Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 31)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 31

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza MUNGU HATUPI UTAJIRI BALI HUTUPA NGUVU ZA KUTENGENEZA/KUPATA UTAJIRI.
Kumbukumbu la Torati 8:18

Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Acha maombi ya kumuomba Mungu akupe utajiri kwani Yeye hukupa uweza wa kupata utajiri. Sasa suala la kuutumia uwezo ulipewa ni suala lingine.

Kinachotokea ni kwamba una uweza ndani yako tayari ambao hautumiki na hiyo ndio maana u masikini. Tatizo hujautumia uweza uliopewa ndani yako.

Msingi au sehemu ya kuanzia kuanza kuutumia uweza uliopewa na Mungu ni pale unapofanya agano la kushikamana na Mungu katika maisha yako kwa kuyakabidhi maisha yako kwake ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako, ndio kitu cha kwanza na muhimu sana na si vinginevyo.

Nikijuacho mimi ni kwamba kila mwanadamu unayemwona mbele yako ana uweza wa ajabu ndani yake ambao haujaanza kutumika na akiishicho ni sehemu kidogo sana hata 1% haijafika.

Mchakato wa kuufikia uweza huo ni mchakato wa kila siku kidogokidogo, ukiendelea kujifunza na kutenda yaani utakuwa ukibadilika siku kwa siku. Kujifunza ndio mpango mzima na hakuna njia ya mkato ili kuuamsha uweza ulionao uweze kufurahia mafanikio ambayo Mungu amekupa uweza wa kuupata. Wakati mwingine itakupasa kusukumwa ili uanze kuutumia uweza ulio nao na bahati mbaya wengine hata hawajui kama wana uweza wa ajabu ndani yao.

Ili uweze kunielewa vizuri ngoja nikupe mfano ambao naamini ukiuelewa utajua jinsi ya kujiweka mahali sahihi:-

Palikuwepo na mfalme mmoja aliyetokea kuwa na binti mzuri  na ambaye alifikia umri wa kuolewa. Hivyo mfalme aliagiza mbiu ipigwe  kwa vijana wote wasiooa na wanataka kuoa ili awape mtihani na atakayefaulu atapewa dola 1,000,000 na kuozeshwa binti wa mfalme.

Siku ya siku umati wa vijana ulikusanyika na ndipo mfalme aliwapa huo mtihani ambao ulimuhitaji kijana kuweza kuvuka mto wenye kina kirefu na uliokuwa na sifa ya mamba mla watu. Mara baada ya kusema hivyo nusu ya vijana waliondoka pale pale na waliobaki wakawa wanatafakari namna watakavyoweza kupigana chenga na huyo mamba hadi kuvuka ng’ambo ya pili wakiwa salama na ghafla wakamuona kijana mmoja amejitosa. Huyu kijana alionekana kuwa standi wa kupiga mbizi na kuzama kumchanganya mamba na hatimaye kujikuta amevuka mto salama.

Shangwe na vigelegele kwa ustadi aliouonesha pia ujasiri wa kutohofia kufa. Alishangiliwa sana na ndipo mfalme alimwita ili amkabidhi cheque ya dola 1,000,000 na binti yake. Cha kushangaza kijana akawa analia anasema yeye hataki hizo dola wala huyo binti anachotaka ni aoneshwe ni nani aliyemsukumia mtoni bila ridhaa yake. Du kumbe alisukumwa si kwa ridhaa yake hata hivyo alishinda. Hata wewe unayesoma huu ujumbe yu mkini umeshindwa kufanya makubwa kwa kuwa hakuna wa kukusukuma ufanye. Anza leo kuhusiana na watu waliokuzidi uweze kusukumika. Mungu atusaidie.

Waefeso 3:20

Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

Ndugu yangu unayo nguvu ndani yako kuliko hata nguvu ya transformer, kazi kwako kuanza kuitumia hiyo nguvu ikusaidie kufanya makubwa. Tuwasiliane iwapo utapenda kujua zaidi.
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...