Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 20)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 20

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea aina mbili za sumu juu ya uwekezaji. Leo tunaendelea na nikuombe endelea kunifuatilia:-
.
3. KUJIHALALISHIA/DHANA YA UMILIKI – Katika kuongelea aina hii ya tatu, Makala iliyopita nilimalizia kwa kusema:-
‘Swali linasema unataka kuwa mzima? Hebu angalia jibu la mgonjwa kwa swali la Bwana Yesu - Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.

Je swali na jibu vina uhusiano? Kinachoonekana kwa huyu mgonjwa ni kwamba alikwisha jihalalishia ya kuwa kupona kwake asahau kwa hiyo akawa mmiliki wa ugonjwa wake na kwamba haiwezekani yeye kupona. Unaiona hatari ya kujimilikisha inavyotesa watu. Kwa Jina la Yesu naomba usiwe mmojawapo. Funguliwa na hiyo roho.

Ndipo Yesu kwa huruma akaamua kumfungua vinginevyo angebaki vivyo hivyo - Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.
Nataka ujue ya kuwa kwa YESU hakuna la kushindikana. Mkimbilie Yesu Kristo upate uhuru kwa kila idara.’

Leo nataka utambue ya kuwa, huyu mtu aliendelea kuteseka na ugonjwa kwa miaka 38 si kwamba shetani alionekana ni mwenye nguvu sana kumshinda Yesu na pia si kwamba Yesu kwa kipindi chote hicho ambacho amekuwa akiugua uweza wake  ulipungua, la hasha, ila kukubali kwake kwamba ugonjwa huo kupona ni vigumu ndiko kulimfanya abaki kifungoni akiteseka. Tukiangalia kwa makini juu ya huyu mtu kwa tabia yake ya kujionea ni vigumu kuondokana na ugonjwa aliokuwa nao, tunajifunza mambo yafuatayo:-

1. Swali ninalojiuliza ina maana miaka 38 haikutosha kumfanya kushoshwa na mateso aliyokuwa akiyapitia kiasi cha kushidwa kutambua majira ya malaika walipokuwa wakija kutibua maji?


2. Kama ndugu msomaji unadhani huo ulikuwa muda mwingi sana wa mtu kuteseka, kwa nini hakuamuua kubaki ndani ya maji na siku malaika wakija kutibua wamkute ndani ya maji tayarI? Mungu angalimuona juu ya kuwa kushoshwa kwake na hali hiyo na angalibadilisha historia kabisa. Yesu alimuuliza swali rahisi sana ‘UNATAKA KUWA MZIMA’ na chakushangaza aliendelea kuthibitisha hali yake yakukata tamaa ya kuwa kupona kwake ni vigumu akiwa na ushahidi wa sababu.


3. Ukitaka kuthibitisha hoja yangu, ni pale alipojibu ‘Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu’. Huyu mgonjwa alijua fika uponywaji wake ungalipatikana katika yale maji, lakini cha kushangaza kila wakati wenzake walimuwai kuingia. Hii inamaanisha wenzake walijikalisha karibu na maji na yeye alikaa mbali na maji. Hivi ni kwa nini ukae mbali na sehemu unayojua ndipo penye baraka zako?


4. Alisema ‘ Nilipokuwa nakwenda’ Kwa hiyo inamaana aliweza kutembea mwenyewe, sasa kwa nini alisema ‘Sina mtu wa kunisaidia’. Sasa waweza ona jinsi alivyokubali ya kuwa ugonjwa ni wake na haiwezekani kupona. Kwa nini umlaumu mtu mwingine wakati wewe mwenyewe umeruhusu na kwa nini utegemee watu wengine wafanye kwa niaba yako  jambo ambalo waweza lifanya wenyewe. Aibu!


5. Kama kweli alikuwa ameshoshwa na ile hali, kwa nini alitegemea maji tu kama njia pekee ya kufunguliwa wakati kuna  fursa nyingi tu za kiMungu mfano wa mikutano mbalimbali aliyoifanya Yesu Kristo kwa nini hakukimbilia huko kutafuta msaada kama alivyofanya akida mmoja.

Tusome LUKA 7:1-10

Luka 7:1 Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.
Luka 7:2 Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.
Luka 7:3 Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake.
Luka 7:4 Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili;
Luka 7:5 maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi.
Luka 7:6 Basi Yesu akaenda pamoja nao. Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule akida alituma rafiki kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu;
Luka 7:7 kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.
Luka 7:8 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
Luka 7:9 Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii.
Luka 7:10 Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima.

Mifano iko mingi jinsi watu walivyohangaika kupata suluhisho la changamoto zao. Naomba kwa wakati wako kasome Marko 5:21-43, Matayo 15:21-28, Marko 10:46-52

Ningaliweza kuendelea na kuendelea, lakini naamini nimethibitisha kile ninachosimamia ya kuwa huyu mtu alijikatia tamaa kiasi cha kuona ugonjwa alikuwa nao kupona haiwezekani.

Naomba niongee na wewe unayesoma hii Makala, tafadhali tambua hakuna kitu cha kukutesa wewe kikawa cha kudumu ni mpaka wewe mwenyewe uruhusu. Kataa Yesu anaweza na HAKUNA JAMBO GUMU LA KUMSHINDA.

Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...