Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 33)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 33 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza umuhimu wa mizania katika mafanikio. Tumejifunza mengi kuhusiana na masuala ya fedha na sasa ni muhimu tukajua umuhimu wa mizania katika mafanikio. Kikubwa ninachotaka kukufahamisha leo ni kuwa mafanikio sahihi ni lazima yawe yametokana na uwekezaji wa kiroho na uwekezaji halisia unaoweza onekana kwa macho ya nyama. Ni ujinga kujikita kwenye mambo ya kiroho 100% ikiwa ni pamoja na utoaji wa fungu la kumi kwa uaminifu ati kwa kuwa imeandikwa utabarikiwa kwa kuwa mwaminifu na kubaki umekaa na kusubiria baraka zimwagike. UTASUBIRI SANA na ndipo utaanza kujiuliza na kuona kama Mungu amekuacha. Hivi unawezaje mfano kuwa mwaminifu wa fungu la kumi na kushindwa kuwa mwaminifu wa kuwekeza 10% kwa uaminifu kama ilivyo kwa fungu la kumi na ukafuata kanuni zote za kufanikisha, na uone kama...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 32)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 32 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza MAMBO MAKUU MATATU UNAYOTAKIWA KUZINGATIA JUU YA FEDHA. Tumejifunza mengi kuhusiana na masuala ya fedha na sasa ni muhimu tukajua mambo matatu yakayotusaidia kutuweka sawa linapokuja suala la fedha. 1. Elimu juu ya fedha – Itafurahisha kama utaweka kipaumbele kujikumbusha mara kwa mara juu ya hii elimu kwani kurudia rudia imethibitika kuwa ni njia bora kufanya jambo unalorudia kushikamana na ubongo wako wa ndani  (sub-conscious mind) na kusababisha utekelezaji wa jambo husika kuwa rahisi zaidi  kuliko kutorudiarudia. Sote tunahitaji hii elimu na ingewezekana mashuleni pia ifundishwe. 2. Kuipangilia fedha – Tabia ya kupata pesa na kuanza kuitumia ndio imetufikisha hapa tulipo. Mtu yeyote makini akipata tu pesa huipangilia katika mpangilio uliothibitika kuwa bora zaidi 30/70 na waweza ...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 31)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 31 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza MUNGU HATUPI UTAJIRI BALI HUTUPA NGUVU ZA KUTENGENEZA/KUPATA UTAJIRI. Kumbukumbu la Torati 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. Acha maombi ya kumuomba Mungu akupe utajiri kwani Yeye hukupa uweza wa kupata utajiri. Sasa suala la kuutumia uwezo ulipewa ni suala lingine. Kinachotokea ni kwamba una uweza ndani yako tayari ambao hautumiki na hiyo ndio maana u masikini. Tatizo hujautumia uweza uliopewa ndani yako. Msingi au sehemu ya kuanzia kuanza kuutumia uweza uliopewa na Mungu ni pale unapofanya agano la kushikamana na Mungu katika maisha yako kwa kuyakabidhi maisha yako kwake ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako, ndio kitu cha kwanza na muhimu sana na si vinginevyo. Nikijua...

SOMO JUU YA FEDHA/SHEKELI (SEHEMU YA 30)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 30 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo. Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la saba linalomtengeneza mtu:- ROHO MTAKATIFU – Mkristo katika makuzi yake ya kiroho kuna hatua anapitia zilizo muhimu, hatua ya kwanza ni hatua anayoifikia kuujua ukweli ya kwamba hawezi kumpendeza Mungu pasipo kuukubali mpango wa Mungu wa ukombozi kupitia Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa Maisha yetu. Kila mwanadamu chini ya jua hana budi kutubu dhambi zake na kumpokea Yesu  Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha binafsi. Baada ya hapo ubatizo wa maji hufuata japo si utaratibu rasmi kwa kuwa mtu aweza kumpokea Yesu Kristo na kubatizwa kwa Roho Mtakatifu kabla ya ubatizo wa maji. Hivyo hatua hii ya ...

