Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 24)


Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 24

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo.

Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Ukiyajua itakurahisishia ujiweke wapi ili uwe kivipi. Napenda kuita vitu vinavyokutengeneza au kukupa sura au mtazamo tunaouona tukuangaliapo na kuweza kukuelezea tukikutofautisha na wengine. Mambo yanayomtengeneza mtu na haya yafuatayo:

MALEZI/HISTORIA YA FAMILIA ULIYOKULIA – Wengi wetu tumejikuta matatani kifedha kutokana na mambo tuliyo yachukua kwenye familia na mazingira tuliyokulia  wakati wa malezi yetu au ukuwaji wetu na kuyaishi na kama matokeo tuko jinsi tulivyo na mbaya zaidi tumeendelea kuyakumbatia badala ya kuachana nayo.
Mambo mengi hasi na ya kutudhorotesha kifedha tumeyabeba na kuyaamini na kuyaishi. Mifano ni ni mingi, wengine waliambia ng’ombe wa masikini hazai wakimaanisha kama wazazi wako ni masikini basi nawe lazima uwe masikini. Wengine waliaminishwa wa mbili havai moja wakimaanisha kama fungu lako ni la kukosa hata ufanye vipi wewe ni wa kukosa tu na mengine mengi unayoyajua na wengine wamekwenda mbali zaidi mpaka majina mengine watu wamepewa ya kukatisha tamaa kabisa kama vile kumuita mtoto kaburi na akiuliza anaambiwa wewe ni kuzikwa tu maana kila niliyezaa amekufa na sasa twakusubiria wewe na wewe pasi kujua unaamini unasubiria kufa na hata hujishughulishi. Mungu atusaidie.
Hebu tuangalie maandako matakatifu yanasemaje:-
Yeremia 31:29
Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi.

Ezekieli 18:1 – 2

Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Je! Maana yake ni nini hata mkatumia mithali hii katika Israeli, mkisema, Baba wamekula zabibu mbichi, nao watoto wakatiwa ganzi la meno?

Tambua jambo moja ya kuwa yale yaliyokuwa yakimuandama baba yako au mama yako kamwe hayawezi kukuandama wewe hiyo si kanuni ya Kimungu labda kama                     umejikabidhisha kwa shetani. Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa kumkubali Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako binafsi, tazama ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya. Alisema IMEKWISHA hakika alimaanisha alimaliza kila kitu pale msalabani. Mwamini Yesu Kristo uwe huru na mikatale ya shetani.
Chukua hatua kwa kuyakabidhi maisha yako kwa Yesu uwe huru na vifungo vilivyokukamatia kama matokeo ya kuaminishwa katika malezi yako ambayo sasa imekuwa shida. Jibu ni Yesu Kristo peke yake.
Jitenge na utumwa huo mkabidhi Bwana Yesu uwe huru.
Waamuzi 6:25 - 32
Waamuzi 6:25 Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;
Waamuzi 6:26 ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.
Waamuzi 6:27 Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama Bwana alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku.
Waamuzi 6:28 Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa.
Waamuzi 6:29 Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili.
Waamuzi 6:30 Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo.
Waamuzi 6:31 Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe hivi asubuhi; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake.
Waamuzi 6:32 Basi akamwita Yerubaali siku hiyo, akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa sababu ameibomoa madhabahu yake.

Acha kuzubaa ni wakati sahihi sasa wa kuachana na mambo yote uliyorithishwa kutokana na malezi na historia ya familia yako. Changamka wakati ni sasa, wewe ulikuja duniani huna photocopy wewe ni original.  Gideon alishughulika na madhabau ya nyumba ya baba yake kuhakikisha anaibomoa  ili tu aweze kufikia maono yake binafsi.
Waamuzi 6:15
Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.
Mstari huu unaonesha jinsi maisha yake na wazazi wake na namna alivyoaminishwa na kujikuta anashindwa kufikia ndoto zake na ndipo Mungu alimuamuru kuiharibu madhabahu ya baba yake iliyojengwa kwenye nyumba yao ili kuweza kuwa huru na kufurahia maisha ambayo Mungu alimuumbia. Je umegundua jinsi baba yake alivyo mkingia kifua mwanae, soma WAAMUZI 6:25-32 Hii inadhihirisha jinsi hata baba alivyokuwa na yeye amechoka na hali hiyo lakini alikuwa hana ujasiri.
Nakuomba kuanzia leo usikubali kunia machache, nenda kafanye makuu kwa utukufu wa Bwana Yesu. Mungu akubariki.

Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
             
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...