Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Utaambulia nini kwenye Wazo la Leo?

Utaambulia nini kwenye Wazo la Leo? Jifunze kutambua vitu muhimu kwenye maisha yako kwanza. Vingine ni vya ziada. Hiyo yaweza kuwa siri ya maisha bora hapa Duniani. Kupokea na Kutoa ni kama watoto mapacha. Siku zote wanaongozana pamoja haswa wanapokuwa wadogo. Leo hii tunaishi kwenye Dunia yenye fursa mbalimbali. Fursa hizo zinatubariki na pia tunazitumia kubadili wengine. Ni sawa na kusema tunapokea na pia kutoa. Haijalishi ni fursa gani iko mbele yako, kama ni kusoma, kazi, kupata mwenza au hata kitu chochote ukipendacho kinachokupatia maarifa kama vile Karakana ya Ubongo, hizo zote ni fursa. Madhalani tunapenda kuishi. Tufikirie pamoja maswali ya kujiuliza ili tufanye majaribio (Experiments). Tusipende sana kukimbilia majibu maana ni njia rahisi zaidi ya kujiua. Haswa jibu linapokuwa siyo lenyewe . Ni vizuri kutambua ya kuwa, hata unapokuwa umeshapata jibu la kwanza, endelea kufikiri ili upate jibu la pili, tatu, nne na kuendelea ili usiwe Mfu. Ipe akili isiyoonekana kazi ya ...

Namna ya kutengeneza na Kuishi maisha Bora

Utaambulia nini kwenye Wazo la Leo? Jifunze kutambua vitu muhimu kwenye maisha yako kwanza. Vingine ni vya ziada. Hiyo yaweza kuwa siri ya maisha bora hapa Duniani. Kupokea na Kutoa ni kama watoto mapacha. Siku zote wanaongozana pamoja haswa wanapokuwa wadogo. Leo hii tunaishi kwenye Dunia yenye fursa mbalimbali. Fursa hizo zinatubariki na pia tunazitumia kubadili wengine. Ni sawa na kusema tunapokea na pia kutoa. Haijalishi ni fursa gani iko mbele yako, kama ni kusoma, kazi, kupata mwenza au hata kitu chochote ukipendacho kinachokupatia maarifa kama vile Karakana ya Ubongo, hizo zote ni fursa. Madhalani tunapenda kuishi. Tufikirie pamoja maswali ya kujiuliza ili tufanye majaribio (Experiments). Tusipende sana kukimbilia majibu maana ni njia rahisi zaidi ya kujiua. Haswa jibu linapokuwa siyo lenyewe . Ni vizuri kutambua ya kuwa, hata unapokuwa umeshapata jibu la kwanza, endelea kufikiri ili upate jibu la pili, tatu, nne na kuendelea ili usiwe Mfu. Ipe akili isiyoonekana kazi ya ...

Mazingaombwe ya Kukopi na Kupesti

Mazingaombwe ya Kukopi na Kupesti Yanahitaji Ufanye Uchunguzi (Experiment). Wewe uko wapi sasa? Uko ndani ya Gari ipi? Mdogo mdogo Gari ya Karakana ya Ubongo inasogea. Hatuhitaji kujiongezea dopamine iliyo nje ya mwili ili upate stimu ya kusonga mbele. Inawezekana kuwa mjanja bila dopamine ya vitu kama kulewa na madawa ya kulevya. Watu wengi wenye magonjwa mbali mbali yanayosumbua sana wanahitaji kuacha kujiongezea dopamine kienyeji. Tusipobadilika sisi wenyewe hakuna kitu chochote nje yetu kitakachodubadilisa. Hata ujiongezee dopamine kiasi gani. Ni suala la kujijengea tabia stahiki kama vile kwenda kitandani kulala ukiwa vizuri zaidi ya jana yako (Go to bed smarter than yesterday). Mwandishi maarufu wa Tanzania ambaye ameandika kitabu cha Kusudia Kuwa Wewe, Bwana Lameck A. Hulilo huwa anapendelea kusema: ‘Inawezekana. Hebu jitafutie hicho kitabu uone jinsi unavyoweza kufanya mazingaombwe ya kuwa ulivyokusudiwa kuwa bila ku-kopi na ku-pasti walivyo wengine. Bila kutumia...

