Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 21
Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea na kumalizia aina ya tatu ya sumu juu ya uwekezaji. Leo naanza kuongelea aina ya nne na nikuombe endelea kunifuatilia:-
.
4. Utumishi wa Umma/Dhana ya mshahara
Aina ya nne ya sumu ya uwekezaji ni dhana ya utumishi wa uma/mshahara. Wengi wamejikuta katika dimbwi la umasikini kwa sababu maisha yao yote wamekuwa wakiishi kwa kumtegemea boss, mwajiri, au serikali ili kupewa mshahara kwa lengo la kutajirika siku za usoni. Amka acha kulala!
• Boss wako si asili ya mafanikio yako bali ni chanzo cha kuhakikisha unatumika kumfanikishia.
• Ajira yako vivyo hivyo kamwe haiwezi kukufanikisha labda kama utakuwa kwenye ngazi maalum (executives) bali ajira yako inakuimarisha kuwa mtumwa mstaarabu. Wewe ni kutumika na kupewa mshahara mkononi kwenda kinywani basi.
Ikumbukwe ya kuwa si jukumu la mwajiri wako kuhakikisha una pata mafanikio katika maisha yako. Wengine wakiona mabadiriko chanya wanahisi umeanza kuwaibia na ni hatari kuachishwa kazi. Jukumu la kufanikiwa linabaki kuwa lako maana hata serikali haina huo wajibu kwako.
Kumbuka si upatacho kisababishacho mafanikio bali ufanyacho mara baada ya kupata ndio msingi wa mafanikio. Kwa hiyo haijalishi unalipwa kiasi gani kama mshahara ila utakapo fanya jambo sahihi kwa upatacho mabadiliko chanya ni lazima.
Ni lazima ujifunze kuachana na dhana ya mshahara na uanze kuchukulia ni kipato naamaanisha futa neno mshahara bali upatapo ita kipato. Utakapo weza kuuaminisha ufahamu wako ya kuwa upatacho ni kipato na si mshahara utafauti unaanza.
Kama unasubiri kufanikiwa kwa kupata mshahara utasubiri sana. Utafiti unaonesha ya kuwa ni asilimia 2 tu kati ya mamilionea wote ulimwenguni wametokana na mshahara.
Kumbuka:
Mshahara
- Kila mara ni huo huo hakuna mabadiliko
- Kiwango cha wewe kulipwa kinaamuliwa na mtu mwingine/watu wengine. Wewe huna nafsi ya kupanga
- Hauongezeki ni mpaka mtu fulani aamue
- Utalipwa tu iwapo utakuwa umetolea jasho yaaani umefanyia kazi na si vinginevyo. Hakuna kazi hakuna malipo
- Kamwe mshahara wako hauelezei unachostahili yaani hauelezei ya kuwa upatacho ni sawa na thamani yako na uzalishacho. Ni pungufu ya uwezo wako.
- Mshahara hukoma unakapokoma kufanya kazi.
- Mshahara waweza cheleweshewa,
- Kuzuiwa, kuadhibiwa, kukatwa na kusimamishwa na mtu mwingine bila ridhaa yako. Orodha inaendelea wakati kipato ni tofauti na mshahara.
Kipato:-
- Hubadilika tegemeana na muda
- Hakuna wa kukuamulia
- Huongezeka bila kusitishwa na mtu.
- Huja iwapo unafanya kazi au hufanyi bali mfumo unajiendesha wenyewe. Ili kupata mshahara yakupasa uufanyie kazi lakini kipato, fedha hukufanyia kazi.
- Hukuelezea thamani yako na uwezo wako pia.
- Hakuna ujanja janja na kukandamizwa na mwingine.
Tujifunze kutoka kielelezo kifuatacho Mwanzo 27:1-10
Mwanzo 27:1 Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
Mwanzo 27:2 Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.
Mwanzo 27:3 Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
Mwanzo 27:4 ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.
Mwanzo 27:5 Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete.
Mwanzo 27:6 Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia, nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako, akinena,
Mwanzo 27:7 Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili nile, na kukubariki mbele za Bwana kabla ya kufa kwangu.
Mwanzo 27:8 Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama nitakavyokuagiza.
Mwanzo 27:9 Enenda sasa kundini ukanitwalie wana-mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo.
Mwanzo 27:10 Kisha utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya kufa kwake.