SOMO JUU YA FEDHA/SHEKELI (SEHEMU YA 29)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 29 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo. Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la tano linalomtengeneza mtu:- NENO LA MUNGU – Kama kuna jambo hutengeneza ufahamu basi ni neno la Mungu, Ukilipa nafasi neno la Mungu katika maisha yako basi nalo neno hukupa nafasi stahiki katika nchi uishiyo. 2 Timotheo 2:15 Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. Ushauri kwako msomaji, nakushauri fanya mojawapo au yote yafuatayo ila moja au mbili lazima viwemo kwenye uchaguzi wako:- 1. Hakikisha unaisoma biblia yote ndani ya waka mmoja 2. Soma sura moja ya kitabu cha mithali kila siku 3. Fikia kasi ya kujisome...

SOMO JUU YA FEDHA/SHEKELI (SEHEMU YA 28)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 28 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo. Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la tano linalomtengeneza mtu:- MAONO – Naona vyema nianze na maana ya maono, neno ambalo ni wingi likitokana na neon kuona. Wengi wanatizama bali hawaoni. Waweza kutana na watu wa jinsi mbili yaani kipofu na asiye kipofu na chakushangaza ni kwamba kipofu aweza kuona akashindwa kutizama kwa ajili ya upofu lakini asiye na upofu akaweza kutizama na kushindwa kuona. Na kama ungaliambiwa chagua moja kati ya kuona na kutizama, basi kuona ni jambo la maana zaidi kuliko kutizama. Ukifumba macho taswira utakazoanza kuziona ndani yako itamaanisha uko kwenye hatua ya kuona na si kutizama. Kifupi kuona ni taswira zipatik...

SOMO JUU YA FEDHA/SHEKELI (SEHEMU YA 27)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 27 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo. Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la nne linalomtengeneza mtu:- NANI RAFIKI YAKO/MAHUSIANO – Siku moja mkulima alikuwa mlimani na akabahatika kuyaona mayai ya tai na kubahatika kuchukua yai moja. Lengo alitaka kuona akichanganya na mayai ya kuku yakaatamiwa pamoja, je mwisho wa siku itakuwaje. Ukweli ni kwamba mwisho wa siku kuku alitotoa mayai yote ikiwa ni pamoja na yai la tai. Hivyo vifaranga vya kuku na tai vikawa vikilelewa pamoja. Tai huyo mdogo 1. Aliishi sehemu ile ile vifaranga vingine vilpoishi 2. Naye alifanya kama vifaranga vya kuku vifanyavyo 3. Naye aliogopa kama vifaranga vya kuku vilivyoogopa 4. Alikula vile vifaranga ...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 26)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 26 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo. Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la tatu linalomtengeneza mtu:- UMEZUNGUKA NCHI YAKO/DUNIA KWA KIWANGO GANI? – Kitendo cha kuzalia, kukulia, kusoma na kisha maisha katika nchi yako bila kuona sehemu nyingine ya dunia ikoje kumembupaza wengi na mbaya zaidi wengine wamezaliwa kijiji X wamesoma kijiji X wameoa kiji X na maisha yote hadi kuzeeka na kufa wangali kijiji X. Niambie mtu wa jinsi hiyo atakuwaje kuchukulia mambo maana ayajuayo ni ndani ya mipaka yake na wala hajui upande mwinge wa dunia mambo yakoje. Watu wa jinsi hii wameishia na maisha yasiyoridhisha na kuwa na mtazamo usiozidi mipaka yao. Mithali 4:7 Bora hekima, basi jipatie heki...

