kwa sababu viongozi wangu hawawajibiki’ nk
Jambo la kushangaza ni kwamba kwa kila utetezi unaoutoa, wako watu maelfu wa jinsi yako na pia kwa upande wa pili wa shilingi kuna mtu mmoja miongoni mwao hufanikiwa tena kwa kiwango kikubwa pamoja na hali zote hizo. Je hapo tusemeje?
Hali hii ya kujihalalishia kamwe haitoweza kukutoa ni mpaka ufanye uamuzi wa kutengana nayo na INAWEZEKANA. AMKA CHUKUA HATUA.
Yohana 5:1-14
[1]Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
[2]Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
[3]Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.
[4]Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]
[5]Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
[6]Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
[7]Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
[8]Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
[9]Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.
[10]Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.
[11]Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.
[12]Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani?
[13]Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale.
[14]Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.


Leo nataka tujifunze kitu kwa huyu mtu aliyekuwa mgonjwa kwa miaka 38 mfululizo:  ‘
[5]Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
[6]Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
[7]Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.

Swali linasema unataka kuwa mzima? Hebu angalia jibu la mgonjwa kwa swali la Bwana Yesu - Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.

Je swali na jibu vina uhusiano? Kinachoonekana kwa huyu mgonjwa ni kwamba alikwisha jihalalishia ya kuwa kupona kwake asahau kwa hiyo akawa mmiliki wa ugonjwa wake na kwamba haiwezekani yeye kupona. Unaiona hatari ya kujimilikisha inavyotesa watu. Kwa Jina la Yesu naomba usiwe mmojawapo. Funguliwa na hiyo roho.

Ndipo Yesu kwa huruma akaamua kumfungua vinginevyo angebaki vivyo hivyo - Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.
Nataka ujue ya kuwa kwa YESU hakuna la kushindikana. Mkimbilie Yesu Kristo upate uhuru kwa kila idara.




Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
             
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...