Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 23
Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya ufikiri sahihi linapokuja suala la kuitawala fedha/shekel na udhibiti juu ya matumizi na nikuombe endelea kunifuatilia:-
.
Ufikiri sahihi juu ya fedha:-
Ninapoongelea juu ya ufikiri sahihi juu ya fedha ninamaanisha ile hali itakayokupelekea kupata badiliko zuri kimaisha ikiwa ni pamoja na kuidhibiti pesa uipatayo isikupokonyoke na izidi kujiongeza. Hapa natamani upate kunielewa vizuri maana ni ukombozi si kwako tu bali familia na jamii inayokuzunguka.
Nitakuwa sikutendei haki nisipokueleza ukweli ya kuwa msingi wa kufanijiwa/kutajirika katika maisha haya tuliyo nayo ni katika KUMJUA YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA. KINACHOTAKIWA NI KUYAKABIDHI MAISHA YAKO KWA YESU KRISTO AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO. HILI NI LA MUHIMU NA LA KWANZA NA USIPOLIZINGATIA, MAFUNDISHO YANGU YOTE YATAPOTEZA UMAANA.
Sisemi huwezi kufanikiwa nje ya Yesu Kristo lakini mafanikio nje ya Yesu Kristo ni sawa na kujenga nyumba hewani maana kila ukiweka tofali linadondoka na kamwe nyumba haijengeki.
Sitaki uwe na mafanikio ukiwa huna furaha, sitaki uwe umefanikiwa ukitoa ndugu zako kafara, sitaki uwe na mafanikio kwa kumiliki majini, sitaki ufanikiwe ukiishi bila amani, sitaki uwe na mafanikio ukitegemea pete ya bahati. SITAKI SITAKI SITAKI SITAKI SITAKI SITAKI SITAKI, NAAMINI UMENIELEWA. YESU KRISTO NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA MTU HATAMWONA BABA BILA YESU KRISTO NA KITU USICHOJUA NI KWAMBA MALI NA FEDHA NI MALI YAKE. YAANI YEYE NDIYE MMILIKI NA ITAKUWAJE UPENDE KUMILIKI FEDHA NA KILA AINA YA MALI UZIJUAZO WEWE PASIPO KUWA NA MAHUSIANO MAZURI NA MWENYE NAZO?
Sasa jifunze kuwa na muda wa utulivu ukiwa peke yako na kujifunza kuishi kwa kufikiri sana kuliko kujituma sana. Hili litakusaidia sana kuibua ubunifu katika shughuli zako na kufanya suala la kusaka shekeli kuwa jambo la furaha.
Jambo la pili ni vyema ukatambua ni kitu gani ukikifanya unajisikia vizuri na kupenda (passion). Unatakiwa kudumu kulifanya hilo jambo maana ndipo mafanikio yako yalipo.
Kuanzia sasa kila pesa uipatayo iwe ni ujira au gawio kwenye uwekezaji wako, faida kwenye biashara zako au zawadi fanya yafuatayo kabla ya kuanza matumizi ya aina yoyote:-
1. Mtolee Mungu fungu la kumi kama kiwango cha chini na waweza kukipandisha kadiri Mungu akufanikishavyo.
2. Tenga fedha kwa ajili ya ujasiriamali na uwekezaji
3. Kilichobaki ndio staili yako kwa matumizi mbalimbali ila nakuomba unapotaka kutumia fedha tumia kwa mwongozo ufuatao:-
• Hivi ni kweli ninakiitaji nitachotaka kukinunua?
• Je bei ni sahihi?
• Je huu ni muda muafaka kufanya haya manunuzi?
• Hivi ni lazima ninue hakuna mbadala?
• Hivi kama nikiacha kuna hasara yoyote kubwa nitaipata?
• Hivi nimefanya uchunguzi wa nitakacho kununua?
• Hivi kuna uwezekano wa kitu hiki kupanda bei siku za usoni?
• Je hivi nikinunua utunzaji wake utakuwa wa gharama?
• Je nimefanya ulinganifu wa bei na sehemu zingine wanaouza kitu hicho hicho (Window Shopping)?
• Hivi mwenza wangu anakubaliana na maamuzi yangu ya kununua?
• Je ni kweli kitu hiki kitaendelea kuitajika wiki ijayo, mwezi ujayo au mwaka ujayo au ni bora kuachana nacho?
• Hivi nikinunua ndio itamaanisha ubora wa maisha yangu utaongezeka?
• Je kwa hali yangu ya fedha manunuzi haya yako ndani ya uwezo au nataka kujionesha na wengine wanione ya kuwa na mimi naweza au nimo?
• Je nikinunua hakiathiri ushuhuda wangu kama mkristo?
• Je malengo yangu ya kuzidi kumfahamu Mungu na malengo yangu ya kimaisha yatafikiwa kwa kufanya maamuzi ya ununuzi huu nitakao kuufanya?
Haya na mengine mengi ni vyema kujiuliza kabla hujafanya maamuzi ya kutumia fedha. Kikubwa jifunze kuwa wewe na achana na tabia ya kuiga au kutaka kuonekana nawe umo. Bora uonekane uko nje ya wakati lakini mwenyewe wajua ufanyacho. Mungu atusaidie.
Ninapomalizia ningependa ujue ya kuwa hakuna wakati mzuri wa kuokoa pesa na kuitunza kama wakati wa kufanya manunuzi. Chukulia baada ya elimu hii umebadili ghafla maamuzi yako ya kununua simu ya 2,000,000 na kununua ya 200,000 unaona jinsi ambavyo utakuwa umeokoa 1,800,000 ambazo zingepotea kwa kukosa elimu hii na sasa kiasi hicho unakiwekeza na kukuzalishia. Mwenye kuelewa na aelewe.
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.
Gambling in Oregon - DrmCD
JibuFutaThere's nothing like gambling at the casino. If you are the 계룡 출장안마 first, most likely your nearest casino, you will likely 군포 출장샵 be near 김해 출장샵 the 충청북도 출장마사지 end of 오산 출장마사지 your journey.