Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA/SHEKELI (SEHEMU YA 17)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 17

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya UKOSEFU WA UFAHAMU JUU YA UWEKEZAJI.
Ninaandika hii Makala nikiwa na shukrani nyingi kwa mwenyezi Mungu kwani kwa miaka 59 (Leo niandikapo Makala ni tarehe 02.03.2020)  iliyopita hii siri sikuijua kabisa na nimekuja kuijua nikiwa nimebakiza miezi michache nifikie miaka 60.

Ninashukuru kwa sababu nayaona maisha yangu yakiwa na pande mbili, moja ni onyo juu ya yapi  usiyafanye au kuyafuata maana mimi nimeshuhudia madhara hasi ambayo nimeyaishi kwa kuyafanya hayo ambayo leo nasimama kwa ujasiri nikiwaonya wote wanaosoma hii makala wasiyafanye/wasiyafuate.

Lakini upande wa pili wa maisha yangu nimebeba mambo mazuri ya wewe kuyafuata  au kuyafanya maana nimeona namna yalivyofanyika baraka si tu kwangu bali kwa familia nzima. Haya nitazidi kusisitiza kuyafuata.

Hivyo kwa ujumla wake pande hizi mbili leo zinanipa mamlaka ya kuandika na kuandika ili kila asomaye afaidike.

Sasa linapokuja suala la ufahamu juu ya uwekezaji – sina budi kulielezea kwa kukazia maarifa maana mimi nimekuwa nikiishi na pia nimesoma vidato vyote pamoja na chuo lakini hakuna mtu aliyethubutu kunifundisha nikafundishika na kuchukua hatua achali mbali maisha yangu ya kazi kama mwalimu wa fizikia na hisabati pamoja na kuwa meneja wa uhasibu na mwishowe mkaguzi mwandamizi bado suala la ufahamu juu ya uwekezaji lilikuwa mithili ya umbali ulivyo kati ya Tanzania na Marekani. 

Kutokujua au kutokuwa na ufahamu juu ya uwekezaji si suala la kufurahia hata kidogo kwani limechelewesha wengi kufikia mafanikiona kubaki kwenye dimbwi la umasikini.

Shida ninayoipata ni pale makanisani elimu hii pia imekuwa adimu. Kutofundishwa kwa elimu hii si kwamba wachungaji na wasaidizi hawapendi kufundisha bali tatizo walio wengi kama si wote hawajui. Hivyo  hili linafanya hali kuwa mbaya zaidi na wale wanaofahamu wamejikuta wakijitenga kwa kutofundisha. Mungu atusaidie.

 ‘Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.’ Mhubiri 10:15

Watu wengi hawajui jinsi ya kuipata elimu hii ya uwekezaji ambayo ni ya muhimu kwa mstakabali wa maisha yetu.

Hakuna atakaye kupangia kesho yako iwapo hutaipangilia mwenyewe.

Ukosefu wa ufahamu juu ya uwekezaji umewaacha wengi katika dimbwi la umasikini, kuishiwa (ukata), na ugumu wa maisha.

Mtu yeyote atakaye mafanikio analazimika kufanya juhudi ya makusudi kuhakikisha ufamu wake unaelewa na kuchukua hatua kuhakikisha mambo yanatokea na si hadithi tena.

Wengi wetu tumekuwa vizuizi kwa walio wengi kwa kuwakatisha tamaa juu ya uwekezaji na kama matokeo wengi wameishia kuwa na mawazo hasi juu ya uwekezaji na kujikuta wanaendelea katika umasikini. Njia pekee ni kuhakikisha tunaondokana kabisa na mawazo hasi (mgando).

Tutaendelea kujifunza aina 5 za ufahamu uliotiwa sumu juu ya uwekezaji.

Acha kwa leo niishie hapa. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...