Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 27
Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo.
Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la nne linalomtengeneza mtu:-
NANI RAFIKI YAKO/MAHUSIANO – Siku moja mkulima alikuwa mlimani na akabahatika kuyaona mayai ya tai na kubahatika kuchukua yai moja. Lengo alitaka kuona akichanganya na mayai ya kuku yakaatamiwa pamoja, je mwisho wa siku itakuwaje.
Ukweli ni kwamba mwisho wa siku kuku alitotoa mayai yote ikiwa ni pamoja na yai la tai. Hivyo vifaranga vya kuku na tai vikawa vikilelewa pamoja. Tai huyo mdogo
1. Aliishi sehemu ile ile vifaranga vingine vilpoishi
2. Naye alifanya kama vifaranga vya kuku vifanyavyo
3. Naye aliogopa kama vifaranga vya kuku vilivyoogopa
4. Alikula vile vifaranga vya kuku vilivyokula
5. Alifanya au alikuwa na tabia kama za vifaranga vya kuku
6. Alipata mateso yale yale yaliyowasibu vifaranga wa kuku
Kadri kimo kilivyoongezeka alianza kuona tofauti kati yake na vifaranga vya kuku.Siku moja alisikia kilio cha tai jike na ghafla kuna kitu toka ndani kikainuka kwa lugha nyingine niseme machale yalimcheza kayatanua mabawa yake, akaanza kupaa na akashangaa akienda mbali zaidi kuliko uwezo wa ‘wenzake’.
Nataka tujifunze kitu kimoja hapa. Huyu tai toka siku ya kwanza uwezo wa kupaa kuliko kuku ulikuwa ndani yake, lakini kule kuendelea kuhusiana na vifaranga vya kuku vilimfanya asione huo uwezekano ambao alikuwa nao ni mpaka siku ya siku ilipotokea na mengine yakabaki kuwa historia.
Mahusiano yako yamekuweka sehemu usiyostahili na kupotosha hatima yako katika maisha. Ni kujidanganya ya kuwa waweza kuwa na mahusiano maovu na kutegemea mwisho mwema. Nioneshe rafiki yako, nami nitakuelezea ulivyo, kama msemo usemavyo ndege watembeao pamoja huruka pamoja.
‘Kamwe huwezi kulala kwenye mapaja ya Delila na uamkie kwenye mabega ya Abraham.’
1 Wakorintho 15:33
Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Huwezi kubishana na ukweli mahusiano yako huaribu akili na hatimaye hatima ya maisha yako. Kuwa na busara na jichagulie marafiki kwa uangalifu si kila mtu wa kuhusiana naye.
USIRUHUSU MAHUSIANO YAKO YAKUHARIBIE HATIMA YAKO YA MAISHA.
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.
Maoni
Chapisha Maoni