Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 28
Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo.
Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la tano linalomtengeneza mtu:-
MAONO – Naona vyema nianze na maana ya maono, neno ambalo ni wingi likitokana na neon kuona. Wengi wanatizama bali hawaoni. Waweza kutana na watu wa jinsi mbili yaani kipofu na asiye kipofu na chakushangaza ni kwamba kipofu aweza kuona akashindwa kutizama kwa ajili ya upofu lakini asiye na upofu akaweza kutizama na kushindwa kuona.
Na kama ungaliambiwa chagua moja kati ya kuona na kutizama, basi kuona ni jambo la maana zaidi kuliko kutizama.
Ukifumba macho taswira utakazoanza kuziona ndani yako itamaanisha uko kwenye hatua ya kuona na si kutizama. Kifupi kuona ni taswira zipatikanazo kwenye akili/ufahamu wako na kutizama ni nje ya akili zako. Hivyo kuna macho ya akili na vivyo hivyo macho ya mwilini.
Ukitaka kutanua uwezo wako wa kuona, naomba nikupe zoezi yafuatayo:-
Orodhesha matamanio yako bila kujali uwezo au fedha ulizo nazo. Kifupi chukulia fedha si tatizo ungetamani mambo gani 100. Kama u mwanafunzi mzuri mfuatiliaji nikuombe ufanye hii kazi ya kuorodhesha matamanio yako angalau 100 ukichukulia fedha si tatizo kabisa na tuwasiliane kwa hatua zaidi.
Naomba niendelee kwa mfano ufuatao:
Siku moja bwana mmoja alinisimulia hadithi ya kwamba alipokuwa baharini aliwaona watu wakivua samaki kwa kutumia ndoana. Kati ya hao watu alikuwapo mtu mmoja aliyekuwa na kijiti kifupi mkononi na kila akipata samaki ni lazima ampime kwenye kile kijiti na kama alionekana samaki ni mrefu kuzidi kijiti alimrudisha baharini ila kama samaki alikuwa sawia au pungufu ya kijiti huyo aliweza kumuweka kwenye chombo cha samaki wa kwenda nao nyumbani. Tendo hili lilivuta udadithi kiasi kwamba aliyekuwa akiona kitendo hicho alimsogelea na kumuuliza kwa nini baadhi ya samaki anawarudisha baharini? Jibu alilopewa ni kwamba kabla ya kuja kuvua samaki aliamua kupima kikaangio chake na urefu wa kijiti ndio sawa na kikaangio cha samaki na hivyo haoni sababu ya kubeba samaki mwenye kuzidi kikaangio chake ni bora kumrudisha tena baharini. Unajifunza nini hapo?
Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Wengi wetu tuko sawa na mvuvi mwenye kijiti cha kupimia samaki sawia na kikaangio chake. Kwa nini umekuwa na malengo uliyonayo? Wengi wameangalia vikaangio vyao. Wengine husema uwezo wangu nikijibana ni kununua baiskeli basi zaidi ya hapo siwezi. Huu ni mmoja ya usemi ya baadhi yetu kisa ameangalia uwezo alionao kwa sasa maana ni muuza chipsi mayai na hivyo hawazi kabisa kumiliki jet kisa uwezo mdogo (kikaangio).
Naomba nikujuze kitu ambacho hukijui, wewe una uwezo wa ajabu ndani yako kiasi cha kununua mji mzima wa Dar es Salaam, na huo uwezo uko ndani yako na zaidi ya kununua mji mzima wa Dar es Salaam uko ndani yako. Hakuna mwanadamu aliyezaliwa kihasara kila mmoja wetu ana uwezo wa ajabu kuliko alivyo na kwa taarifa yako unaishi chini ya asilimia 1% ya uwezo ulio nao.
Kitu kikubwa ni kuanza taratibu kuuamsha uwezo wako na njia rahisi ni kujisomea vitabu sahihi na kuyatekeleza ujivunzayo, kuwasikiliza watu sahihi na kutekeleza wakuambiayo, kuhudhuria mafunzo sahihi taratibu utaanza kushangaa utakavyo anza kuyafanya na wengine watakuita una bahati. Asikudanye mtu hakuna cha bahati hapo. Mambo niliyo kutajia yatakusaidia kupata ufumbuzi wa mambo mengi ya maisha kuhusu kufanikiwa kwako.
Mithali 29:18
Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
ACHA KUJIPIMIA KIDOGO SABABU YA KIPAKULIO ULICHO NACHO NI KIDOGO KUMBUKA MUNGU AMEKUPA VINGI KUPINDUKIA JAPO HUVIONI.
Naomba nikushauri soma vitabu hivi vitano vitakusaidia sana kuamsha uwezo uliojificha ndani yako:-
1. Incognito By David Eagleman
2. Phantoms in the Brain By V.S. Ramachandran
3. The Tell-Tale Brain By V.S. Ramachandran
4. Making a Good Brain Great By Daniel Amen
5. The Female Brain By Louann Brizendine
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.
Maoni
Chapisha Maoni