SOMO JUU YA FEDHA/SHEKELI (SEHEMU YA 25)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 25 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo. Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Ukiyajua itakurahisishia ujiweke wapi ili uwe kivipi. Napenda kuita vitu vinavyokutengeneza au kukupa sura au mtazamo tunaouona tukuangaliapo na kuweza kukuelezea tukikutofautisha na wengine. Leo tunakwenda kuangalia jambo la pili linalomtengeneza mtu:- MAZINGIRA – Mazingira aishiyo mtu yanamchango mkubwa wa ufahamu wa mtu na maendeleo yake. Mazingira hutengeneza akili ya muhusika. Ukiwa kwenye mazingira yaliyodorora pasi shaka akili nazo zitadorora. Chukulia mfano wa mtoto wa miaka mitano aishie kariakoo na mtoto wa umri huo huo aishie bunyangomale huko Tukuyu. Pamoja na kwamba watoto hawa wana umri ulio sawia lakini ukiwaweka pamoja aishi...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 24)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 24 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo. Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Ukiyajua itakurahisishia ujiweke wapi ili uwe kivipi. Napenda kuita vitu vinavyokutengeneza au kukupa sura au mtazamo tunaouona tukuangaliapo na kuweza kukuelezea tukikutofautisha na wengine. Mambo yanayomtengeneza mtu na haya yafuatayo: MALEZI/HISTORIA YA FAMILIA ULIYOKULIA – Wengi wetu tumejikuta matatani kifedha kutokana na mambo tuliyo yachukua kwenye familia na mazingira tuliyokulia  wakati wa malezi yetu au ukuwaji wetu na kuyaishi na kama matokeo tuko jinsi tulivyo na mbaya zaidi tumeendelea kuyakumbatia badala ya kuachana nayo. Mambo mengi hasi na ya kutudhorotesha kifedha tumeyabeba na kuyaamini na kuyaishi. Mifano ni ni mingi,...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 23)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 23 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya ufikiri sahihi linapokuja suala la kuitawala fedha/shekel na udhibiti juu ya matumizi na nikuombe endelea kunifuatilia:- . Ufikiri sahihi juu ya fedha:- Ninapoongelea juu ya ufikiri sahihi juu ya fedha ninamaanisha ile hali itakayokupelekea kupata badiliko zuri kimaisha ikiwa ni pamoja na kuidhibiti pesa uipatayo isikupokonyoke na izidi kujiongeza. Hapa natamani upate kunielewa vizuri maana ni ukombozi si kwako tu bali familia na jamii inayokuzunguka. Nitakuwa sikutendei haki nisipokueleza ukweli ya kuwa msingi wa kufanijiwa/kutajirika katika maisha haya tuliyo nayo ni katika KUMJUA YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA. KINACHOTAKIWA NI KUYAKABIDHI MAISHA YAKO KWA YESU KRISTO AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO. HILI NI LA MUHIMU NA LA KWANZA NA USIPOLIZINGATIA, MAFUNDISHO YANGU ...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 22)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 22 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea na kumalizia aina ya nne ya sumu juu ya uwekezaji. Leo naanza kuongelea aina ya tano na nikuombe endelea kunifuatilia:- . 5.   Utajiri/Dhana ya  mali/vitu kuwa ndio utajiri Kama unadhani ukijilimbikizia mali ndio utajiri naomba nikupe pole kwani hiyo pekee ni ubinafsi na utakutesa sana. Ninapoongelea mafanikio namaanisha kuacha alama, kugusa maisha ya watu wengine. Huwezi kujiita umefanikiwa kama huna mawazo ya kugusa jamii kwa mahitaji mbalimbali. Huu ndio utajiri wa kweli kufanyika baraka kwa watu wengine. Siri kubwa ya kufanikiwa ni kuelewa kwa kina dhana ya uwekezaji – Hapa msisitizo ni kwamba unawaza chochote upatacho utawezaje kukizidisha na wala si kupanga matumizi. Napenda hapa twende p...