Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 25
Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo.
Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Ukiyajua itakurahisishia ujiweke wapi ili uwe kivipi. Napenda kuita vitu vinavyokutengeneza au kukupa sura au mtazamo tunaouona tukuangaliapo na kuweza kukuelezea tukikutofautisha na wengine. Leo tunakwenda kuangalia jambo la pili linalomtengeneza mtu:-
MAZINGIRA – Mazingira aishiyo mtu yanamchango mkubwa wa ufahamu wa mtu na maendeleo yake. Mazingira hutengeneza akili ya muhusika. Ukiwa kwenye mazingira yaliyodorora pasi shaka akili nazo zitadorora.
Chukulia mfano wa mtoto wa miaka mitano aishie kariakoo na mtoto wa umri huo huo aishie bunyangomale huko Tukuyu. Pamoja na kwamba watoto hawa wana umri ulio sawia lakini ukiwaweka pamoja aishie kariakoo ataonekana mwenye maarifa sana kuliko wa bunyangomale. Tofauti uionayo imesababishwa na mazingira tofauti watokayo watoto. Naamii tunakwenda pamoja. Hata biblia inaafiki hili ya kuwa badiliko la mazingira huathiri ufahamu wa mtu,
• Unaishi wapi ina maana kubwa sana
• Wanafanyia kazi wapi ina maana kubwa sana
• Unaabudu wapi ina maana sana
Pia ukimchukua samaki aina ya papa ukamweka kwenye chombo cha kutunzia samaki nyumbani kama urembo majumbani ukuaji wake utaathiriwa sana na ukubwa wa chombo yaani mazingira uliyomuweka na uchache wa maji, lakini papa huyo huyo ukimuweka baharini utashangaa atakuwa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na alivyokuwa kwenye chombo cha kuweka samaki sitting room kama urembo.
Mwanzo 12: 1 - 4
Mwanzo 12:1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
Mwanzo 12:2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Mwanzo 12:3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Mwanzo 12:4 Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.
Kwa miaka sabini na mitano maisha ya Abrahamu yaliathiriwa na mazingira yake. Katika mazingira yake:
• Alikuwa amejitenga kiimani na Mungu
• Hakuwa na mtoto pamoja na kwamba alikuwa ameoa mke
• Aliishi chini ya mpango na kusudio la Mungu
• Aliishi chini na uwezo aliokuwa nao
• Alikuwa shujaa wa eneo wakati yeye ni shujaa wa ulimwengu
Ili Mungu aweze kumtumia, kumbariki na kumfanya kuwa baraka, Ilimlazimu Mungu kumuhamisha ili kukuza ufahamu wake katika mazingira tofauti.
• Kama ujapata taarifa mpya utabaki nyuma ya mambo.
• Kama hujahamasika unachakaa
• Kama hujaweza panda ngazi tafsiri yake unashuka
• Kama hujahabarishwa unakuwa umepotoka
• Kama mambo huyajui kwa kina hutaweza kuyaelezea kwa mtiririko
Kwa upande wa Abrahama ilimpasa kubadili mazingira, lakini kwa baadhi yetu tunahitajika kukua zaidi ya mazingira tuishio, hivyo badala ya mazingira kutuathiri, tunatakiwa tukuwe kuweza kubadili mazingira kutokana na upeo mkubwa tutakaoupata.
MWANZO 15:1 - 6
Mwanzo 15:1 Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.
Mwanzo 15:2 Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?
Mwanzo 15:3 Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Mwanzo 15:4 Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.
Mwanzo 15:5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Mwanzo 15:6 Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Miaka michache baadae ya kuharibikiwa tena, kazi kubwa ambayo Mungu aliifanya nikumpanua ufahamu ili kuweza kuwa juu ya mazingira. Aliambiwa aangalie juu mbinguni ili kuweza kuukuza ufahamu wake na hatimaye kumbadili mtazamo wake.
KAMWE USIRUHUSU MAZINGIRA YAKO YAKUAMULIE HATIMA YAKO. Jiendeleze upate kubadilika kimtizamo kiasi cha kuyabadilisha mazingira na si kubadilishwa na mazingira.
Kama kuna kazi kubwa mwanadamu aliyo nayo ni kukuza ufahamu wake kiasi cha kumfikisha mahala aweze kuwa juu ya mazingira. Hivyo haijalishi uko wapi mafanikio ni urithi wako kinachokusumbua ni upeo mdogo. Kujiendeleza ndio mpango mzima.
Penda mafunzo, penda kusoma vitabu vya watu waliokutangulia na kufanya makubwa hapa duniani upate kuamka na kuchukua nafasi yako. Hudhuria mafunzo hata ikibidi kulipia lipia. Sikiliza watu waliokutangulia. Ongea nao ana kwa ana utashangaa unabadilika ghafla na kuyatawala mazingira yako.
Mungu anasema UTABARIKIWA SHAMBANI UTABARIKI MJINI. MUNGU ATUSAIDIE.
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.
Maoni
Chapisha Maoni