Leo nimeonelea vyema tukumbushane ya kuwa hatupo hapa duniani milele. Sote tu wapitaji na sijui kama umewahi kujiuliza hili swali ya kwamba siku moja utatoweka. Ukilijua hili vizuri hutakuwa na muda wa kupoteza maana kifo hakina taarifa wala kanuni. Hivyo kila siku akupayo Mungu hakikisha unajipangia kufanya vitu kana kwamba kesho hutakuwepo. Hili litakufanya uwaguse watu wengi Zaidi katika uwepo wako duniani. Utalazimika kuishi maisha yenye maana na kuwa mwangalifu kwa mengi ili uache alama utakapokuwa haupo. Napenda msemo anaoutumia Joel Nanauka ya kwamba ulikuja duniani binafsi lakini yakupasa kuondoka ukiwa taasisi akimaanisha taasisi si ya mtu mmoja bali ya wengi. Hivyo kuondoka kwako kuache mazungumzo kwa wengi kwa jinsi ulivoyagusa maisha yao na hapo ndipo unakuwa taasisi na sio tena mtu binafsi. Maisha ni mafupi. Ishi kila siku kwa utimilifu wake (Live full today). Kuwa bora kuliko katika kila jambo ulifanyalo. Kujua utakufa itakujengea kukumbushwa utakapoondoka watak...