Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 29
Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.
Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo.
Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la tano linalomtengeneza mtu:-
NENO LA MUNGU – Kama kuna jambo hutengeneza ufahamu basi ni neno la Mungu, Ukilipa nafasi neno la Mungu katika maisha yako basi nalo neno hukupa nafasi stahiki katika nchi uishiyo.
2 Timotheo 2:15
Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.
Ushauri kwako msomaji, nakushauri fanya mojawapo au yote yafuatayo ila moja au mbili lazima viwemo kwenye uchaguzi wako:-
1. Hakikisha unaisoma biblia yote ndani ya waka mmoja
2. Soma sura moja ya kitabu cha mithali kila siku
3. Fikia kasi ya kujisomea kitabu kimoja chotchote sahihi kila wiki
Mungu atusaidie tukifikia nidhamu ya kutenda mambo hayo yote matatu tutabaki tukijishangaa jinsi tutakavyomchukulia Mungu katika maisha yetu. Tutafikia hatua ya kumuona Mungu ndio thamani pekee kubwa tuliyonayo kuliko chochote kwa kumuishi na si kumuongelea.
BORESHA MAISHA YAKO KWA KULIISHI NENO LA MUNGU
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.
Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.
Maoni
Chapisha Maoni