Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA/SHEKELI (SEHEMU YA 16)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 16

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya PESA HAITAFUTWI BALI INATENGENEZEWA NJIA.

Maisha ya utafutaji/usakaji pesa umewaacha wengi katika maumivu na wengine kupoteza maisha.

Dhana ya fedha ni vyema kuijua kwa undani. Fedha kwa lugha nyepesi ni mtumishi. Najua ninaposema mtumishi tayari umeanza kupata picha ya nini hufanywa na mtumishi.

Kwa kawaida mtumishi ni mtu wa kutumwa huko na huku ili kusaidia kufanya mambo yaende inavyotakiwa. Na mtumaji hawezi kumtuma mtu mahali ambapo hakuna uhitaji wa mtu kutumwa.

Hivyo kwangu pesa inatambulika kwa jina la mtumishi. Jirani yangu akiwa mgonjwa na hana namna ya kufika hospitali sijiulizi mara mbili kama mtumishi yupo naitisha uber na mtumishi mara moja anachukua nafasi yake na kuhakikisha mgonjwa amefika hospitali na kumfikisha kwa daktari na hatimaye kupewa dawa na kumrudisha nyumbani. Yote hayo yanawezeshwa na mtumishi pesa.

Uhitaji wa mtumishi fedha ni mkubwa mno na kama huna ndipo maisha hukosa ladha. Ladha ya maisha kwa mwanadamu ni vyema awe na fedha, ukata ni kutishia/kukosa matumaini ya maisha.

Kimsingi fedha hupatikana kupitia njia kuu mbili.

1. Fedha ipatikanayo kwa kutoa jasho (Active Income) – Hapa unahitajika wewe binafsi ujishughulishe ili uweze kuzipata fedha iwe kwa kujiajiri au kuajiriwa. Hapa ni pamoja na waajiriwa na wanao fanya biashara binafsi (kununua na kuuza, ushauri wa kitaalamu, nk). Fedha ya aina hii ina ukomo na ni vyema ukawa na mpango wa kuachana nayo kama si kupunguza kasi ya namna ya kuzipata.

Shida ya aina hii ya upatikanaji wa fedha inakutegemea wewe, na itokeapo umeumwa kwa mwajiria mwisho miezi sita unastafishwa kwa sababu ya ugonjwa ikiwa na maana ya kuwa kamwe utapewa mshahara tena. Hali kama hii usababisha maisha kubadilika nyumbani.

Wewe utakuwa shahidi hata wafanyabiashara wazuri wakifa tu basi na shughuli zao hufa.

Nahitaji upate ufahamu kisawasawa juu ya upatikanaji huu wa fedha. Kwa kweli ni vyema kuanza nao lakini kuishia nao ni hatari kwa mstakabari wa maisha yako. Uwepo wa mtu mtafutaji ndio msingi wa kipato cha aina hii na kutokuwepo kwa muhusika ndio ukomo wa aina hii ya kipato.


2. Fedha mtiririko (Passive Income) – Fedha ipatikanayo kwa njia hii ndio lengo la somo la leo. Fedha za aina hii hazihitaji mtu awepo. Uwepo au usiwepo pesa zazidi kukufuata. Na hapa ndipo nisemapo acha kuzitafuta pesa bali zitengenezee njia nazo zitaanza kukufuata. Uwe unacheza golf au bao au mazoezini au unasafiri nchi mbalimbali pasipo kujishughulisha fedha zaendelea kutiririka. Hizi ndizo fedha natamani kila mmoja wetu awe na mpango nazo maana hazina ukomo.

Fedha za aina hii wengine hufananisha na upatikanaji wa fedha kwa kutumia jasho la wengine yaani pasipo wewe kujishughulisha na fedha kuendelea kuzipata.

Mfano wa shughuli za aina hii ni kama vile kumiliki vitega uchumi mfano majengo na kuwa na wapangaji ambao kila mwezi wanakulipa pango. Hapa wewe ulijitengenezea mfereji wa fedha nazo zinafuata mkondo na kukufikia. Uwe mapuzikoni au safari lazima pango lilipwe.

Mfano mwingine ni umiliki wa hisa kwenye soko la hisa au mfuko wa pamoja ambapo unanunua hisa zako na kila mwisho wa mwaka unagawiwa faida.

Hapa tunaona hakuna tena kujishughulisha bali ni kupokea fedha kwa kwenda mbele.

Hakika raha ya fedha ni kuitengenezea njia.           

Acha kwa leo niishie hapa. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...