Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 32)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 32

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza MAMBO MAKUU MATATU UNAYOTAKIWA KUZINGATIA JUU YA FEDHA.

Tumejifunza mengi kuhusiana na masuala ya fedha na sasa ni muhimu tukajua mambo matatu yakayotusaidia kutuweka sawa linapokuja suala la fedha.

1. Elimu juu ya fedha – Itafurahisha kama utaweka kipaumbele kujikumbusha mara kwa mara juu ya hii elimu kwani kurudia rudia imethibitika kuwa ni njia bora kufanya jambo unalorudia kushikamana na ubongo wako wa ndani  (sub-conscious mind) na kusababisha utekelezaji wa jambo husika kuwa rahisi zaidi  kuliko kutorudiarudia. Sote tunahitaji hii elimu na ingewezekana mashuleni pia ifundishwe.

2. Kuipangilia fedha – Tabia ya kupata pesa na kuanza kuitumia ndio imetufikisha hapa tulipo. Mtu yeyote makini akipata tu pesa huipangilia katika mpangilio uliothibitika kuwa bora zaidi 30/70 na waweza ongeza kadri vyanzo vya pesa viongezekapo. Yawezekana ndio kwanza unasoma makala zangu kwa mara ya kwanza ila kwa wafuatiliaji wa Makala zangu wakisikia tu 30/70 tayari  wanajua mpangilio wa fedha:-

10% - Ni Dhaka kama u muumini na kama si muumini saidia makundi yenye uhitaji
10% - Tunza na ikifikia kiwango cha kuweza kuanzisha mradi itoe ulipoitunza na anzisha mradi. Hivyo hatutunzi fedha kwa lengo la kutunza bali twataka ifikie kiwango cha kuanzisha mradi ulio katika mpango. Inashauriwa kutunza sehemu ambayo si rahisi kuichukua kirahisi. Sehemu sahihi uanzapo utaratibu wa kutunza fedha (kusave) ni mfuko wa umoja (UTT) waulizie bank ya CRDB watakuelimisha au njoo inbox nikutumia elimu ya mfuko wa umoja. Hii itakusaidia kukujengea tabia ya kutunza bila kutoa toa mpaka ifikie kiwango utakacho.

10% - Hii ni maalum kwa kununua shares, tresurry bonds, tresurry bills nk ila bado nashauri kama ndio unaanza tabia hii adimu ni vyema ujiunge na mfuko wa Umoja (UTT) . Kimsingi ukiweza kutunza 20% kwenye mfuko wa umoja basi 10% itabaki kwenye mfuko na 10% utaichukua kuanzisha mradi.

3. NIDHAMU YA PESA – Kuna msemo mitaani unasema tumia pesa  mpaka ikutambue pia wengine husema tumia pesa utapata akili ya kuitafuta na mengine mengi yenye kuonesha utovu wa nidhamu juu ya fedha.
Fedha inahitaji nidhamu. Nidhamu ni kufanya kile ulichojipangia ya kuwa utafanya bila kujali hali. Ni msimamo thabiti wa utekelezaji mipango. Waweza jua elimu ya pesa na mipango ya fedha na bado ukashindwa kutekeleza na wakati  mwingine ukawa mwalimu wa elimu ya fedha lakini kwako ikawa mtihani kutekeleza. Hili ni tatizo kwa kila mwanadamu atakapo kuachana na tabia ya zamani na kuanzisha tabia mpya huwa ni ligi lakini penye nia pana njia. Hili ndilo la msingi sana katika maisha na hasa kama unataka mabadiliko ni lazima kufanyia kazi ulivyojifunza. Hata maandiko husema yeye ajuaye vingi kwake vingi vitahitajika. Pia biblia inasema yeye ajuaye kutenda mema na asitende atakuwa anatenda dhambi. Mungu atusaidie.
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...