Mazingaombwe ya Bahari Mbili

Mazingaombwe ya Bahari Mbili: Wanakarakana ya Ubongo! Mwaka ni mpya bado. Leo ninaongelea mazingaombwe yanayotokea kwenye mazingira yanayotuzunguka. Kuna Bahari mbili humu Duniani ambazo maji yake yanatokea Mto Jordan. Bahari ya kwanza inaitwa "Dead Sea" kwa lugha ya wenzetu. Au Bahari Mfu kwa lugha yetu. Hii Bahari Mfu japo ni Bahari lakini imekaa kama Ziwa. Inasemekana kwamba maji yake yana chumvi nyingi sana kiasi kwamba hakuna kiumbe chochote kile kinachoweza kuishi kwenye maji hayo. Hakuna cha Samaki wala Mamba wala Nyangumi, wala uhai mwingine wowote kama vile mimea ya Baharini vinavyoweza kustahimili hicho kiasi cha chumvi ya maji ya Bahari Mfu. Na ndo uhalisia wa hilo jina lake. Wataalamu wanatuambia chumvi iliyomo ndani ya Bahari Mfu ni nyingi kiasi kwamba hata mwili wa binadamu unaelea kwa urahisi kabisa. Kiwango cha hiyo chumvi ni mara kumi zaidi ya viwango vya chumvi vilivyomo kwenye maji ya Bahari nyingine unazozijua wewe. Bahari nyingine inaitwa Galilee. ...

Mazingaombwe ni sehemu ya Maisha! Chagua yale yenye Manufaa kwako.

Wana Karakana ya Ubongo! Jana niliongelea jambo moja kuhusu namna ya kusoma akili za watu kwa kutumia kitu nilichokiita mazingaombwe. Kuna siri kubwa ndani ya kufanya mazingaombwe. Pia unahitaji ujuzi wa hali ya juu. Kwa maana hiyo wale wanaoifanya kazi hiyo hutumia muda mwingi sana kujifunza. Huwezi kukurupuka na kujua siri hizo kwa siku moja. Siku hizi kuna Talk za Shows ambazo zinaonyesha siri za matukio mbalimbali ya mazingaombwe. Hata watoto kwenye baadhi ya mashule wanafundishwa mbinu ndogo ndogo kwa njia ya Hesabu, sarafu na karata. Mfano wanafundishwa namna ya kufanya sarafu itokomee kusikojulikana na pia ikaonekanie mahali pengine. Ni aina ya burudani kama hujui siri ya kinachofanyika. Pia wanatumia karata kusoma ubongo wa mtu kumwambia karata aliyofikiria kwenye akili yake. Kuna wakati kama mtu sio mzoefu anaweza kukosea. Kwa hiyo unatakiwa umakini mkubwa. Kwenye moja ya Talk shows, kuna mwana mazingaombwe mmoja ambaye anafanya mazingaombwe yake halafu anaonyesha mbinu...

Mikono Yangu

Mikono inayoonekana niliyo nayo ni miwili tu. Leo nataka nifanye mazingaombwe ya ukocha, tafadhali ambatana nami. Mikono yangu isiyoonekana inaweza ikawa mingi au michache. Ninaendelea kujipima kama kocha. Je, kuna chochote ambacho umekifanya kwa utofauti na ukaona matunda na faida ya Gari yetu ya Karakana ya Ubongo? Nitafurahi kama utanipa mrejesho sahihi. Unaweza kuutoa hapa au hata inbox. Kwa kawaida, bado mwaka ni mpya na ninaendelea kukutakia Heri ya Mwaka Mpya wa 2018. Mwaka ambao tunabadilisha malengo yetu kiutendaji yawe mazuri kutekelezwa kwa kujenga tabia stahiki. Mazingaombwe yangu ya leo ni uvumbuzi wa aina yake kwa ajili ya ku-copy na ku-paste yenye faida. Mifumo yetu, masoko yetu na ugunduzi ni vitu ambavyo inabidi kuvitengeneza. Jana nimeona Mwana-Karakana aliyejitambulisha ni Mwalimu wa Piano japo ana shahada ya ugavi na manunuzi. Nikajiuliza ni kitu gani kimemsukuma ajitambulishe wakati sijatuma siku nyingi ile meseji ya namna ya kujitambulisha. Nikafanya utafi...

Mikono Isiyoonekana!

Bado tunafurahia mwaka mpya kwa namna ya kipekee kabisa. Nikiwa Kocha ninapenda kufanya kitu kinaitwa "walk the talk." Kuna Wataalamu wanasema ili kujenga tabia ni lazima urudie rudie kufanya kitu angalau siku zisizopungua ishirini na moja (21). Ila kwa wale wenye nia na dhamira nzito inachukua masaa ishirini (20) kujitengenezea tabia fulani. Mikono isiyoonekana itatumikaje kwa siku hii ndani ya Wazo la Leo? Ukizingatia jana Nilikuuliza swali, " Je, mikono yako inatumika vizuri?" Bado ninajijengea tabia kama Kocha niweze kutumia mikono yangu inayoonekana na pia ile isiyoonnekana. Nimefurahishwa na Mwana-Karakana huyu aliyetumia mikono ya kuandika yafuatayo: "Mimi leo nina watu wawili watajiunga kwenye kundi hili" Ninaweza kusema kwamba mikono yake ni sehemu ya mikono ya Kocha wenu isiyoonekana. Je, wewe una mikono mingapi isiyoonekana? Je, inafanya kazi vizuri? Tafakari! Chukua hatua pia. Ninaamini kama umetafakari vizuri utagundua mimi kocha wa...