Tunaishi katika dunia ambayo kila mtu na mapito yake na kwa viwango tofauti. Ukweli wa mambo ni huu – Wako watu ambao maisha yao yamebeba maonyo juu ya maisha. Ukipata nafasi kuwasikiliza juu ya yale waliyoyapitia na yaliyowasibu kama matokeo au zawadi ya kufanya waliyofanya; Utakuwa umeonyeka kutothubutu kuyafanya hayo uliyo yasikia na ndio maana wahenga walisema ‘Asiyesikia la mkuu huvunjika guu’. Lakini upande wa pili wa shilingi tunapata mafundisho ya kuzingatia kupitia maisha ya watu. Kitu kimoja cha kushangaza ni kwamba hakuna binadamu asiye na stori ya kukueleza. Kikubwa tu stori yake yaweza kuwa onyo au fundisho, na yote unayahitaji ili uwe na maisha yenye mizania. Udhoefu wa watu waweza okoa maisha yako ya ndoa ambayo inakaribia kuvunjika (divorce). Udhoefu wa watu waweza kukuokoa na kiharusi. Udhoefu wa watu waweza kukuokoa na maisha duni ambayo umeyaishi miaka nenda miaka rudi. Udhoefu wa watu ni madini ya ajabu katika kuboresha maisha na ndio maana mafunzo yako ya pan...