Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Majengo, biashara kubwa, viwanja vizuri vya mpira na mengine mengi ambayo wengine huita maajabu ya dunia ni matokeo ya mawazo. Ninachotaka kusema ni kwamba kila mtu ana mafazo ambayo akiyafanyia kazi maisha hayatakuwa kama yalivyo sasa. Mtihani mkubwa ni jinsi ya kuyapata mawazo yako ambayo yako ndani yako mithili ya madini. Wote tunatambua madini si rahisi kuyapata ni mpaka nguvu ya ziada itumike maana hukaa chini sana na mengi ya madidini kama sio yote yako chini ya miamba. Watu hulazimika kununua mitambo ili tu waweze kufikia madini. Kifupi si lelemama. Vivyo hivyo kwa mwanadamu ili kukutana na mawazo kuntu yaliyomo ndani yake, ni lazima afanye kazi ya ziada. Yawezekana umejaribu mawazo mengi kufanyia kazi lakini mambo bado hayajabadilika. Hii haimaanishi ya kuwa wewe huna m...