Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 22
Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea na kumalizia aina ya nne ya sumu juu ya uwekezaji. Leo naanza kuongelea aina ya tano na nikuombe endelea kunifuatilia:-
.
5. Utajiri/Dhana ya mali/vitu kuwa ndio utajiri
Kama unadhani ukijilimbikizia mali ndio utajiri naomba nikupe pole kwani hiyo pekee ni ubinafsi na utakutesa sana.
Ninapoongelea mafanikio namaanisha kuacha alama, kugusa maisha ya watu wengine. Huwezi kujiita umefanikiwa kama huna mawazo ya kugusa jamii kwa mahitaji mbalimbali.
Huu ndio utajiri wa kweli kufanyika baraka kwa watu wengine.
Siri kubwa ya kufanikiwa ni kuelewa kwa kina dhana ya uwekezaji – Hapa msisitizo ni kwamba unawaza chochote upatacho utawezaje kukizidisha na wala si kupanga matumizi. Napenda hapa twende pamoja. Mfano umepata 100,000 ni wazo gani linakujia ghafla. Kwa mtu asiye na dhana ya uwekezaji kitakachomjia ghafla ni namna atakavyoanza kuitumia hadi ikaisha wakati mwenye dhana ya uwekezaji atachukua 30% ya hela iliyoingia mkononi mwake na kufanya yafuatayo:-
10% Atamtolea Mungu Dhaka/ kama si muumini kiwango hiki atasaidia wenye uhitaji
10% ataongezea biashara aliyonayo kama inahitaji maboresho na kama hana biashara basi ataitunza (save) kiwango hiki hadi pale kitakapotimia kuanzisha biashara ataitoa alipoitunza na kuanzisha biashara. Nina maanisha nini hapa? Mwekezaji kila wakati ana mradi unaohitaji fedha ili kuanza, hivyo utunzaji wa fedha ni ili kufikia kiwango cha mtaji wa biashara iliyo kwenye maandishi ikingojea utekelezaji. Kama hujanielewa nitafute kwa ufafanuzi. Kipengele hiki ni muhimu ukielewe kama unataka kuwa muwekezaji. Dhana nzima hapa ni fedha uliyoipata isikukimbie bali izidi kujiongeza.
10% utawapa wengine wakuzalishie nawe uwe unapokea faida tu hata ukiwa likizo Marekani pesa yako iko palepale.Kwa kuanzia nakushauri anza na uwekezaji wa pamoja UTT (UNIT TRUST OF TANZANIA). Tembelea tawi lolote la CRDB utaelekezwa namna ya kuanza uwekezaji wa pamoja au nitafute tuelezane.
Dhana ya uwekezaji ikishakukamata utakuwa mwangalifu na kila pesa uipatayo na kikubwa utajitahidi kutumia kwa kuzalishia kuliko kutumia kwa kupoteza nikimaanisha matumizi yasiyo tija ukitumia unatafuta tena ili kutumia badala ya kuanza kupokea faida kwa kuwa na vyanzo mbalimbali ulivyoanzisha.
Lengo kubwa la dhana ya uwekezaji ni ili ufikie kiwango ambapo pesa itakufanyia kazi na si wewe kuifanyia kazi pesa. Hapa ni kwamba utafikia hatua ya uwekezaji mfano majengo ya kupangisha, kununua hisa kwenye makampuni, kununua hati fungani, kununua vipande kwenye mfuko wa pamoja n.k. Ukifikia hatua hii kujishughulisha au kuhangaika kuitafuta pesa kunafikia ukomo. Hapa sasa ndipo utaanza kugusa maisha ya watu kwa njia mbalimbali maana hukaukiwi pesa kwani utakuwa ukipokea kutoka huko na huko ulikowekeza na utaendelea kuwekeza na kuwekeza mpaka wajukuu, vitukuu na vilembwezi watakutana na utajiri utakao kuwa umeuaha.
Ninachosisitiza hapa ni kwamba hata kama uko katika hali ya kuifanyia kazi pesa kama wengine tufanyavyo lakini lengo ni kufikia siku moja pesa ifanye kazi kwa ajili yetu na si kinyume chake.
Utawezaje kuwa mwekezaji?
1. Ondokana na sumu zote tano nilizokuelezea.
2. Anza kujielimisha juu ya uwekezaji kwa kununua vitabu, magazeti, kuhudhuria mafunzo n.k
3. Fanya maamuzi ya kubadilika kutoka kwenye matumizi na kuanza kuwaza namna ya kubaki na kuizidisha pesa kwa kuishi kwa kanuni ya pesa.
Utajuaje ya kuwa sasa dhana ya uwejezaji tayari imekamatana nawe?
1. Namna ulivyokuwa ukifanya mara baada ya kupata fedha itabadilika maana sasa kila ukipata utaanza kwa kuigawa 30% lazima iende kunakohitajika ndio mengine yafuate.
2. Utaanza kujiunga na UTT maana hata kama una TZA 10,000 unakaribishwa. Usichelewe anza sasa.
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.
Maoni
Chapisha Maoni