Esau anafanana na mfanyakazi yaani yambidi awinde ndio apate kula. Ni mfano sahihi wa mtu anayejituma kwa kutumia msuli, ambapo kwa kawaida uzalishaji wa njia hiyo huwa ni hafifu. Lakini kwa upande mwingine Yakobo ni kama mwekezaji mwenye kupata kipato chake kutoka kwenye biashara. Mfumo ndio unaomfanyia kazi kumfanikishia kupata kipato. Soma mistari inayofuata upate kuona faida ya kuwa smart badala ya kutumia maguvu, kutumia akili badala ya kutumia nguvu, pia ulinganifu wa kipato badala ya mshahara.
Esau alikwenda kuwinda na kuhangaikia ili kufanikisha, lakini Yakobo alizunguka na kuingia zizini nakuwaleta mbuzi ili kuandaliwa baba yake. Hakuna jasho hapo na pia alitumia muda mchache kutimiza jambo kubwa. Tumia akili sana nguvu kidogo yatosha kufanikisha mambo. Kutumia msuli kumepitwa na wakati. Jifunze kufikiri.
Hebu tuangalie tena jinsi dhana ya mshahara na kipato, maguvu na akili vinavyosababisha utofauti.
Tusome Mwanzo 30:25-43
Mwanzo 30:25 Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu.
Mwanzo 30:26 Nipe wake zangu na watoto wangu, niliokutumikia, niende zangu, maana umejua utumishi wangu niliokutumikia.
Mwanzo 30:27 Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba Bwana amenibariki kwa ajili yako.
Mwanzo 30:28 Akasema, Sema mshahara wako utakao, nami nitatoa.
Mwanzo 30:29 Akamwambia, Umejua jinsi nilivyokutumikia, na jinsi wanyama wako walivyokuwa kwangu.
Mwanzo 30:30 Maana mali yako ilikuwa haba kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, Bwana akakubariki kila nilikokwenda. Basi sasa, nitaangalia lini mambo ya nyumba yangu mwenyewe?
Mwanzo 30:31 Akamwuliza, Nikupe nini? Yakobo akasema, Usinipe kitu; ukinifanyia neno hili, nitalisha wanyama wako tena na kuwalinda.
Mwanzo 30:32 Nitapita katika wanyama wako wote leo, na kutoa huko kila mnyama aliye na madoadoa na marakaraka, na kila mnyama mweusi katika hao kondoo, na aliye na marakaraka na madoadoa katika mbuzi; nao watakuwa mshahara wangu.
Mwanzo 30:33 Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa.
Mwanzo 30:34 Labani akasema, Tazama, na iwe hivi kama usemavyo.
Mwanzo 30:35 Basi akatoa siku ile mbuzi waume walio na milia na madoadoa, na mbuzi wake walio na madoadoa na marakaraka, kila aliye na doa jeupe, na kondoo wote waliokuwa weusi, akawatia mikononi mwa wanawe.
Mwanzo 30:36 Akajitenga na Yakobo mwendo wa siku tatu; naye Yakobo akachunga wanyama wa Labani waliosalia.
Mwanzo 30:37 Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito.
Mwanzo 30:38 Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wanywe; wakachukua mimba walipokuja kunywa.
Mwanzo 30:39 Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka.
Mwanzo 30:40 Na Yakobo akawatenga wana-kondoo, akazielekeza nyuso za makundi zielekee wale waliokuwa na milia, na kila aliyekuwa mweusi katika wanyama wa Labani. Akaweka kando wanyama wake mwenyewe, wala hakuwachanganya pamoja na wanyama wa Labani.
Mwanzo 30:41 Ikawa kila walipopata mimba wanyama wenye nguvu, Yakobo akaziweka zile fito mbele ya macho ya hao wanyama katika mabirika ili kwamba wachukue mimba kati ya zile fito,
Mwanzo 30:42 lakini wanyama walipodhoofika hakuziweka zile fito. Basi wale dhaifu walikuwa wa Labani, na wenye nguvu walikuwa wa Yakobo.
Mwanzo 30:43 Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.
Nakusihi hebu soma kuanzia sura ya 29 hadi 31 kumuhusu Labani na Yakobo upate kujua namna athari za kutegemea mshahara kama njia pekee ya kukutoa badala ya kuwa na dhana ya uwekezaji. Utajifunza mengi kwa msaada wa maisha yako.
Nimalizie kwa kusema kukubali kutumikishwa kwa ajili ya mshahara na ukaidumaza akili yako hapo utaishia pabaya; hebu badilisha fikra acha kabisa kufikiria neno mshahara hata kama umeajiriwa anza kuwaza juu ya kipato na kuweka mikakati ya kuzalisha zaidi na zaidi. Mshahara utakufanya uendelee kusubiri tarehe kwa tarehe lakini kipato utakiongeza siku kwa siku kwa ubunifu wa nini cha kufanya. Mungu atusaidie.
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni
Chapisha Maoni