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 21)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 21 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea na kumalizia aina ya tatu ya sumu juu ya uwekezaji. Leo naanza kuongelea aina ya nne na nikuombe endelea kunifuatilia:- . 4.   Utumishi wa Umma/Dhana ya mshahara Aina ya nne ya sumu ya uwekezaji ni dhana ya utumishi wa uma/mshahara. Wengi wamejikuta katika dimbwi la umasikini kwa sababu maisha yao yote wamekuwa wakiishi kwa kumtegemea boss, mwajiri, au serikali ili kupewa mshahara kwa lengo la kutajirika siku za usoni. Amka acha kulala! • Boss wako si asili ya mafanikio yako bali ni chanzo cha kuhakikisha unatumika kumfanikishia. • Ajira yako vivyo hivyo kamwe haiwezi kukufanikisha labda kama utakuwa kwenye ngazi maalum (executives) bali ajira yako inakuimarisha kuwa mtumwa mstaarabu. Wewe ni kutumi...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 20)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 20 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea aina mbili za sumu juu ya uwekezaji. Leo tunaendelea na nikuombe endelea kunifuatilia:- . 3. KUJIHALALISHIA/DHANA YA UMILIKI – Katika kuongelea aina hii ya tatu, Makala iliyopita nilimalizia kwa kusema:- ‘Swali linasema unataka kuwa mzima? Hebu angalia jibu la mgonjwa kwa swali la Bwana Yesu - Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Je swali na jibu vina uhusiano? Kinachoonekana kwa huyu mgonjwa ni kwamba alikwisha jihalalishia ya kuwa kupona kwake asahau kwa hiyo akawa mmiliki wa ugonjwa wake na kwamba haiwezekani yeye kupona. Unaiona hatari ya kujimilikisha inavyotesa watu. Kwa Jina la Yesu naomba usiwe...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 19)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 19 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. Makala iliyopita tuliongelea aina mbili za sumu juu ya uwekezaji. Leo tunaendelea na nikuombe endelea kunifuatilia:- . 3. KUJIHALALISHIA/DHANA YA UMILIKI – Aina hii ya tatu inapaswa kushughulikiwa na kuondokana nayo kabisa. Kujihalalishia au kujiona wewe ndiye mmiliki wa jambo fulani baya imeathiri wengi. Akili ya kujidhania/kujisikia kila wakati ya kuwa wewe ndiye mwenye kustahili kuwa na hali mbaya, kuishi maisha magumu na kujidhania ya kuwa yuko mtu anayekusababishia kuwa na hali uliyonayo na kuomba atoweke duniani ndipo utapata unafuu. Ukweli ni kwamba hakuna mtu awazaye kukufanya ushindwe pasipo wewe mwenyewe kuruhusu, hivyo chochote unachoruhusu kwenye maisha yako ndicho unachopokea. Dalili ya watu wa aina hii ni wale wote wenye kila wa...

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 18)

Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 18 Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku. Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli Leo tunakwenda kujifunza juu ya AINA 5 ZA UFAHAMU ULIOTIWA SUMU JUU YA UWEKEZAJI. . 1. AKILI YA KUHAMAHAMA – Kama kuna kitu cha kushughulikia kuondokana nacho basi ni hii hali ya mtu kutotulia kubaki kutangatanga yaani kutokuwa na jambo au kitu maalum kukifanya bali ni kushika hiki na kukiacha kisha kukimbilia kingine. Watu wenye tabia hii ni vigumu hata kujua wanasali wapi maana hawaachi kuhama hama mara leo huku kesho kule  na inaathiri hata kutulia kituo kimoja cha kazi ni kila wakati kubadili sehemu ya kazi na hata ukifuatilia sababu za kuacha kazi hapa na kwenda pale utakuta hazina mashiko. Kifupi hii ni roho inayomwendesha mtu kumuongoza kutotulia au kuwa na maisha yasiyo mipaka, maisha yasio na mwelekeo au kusuduo. Tabia za watu wa aina hii ni mbili kuu:- i. Hawana mahali maalum – Ni watu wa kutangatanga kut...